Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Wafanyakazi 10 raia wa kigeni wenye asili ya Asia wa kasri la mfalme wa Abu dhabi inayosimamiwa na Kampuni ya Ortelo Business Coparation(OBC) iliyopo eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro,Mkoani hapa wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kufanyakazi nchini kinyume cha sheria za ajira kwa wageni .
Wakisomewa mashtaka mapema leo mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, Niku Mwakatobe Mwendesha mashtaka wa Idara ya kazi mkoani hapa, Immanuel Mweta alidai kuwa mnamo Novemba 2018 hadi januari 2019 washtakiwa hao walitenda kosa la kufanya kazi kinyume na sheria ya kuratibu ajira za wageni.
Mweta aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Darweshi Jumma,Riaz Aziz Khan,Mohammad Tayyab,Ali Bakhash,Abdulrahman Mohammed,Martin Crasta,Imtiaz Feyaz,Arshad Muhammad,hamza Sharif na Zulfiqar Ali ambao wanashitakiwa kwa kosa la kufanyakazi kinyume cha sheria za uratibu wa wageni na kutokuwa na vibali vya kufanyakazi nchini.
Washtakiwa hao ambao walikuwa hawajui lugha ya Kiswahili wa kiingereza na kutumia mkalimani aliyetambulika kwa jina la Muazamu Husein walikana makosa yao na kusema kuwa kampuni hiyo iliwaleta bila wao kujua chochote na wana uhakika na vibali walivyo navyo.
Washtakiwa hao walikuwa wakiwakilishwa na mawakili wawili Godluck Peter akisaidiana na Daud Haraka wakili haraka aliiomba mahakama kuwapatia dhamana washtakiwa hao kwani kosa linalo wakabili linastahili dhamana.
Wakili wa Upande wa mashtaka ,Mweta alidai hawana pingamizi lolote juu ya dhamana ya washtakiwa ila dhamana ifuate utaratibu wa mahakama.
Hakimu Mwakatobe alisema dhamana kwa washtakiwa wote ipo wazi na kila moja anapaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na vitambulisho na mali kauli ya thamani ya million Tano.
Washtakiwa hao walikidhi dhamana na wapo nje na kesi hiyo imeahirishwa hadi Tarehe 22 mwezi 2 mwaka huu itakapotajwa tena.
Akiongea nje ya Mahakama,Afisa wa idara ya kazi mkoa wa Arusha, Alfred Mdumi alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na maofisa wabuhamiaji mkoani hapa wakati wakijaribu kutoroka kuelekea nchini Dubai.
Sent using Jamii Forums mobile app