Wafanyakazi 12 wa Azam Tv wapata ajali mlima Kitonga. Walikuwa wanaelekea jijini Mbeya kurusha matangazo ya NBC premier league

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga.

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.

Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.

Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.

Imetolewa na
Azam Media Limited
13, Februari 2022

20220213_153213.jpg
 
Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.

Capturge.PNG
 
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga. https://t.co/RMb9rd9Esr
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.

Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.

Imetolewa na
Azam Media Limited
13.Februari.2022
View attachment 2118441
kwa hiyo Azam mlitaka mtoe kafara naona limegoma! watu 12 na kipanya mpaka mbeya kweli! yaan mmekosa hata coaster kama sio uchawi ni nin
 
Kuna tatizo kwenye idara ya usafirishaji katika kampuni ya AZAM Media. Haya matukio ya waandishi wao kupata ajali yaangaliwe kwa jicho la umakini haswa katika aina ya madereva wanaowaajiri, aina ya gari , idadi ya waandishi wanaopanda gari, muda wa safari, posho kwa maana budget ya idara ipoje nk.

Nimesoma kwenye wall yao inaonyesha watu 12 wamenusurika walikuwa kwenye hiyo hiace wamenusurika.

Labda tujiulize, Hiace inapakia abiria wangapi, plus mizigo yao na vitendea kazi?

Pamoja ya kwamba chanzo cha mazingira ya ajali yanaonyesha lorry kilikuwa mbele yao lilianza kurudi nyuma baada ya kudhindwa kupanda mlima, Ila hii idadi ya abiria kwenye kipanya haiendani na mazingira mazuri ya kazi kwa hawa waandishi.

Azam wajirekebishe kwa hii idara ya usafirishaji. Watu 12 pamoja na mabegi yao plus vifaa ya kazi dah.
 
Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.

View attachment 2118465
Hapo hata msipo ovateki, malori yanakata sana upepo,
 
Pole kwa wahanga.

Ila Azam wanashindwa kuwalipia ndege hao wafanyakazi wao. Kuliko kupanda kipanya Dar to Mbeya
 
Back
Top Bottom