Wafanyakazi 134 wakutwa na vyeti feki hospitali ya Muhimbili, majina yao haya

Angalia vuzuri mkuu, hapo wapo na madobi (DHOBI I &II)
Duh! Hiyo kali mkuu. Hilo ndilo tatizo ninaloliona nchini kwetu, hata dobi awe na cheti cha form 4? Kuna haja gani ya kuwapumzisha watoto waliofeli std 8 kama mpaka msuguwaji bedsheets awe na cheti cha form 4? Kama ni kusoma detergents na chemicals anazotumia, hata supervisor wake anaweza kumsomea na kumpa maelekezo!
 
Nasema hivi naungana na mhe raisi acha waenda zao, msiteteeee vitu ambavyo havina msingi, hata Kama anategemewa na watu mia tano kama alifoji Cheti wacha aende, hivi Unategemea mtu hana taaluma yoyote Alafu anakuja anatoa matibabu kwa mgonjwa, hebu tuweni sirias acha waenda wakatafute maisha kwingine, ili wataalaumu wenye vigezo waachiwe wafanye kazi, hii ni sekta nyeti Sana ya afya hua Unacheza na maisha ya watu hivyo hapatakiwi mambo yasiyo ya kitaalamu.
Mtu Amesoma miaka kutafuta Cheti hadi akahitimu Alafu ww Unakuja unatafuta Cheti hapo buguruni kirahix rahix acha life ianze upya
 
Hivi vyeti vya form four and form six ni gate passes za kuingia vyuoni, ukisha ingia unapikwa na kuiva. Yaani, mmeshindwa kuwapima pale walipo kama wameiva au hapana?. Unesi, upolisi , uganga n,k ni zaidi ya form 4. hapa watawala wameshindwa kutumia busara hili tatizo ni kubwa la kijamii kuliko mnavyofikiri. Kibaya zaidi limefanyika kiupendeleo vyombo vinavyolinda watawala vimeachwa bila kuguswa. Double standrads hii sio nzuri kwa mstakabali wa nchi yetu.

Binafsi sio lazima majeshi yetu ya kaguliwe vyeti feki, Isitoshe hawana madhara Kwa jamii hata km kuna vyeti feki.
Mie nalia Na wenye nafasi za maamuzi km RC, DC, WEO nk hawa lazima wakaguliwe
 
Hivi vyeti vya form four and form six ni gate passes za kuingia vyuoni, ukisha ingia unapikwa na kuiva. Yaani, mmeshindwa kuwapima pale walipo kama wameiva au hapana?. Unesi, upolisi , uganga n,k ni zaidi ya form 4. hapa watawala wameshindwa kutumia busara hili tatizo ni kubwa la kijamii kuliko mnavyofikiri. Kibaya zaidi limefanyika kiupendeleo vyombo vinavyolinda watawala vimeachwa bila kuguswa. Double standrads hii sio nzuri kwa mstakabali wa nchi yetu.
Nakupinga ... NAKUPINGAA NAKUPINGAA.

...

...

NYUMBA NI MSINGI NA SIO PAA.
 
tatizo la nch h knowledge 2plia kule,wanataka gamba,ndo maana vyuo ving hapa tanzania ingawa huko uraian sijui vgezo vyao lkn hapa kwe2 wanasema il ufundishe chuo lazima uwe na 3.9 kutegemea na chuo lkn utakuta m2 huyu kudeliver material n f lkn mwenye 3.0 yuko nondo n hatar sawa na leo m2 anauzoef zaid ya miaka kum leo anachomolewa,kwel kuna watu watakufa na puresha2 kwa hal hii! ngoja 2one mwisho wake ingawa kama vle n njia ya kupunguza wafanyakaz pas na raia kujua baada ya nch kuyumba kiuchumi hata hyo nyongeza ikawa changa la macho kwa wafanyakaz mazuzu wa kibongo tofaut na kenya,ukiona kiongoz anakusifia kasha kutia kidole!
 
Cheti cha form four ndo criteria yao kubwa, na elimu ya form four ni outdated, watu kama wamesoma na vyuo wamemaliza hio form foir ina impact gani katika kazi yao?!!je kuna ushahidi kuwa kazi zao zime underperform kwa sabb ya cheti cha olevo?! Or 6,, nadhani dhana ya kuwa govt haina hela na ni retrenchment stratery itakuwa kweli
 
Vyeti feki vimewaumbua watu wengi. Ndoa zimesitishwa, Bwana harusi watarajiwa wana vyeti feki.
 
Hawa ni watu wenye ujuz kabisa leo wanaondoka muhimbili pamoja na changamoto zote za utabibu zilizopo pale, MH. Ungedeal na hawa wanaonza kuingia makazini hao waliopo wangepotea wenyewe tu nje ya hapo mtaua watu pressure na pia tutapungukiwa na wataalamu hasa katika sekta muhimu kama ya afya.
Tulia bhana. Kuna wale wapya walio kuwa waende Kenya waziba hilo pengo.

Wana uzoefu wa kutosha.
Hawa feki ndio wana kosesha watu ajira.
 
Jambo la vyeti lilianza kwa JK lakini JK alijua madhara yake kwa Jamii na hatma ya wahusika akaliacha lakini kiukweli litaumiza watu wengi sana huko tuendapo
Kuna tatizo kubwa sana la Waafrica kuamini makaratasi(vyeti) sana na hii imepelekea hata wanafunzi kuwa watumwa wa vyeti kuliko kilichowapeleka Shule au vyuo (Elimu na maarifa) Kwa kujua Cheti ndio kila kitu kuliko Knowledge
Haya mazoea ya short cuts lazima yaishe. Nchi aiendelei coz wajinga ndio wana vitengo
 
acha upumbafu ndugu..
jeshi sio hatel management.....
unajua madhara ya soldiers kuwa terminated ww......????
Tatizo ni double standards kwenye nchi moja.hawa wanaachwa wakati wengine wanakabwa koo kisa hawashiki silaha.
Ngoja nianzishe hospitali yangu binafsi, hapa kuna wataalam wanachezewa tu kisa vyeti vya form four, "photosynthesis", matrices vinahusiana vipi na kuchoma sindano ya artesunate? Hapa najiokotea "cheap labour"
 
RAIS KWA HILI NAKUPA BIG UP.

UKIMALIZA GVT HAMIA PRIVATE. Waambie kuna vyeti Original viko Gvt mtu yuko Private na wengine mtu yuko Private cheti chake kipo GVT, Kwahiyo lengo lako ni kuwasakanya kote.

Hii nchi wajinga wakiisha itaendelea tu.
 
Mimi binafsi sintaona ajabu serikali ikifunguliwa Kesi nyingi kutoka kwa jamaa wa wahanga wa huduma zilizotolewa MNH huku serikali ikifahamu fika kuwa wataalam hao hawana sifa.
 
na hao wengine sio ndugu na jamaa, wangewaacha tu watu wana ma experience yao ya kufa mtu, yaani hao ma senior ukimchukua nurse wa degree ukamuweka hapo wala hawezi shindana na hao ma senior kwa uzoefu, kazi sio hivyo vyeti bali ni huo uzoefu walioupata kwa muda mrefu yaani hao wame graduate practically, na kwenye ajira hapo ni sawa na kutoa hela mfuko wa kushoto na kupeleka wa kulia wote hao ni watanzania
Maexpirience nchi ingeendelea kuwa masikini?
Embu acha kufikiri Kwa kutumia pua
 
Ndugu tunapozungumzia Elimu ambayo inazalisha wataalamu ni Elimu ya juu na tatizo ambalo wengi limewakumba ni vyeti vya O & A level ambapo ni Elimu ambayo ni kama basics ya kile utakachokikuta mbele kielimu. Hakuna wataalamu wanaozalishwa kuanzia form 1-6 pia utakubaliana na mm kuwa pamoja na Elimu ya darasani kuna Elimu nyingine nje ya kuta nne za darasa ambayo ni Elimu ya Ufahamu au Maarifa ambayo inapatikana through Experience kitu ambacho wengi waliofukuzwa kazi tayari Elimu hii wanayo
Mfano mm sisemi kwamba waliofoji vyeti wako sawa hapana wamekosea sana lakini pamoja na kukosea tayari hii ni Product ambayo hipo tayari kwa matumizi tofauti na leo ukiajiri watu wengine wapya. Hapa tayari kosa limeshafanyika na hii ni kutokana na mifumo ya Kielimu na ajira kuruhusu watu ambao ni Fake kuingia kwenye sehemu ya Original

Ningekuwa ni mm wala nisingefukuza Product hii, ndugu hakuna jambo gumu na baya kama kumuumiza mtu kiakili ni kufanya yule aliyefoji cheti cha form 4 akasome na yule aliyefoji cha sex naye wakasome unatoa muda wa miaka 2 kwani kuna Elimu ya QT then ni kutengeneza mfumo ambao hautoruhusu tena ujinga huu kujirudia kwani mpaka sasa hata wakifukuzwa hawa bado mfumo unaruhusu watu fake kuendelea kufoji na kupata ajira au kuendelea na Elimu ya juu, pia swala hili linakosa credibility kwa sababu limegusa watu wachache tu na wengi wameachwa

Hatufuati Maelezo na porojo mkuu kinachofuatwa ni sheria. Sheria haizungumzii habari za experience Bali huzungumzia habari za mtu kufoji na kughushi majina ambayo si yake.

Kwa hiyo hapa tunaangalia sheria inasemaje na sio porojo zako hapa.

Ningekuona unaakili kama ungesema Sheria ibadilishwe ili wenye Experience map wapewe nafasi hata kama wanatumia majina fake.

Vingenevyo unatetea ujinga Kwa sababu unafanana nao
 
Back
Top Bottom