Wafanyabishara ya ngono waiomba serikali ihalalishe biashara yao ili walipe kodi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
640x480xprostitutes_0.jpg.pagespeed.ic.VaD5V-iIvq.jpg

Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi, kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.

Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.

“Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini” alisema Rosemary Kazeze.

Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya kunakosesha serikali mapato.

Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.

“Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein


Chanzo: Mwananchi
 
miongon mwa biashara kongwe duniani wapewe 2 mana hamna namna, nasema kwa sababu wateja n weng tena wakada mbalimbal, kuanzia wafanyabiasha wakubwa na wadogo, wa2msh wa uma ngaz zote, viongoz ngaz zote, maofsa wa jesh nao pia n wateja wazur, wanasiasa n.k kwakuwa wateja wapo uwez kukomesha bora wapewe 2 vbar mana hamna namna
 
Dunia inaelekea mwisho mweh! Lakini si wakuwalaumu. Maana Wateja wanapata ndio maana biashara hii inaendelea. Sasa mpaka wanataka kulipa kodi. Kaaazi kweli kweli.
 
Wanaiga ya nchi jirani ya Zambia maana kule makahaba walianza zamani kulipa kodi kwa serikali yao. Kule ukilala na kahaba ukisumbua kulipa anaita polisi utawekwa ndani hadi utoe hela. Chezea weee...! Watu wako kazini.
 
Inaamana mteja atapewa risit,
Kwa risiti itaandikwaje yaan kanunua k*** au yaan namna ya kuandikiwa aina ya bidhaa ndiyo inanipa tabu?
Nimepokea kutoka kwa ................. Kiasi cha shilingi 50,000/ ikiwa ni malipo ya kustareheshwa kwa dakika 60.
 
Nimepokea kutoka kwa ................. Kiasi cha shilingi 50,000/ ikiwa ni malipo ya kustareheshwa kwa dakika 60.
Sasa ngoja uweke pmj na ya bar alaf wife aikute, Na itakuwa na namba ya cm ili ukitaka huduma upige tu cm!!cpt picha hapo kitakachofuata.
 
Serikali itasaidia sana kama watakubali biashara hii ifanyike kisheria maana zoezi la kwanza kabla ya dada kupewa ruhusa rasmi na serikali itawalazimu wapimwe afya zao kuona je wako salama.. Na wale walio salama tu bila HIV ndiyo watakuwa registered..Hii itasaidia sana hata watumiaji pale ajali itokeapo kama kuburst kwa ndomu wakati uko kwenye 18....
 
Wakiruhusu watarahisisha sana, tutaacha kuchukua wanafunzi, wanachuo na wake za watu maana hao wanagharama sana kwa sababu kila leo nitumie muda wa maongezi ooh mara nina shida nitumie m-pesa, lakini Madada powa mnapiga mechi unaondoka zako hamjuani tena na ukija siku nyingine unachukua mwingine mbele yake wala hakuna wivu au ugomvi
 
Waruhusiwe maana mapato mengi ya kodi yanapotea huko. Kama kodi ya kutokana na bia inaendesha serikali, na kodi ya hii biashara huenda ikawa kubwa kuliko hiyo ya bia.
 
Inaamana mteja atapewa risit,
Kwa risiti itaandikwaje yaan kanunua k*** au yaan namna ya kuandikiwa aina ya bidhaa ndiyo inanipa tabu?
huko walikokubaliwa wanaitwa sex workers au wafanyakazi wa ngono, risiti itaandikwa huduma ya ngono
 
Back
Top Bottom