Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
15,675
12,339
Habari wana jamvi,

Naomba ushauri nataka kwenda uganda kuleta nguo za mitumba, pochi na viatu pamoja na vipodozi napenda kujua cha kufanya maana ndo nataka kuanza ikiwemo accomodation nikiwa uganda,je huku Tanzania nitaziuzaje, mtaji kwa mzigo wa kwanza uwe shingapi vip usafiri,Ushuru na TRA? Msaada plz.

Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

Mkiwa na swali ulizeni
Nairobi kama vya mtumba kama special nenda Kariakoo au Uganda.
Uganda tuseme simpo moja utanunua elfu 75 ya uganda bei ya jumla sawa na 5000 ya TZ. Ambapo vinauzwa sio chini ya 12,000 hadi 15,000 hapa nchini. Ukichukua mzigo mkubwa utapata faida

Unaweza ukatumia Saibaba au Mordern coach kusafilisha mzigo wako kwa bei poua. Nauli 130,000/= kwenda na kurudi. Weka hapo kula kulala. Kuna sehemu panaitwa MUKWANO MALL ndo kariakoo ya Uganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jamvi,naomba ushauri nataka kwenda uganda kuleta nguo za mitumba,pochi na viatu pamoja na vipodozi napenda kujua cha kufanya maana ndo nataka kuanza ikiwemo accomodation nikiwa uganda,je huku tanzania nitaziuzaje,mtaji kwa mzigo wa kwanza uwe shingapi vip usafiri,ushuru na tra,???????msaada plz
Maswali yako mengine yanaweza jibiwa na wewe ....kwa nini Kampala,
Nimewahi kuwa Kampala accomadation sio mbaya kwa elfu 30 unaweza lala mahali salama sana.

Hilo la biashara sijui hata mimi niliwahi tafuta taarifa ....ila kuna mdau alinipa mwanga anaitwa MONEY STUNNA ,KAMA NI MTAALAMU TAFUTA HIYO THREAD.

Ila ni kweli Kampala kuna mitumba mizuri kuliko Dr
 
Mkuu sijawahi fanya biashara ya nguo Ug lakini pia tunajifunza kwa kuona, kule nyumbani 95% ya wafanya biashara wanapata mali ugand na miongon mwao 30% ni wanawake wanauza nguo za kike na wametoka kimaisha wanamiliki vitu vya juu, tahadhari waganda weng ni wez walimwibia baba hadi sasa tukabak masikini wanaiba kwa akili sana, na kama hujui english ndo utakoma!! Any way nenda tu mkuu boda nzuri ni mtukula, short cut ya ushuru unapita mlongo karagwe.
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni
 
MONEY STUNNA vipi kuhusu connection ya biashara hyo kati ya Uganda na Sudan Kusini imekaaje hyo

Sudan wanaitegemea sana Uganda kwa asilimia kubwa kuanzia chakula adi bidhaa nyingine.

Waganda wengi wanafanya biashara south sudan na sababu kubwa mpaka Uganda walipeleka jeshi south sudan ni kuleta aman sababu wananufaika sana na kodi kwenye boda yao na south sudan.

Watu wengi wanapeleka bidhaa south sudan na thaman yao ya pesa iko juu sana sababu ya kuuza mafuta.

Hivo biashara ya chakula na bidhaa nyingine inalipa
 
Ngoja mm niwe shuhuda wa kile unachotaka kufanya mkuu...last year nilienda uganda mwez wa 6 kuchukua hzo hzo nguo za mtumba, nilikuwa na 5m...nilifikia hotel moja pale mukono inaitwa 24/7 ni hotel nzur na ipo barabaran pia kwenye ground floor pana ofisi za kampala coach hvyo unapata uhakika wa safari na kutunziwa mizigo yako pale ofisini kwao....kwa chini zaidi ya hiyo hotel kuna club wanajaa wanafunzi wa vyuo coz lile eneo la mkono lina vyuo vingi sana na utakutana na wabongo wa kutosha na wakenya......janguuu.
 
Back
Top Bottom