Wafanyabiashara wenye maduka Kariakoo wagoma kufungua Maduka wakipinga mashine za TRA

ATM na tawi la benki kama yalivyo matawi mengine ya kawaida. Tawi ni duka kama maduka mengine ya kawaida kwa hiyo huwezi kukusanya pesa kwa watu ili wakuwezeshe ufungue duka. Ukija upande wa Agency Banking, yule anayetaka kuwa agent anakalamia vifaa vyote, na vifaa hivyo vipo kama hizo EFD za TRA.

Sasa kama duka ndio mfano wa agency banking je mwenye duka aliomba kuwa agent wa TRA??!!!!
Au analazimishwa na haoni faida ndio maana.anagoma??!!!!

Nimekuuliza ATM ikipelekwa wilayani manunuzi huchangiwa na halmashauri husika???!!
 
Ritz leo umeleta habari tu,nakumbuka siku ile ishu imetokea mbeya Uliwaponda na kuwakebehi watu wa Mbeya,leo una maoni gani juu ya kazia hii
 
Last edited by a moderator:
Kuna Shida ya uelewa na Siri kubwa iliyojificha kwa baadhi ya wafanyabiashara kariakoo ambao wanitumie majina ya watu ambao hawapo kwenye kusajili biashara zao , mfano inakuta Mtu anasajili biashara moja kwa jina lake la kwanza na ukoo then biashara nyingine anasajili kwa jina lake na la baba yake then nyingine kwa jina la ukoo na la baba!
Shida na balaa imeanza pale unapotakiwa kuweka biometric zako ( vidole na Picha yako kwenye system ya TRA) Mtu Huyu hawezi kujibadili lazima achague jina moja na kubwa zaidi unamkuta Ana leseni ya gari ambayo hizo biometric zimechukuliwa anakuwa blocked kujisajili Mara ya pili na system ndio mambo ya technology !! Sasa baadhi ya watu wenye Shida hii ndio wanaimiza mgomo kariakoo nakubaliana bei iko juu lakini kwa wafanyabiashara aw kariakoo wanashida ya kulipa kodi ndio maana hata Mwaka huu waliliwa baada ya kuagiza Mizigo ilipokamatwa bandarini waliikimbia maana walikuwa wamefanya udanganyifu mwingi sana ! Wafanyakazi wanalipa kodi kwa uaminifu sana ni time ya business people.
 
watu wa serikali huwa ni wazuri tu kuzungumza na kutolea maelezo mambo kama wewe unavyofanya hapa lakini ukweli ni kwamba on the field ni zero.Hali haiko hivyo unavyosema hapa na huku mtaani tunaona.Semeni tu mnatafuta hela za 2015 lakini suala la kuwauzia watu miundombinu ya kodi kwa gharama kubwa haliingii akilini kabisa.Kwa mfano unasema dealers wako wengi una uhakika na unachosema?suala la mashine hizi kukorofisha mara kwa mara unalijua?uhalisia wa mtu kupeleka mashine yenye umuhimu kwake kwa fundi kila wakati umeufikiria?mbona pale supermarket za mlimani walikataa mashine zenu?biashara ya kukopesha inakuwaje?(mie kuna duka nakopa mahitaji yangu na kulipa hela mwisho wa mwezi na tuko wengi wenye utaratibu kama huo,wengi sana ni watz wachache wanaishi kwa cash,wengi wetu tunaishi kwa mikopo)sasa hii mashine inamlazimisha mfanyabiashara kufanya biashara ya cash,hapo mnatupa ujumbe gani sisi maskini wa tz tulio wengi na hasa wafanyakazi wa serikali?rate zenu za kodi haziendani na mazingira halisi ya biashara na uwezo wa mtanzania na faida anayopata mfanyabiashara,hasa retailers ndio wanaumizwa sana kwa sababu ananunua bidhaa iliyokwishakatwa kodi kwa whole saler na hawezi kuipandisha bei kubwa zaidi halafu anakatwa na yeye kodi ile ile.Ukwepaji kodi ulikuwa unawafanya watuuzie vitu kwa bei ya kawaida lakini sasa mkiwabana walipe kodi,kumbukeni pia kurekebisha hesabu zenu,bidhaa ilipiwe kodi moja mara moja au kwa kiasi kidogo ili kumlinda mnunuzi vinginevyo nawahakikishieni msipoliangalia hili,muda si mrefu gharama za maisha zitakuwa juu na watu wataanza kudai mishahara inayoendana na matumizi yao,mtakuja kuumia nyie wenyewe..what goes around...unless suala liwe ni kuuza mashine mpige hela ya mara moja na si kukusanya kodi kwa kutumia mashine hizo,hapo kuna maswali mengi kuliko majibu kwa kweli!

Mkuu utakuwa umekosea, mimi si afisaa wa TRA wala sijawahi kuajiriwa na TG, mimi ni mmoja wa wauza wa hizo EFD! Kama una maswali yanayohusiana na mimi naweza kukujibu, yanayohusu TRA tafadhali onana na wahusika!
 
We riz kipindi mbeya wanagoma si ulisema nyie huko kariakoo mmeshaanza kutumia? Au sio wewe?

Na mie nashangaa, in fact alienda mbali zaidi kwa kuwatukana CHADEMA akiwahusisha na mgomo huo! Sasa Kariakoo nako sijui ni CHADEMA pia!?
 
Kuna Shida ya uelewa na Siri kubwa iliyojificha kwa baadhi ya wafanyabiashara kariakoo ambao wanitumie majina ya watu ambao hawapo kwenye kusajili biashara zao , mfano inakuta Mtu anasajili biashara moja kwa jina lake la kwanza na ukoo then biashara nyingine anasajili kwa jina lake na la baba yake then nyingine kwa jina la ukoo na la baba!
Shida na balaa imeanza pale unapotakiwa kuweka biometric zako ( vidole na Picha yako kwenye system ya TRA) Mtu Huyu hawezi kujibadili lazima achague jina moja na kubwa zaidi unamkuta Ana leseni ya gari ambayo hizo biometric zimechukuliwa anakuwa blocked kujisajili Mara ya pili na system ndio mambo ya technology !! Sasa baadhi ya watu wenye Shida hii ndio wanaimiza mgomo kariakoo nakubaliana bei iko juu lakini kwa wafanyabiashara aw kariakoo wanashida ya kulipa kodi ndio maana hata Mwaka huu waliliwa baada ya kuagiza Mizigo ilipokamatwa bandarini waliikimbia maana walikuwa wamefanya udanganyifu mwingi sana ! Wafanyakazi wanalipa kodi kwa uaminifu sana ni time ya business people.
 
Na mie nashangaa, in fact alienda mbali zaidi kwa kuwatukana CHADEMA akiwahusisha na mgomo huo! Sasa Kariakoo nako sijui ni CHADEMA pia!?
Mkuu usipende kuzuwa wapi nimewatukana Chadema weka qoute yangu ya matusi.
 
Kwanza TRA wajilaumu wenyewe kuwa wameshindwa BIG TIME katika kutoa elimu ya kodi kwa mlipa kodi. Kuna wafanyabiashara wengine wanafikiri VAT wanalipa wao, kumbe wao ni wakusanyaji tu wa kodi hiyo, kwani gharama yao (ambayo inajenga bei yao ya kuuzia) itabaki pale pale. Lakini pia wanagomea kodi hiyo ya VAT kuwa ni kubwa coz na wao mauzo yao yanapungua kwa kuwa wanaonekana kuwa wanauza vitu kwa bei kubwa (kwa mlaji), ambaye naye yuko tayari kuuziwa bila risiti ili apate unafuu wa bei. Mzunguko unabaki hapo hapo kila mtu hamuelewi mwenzake....

Na huo ukusanyaji wa kodi, basi hata huyo wa Kariakoo aone neema yake basi, kuna mibarabara ya Kariakoo mibovu hata unaweza kugoma kuwa uko katikati ya jiji....
 
rtz tunajua wewe unamiliki maduka mengi na familia yako kariakoo na mna kampun ya clearing and fowardng nje ambapo mnapakia mizigo ya watu kwa nusu bei kwa sababu bandarini hamlipi kodi mnakwepa kodi...kwenye malori mmefanya mgomo ukamtumia mzee kuptia kampun yako na mosha ya delna transportation ltd kumshawshi pm amwwagze magufuli kpndsha sheria ya mizani na huo mgomo wa kukwepa mashne za tra tunajua wewe ndiye mhuska mkuu mnataka nchi ipate mapato wapo mbona wewe na ndugu zako mnavuruga nchi kama shamba la bibi???yani mnataka twende wapi kama mpaka familia ya rais inahujumu uchumi wa nchi??

Duh
Sawa tutafika tu
Na kumbukeni Mungu yupo na siku zinakuja.
cc:mokoyo
 
Sasa kama duka ndio mfano wa agency banking je mwenye duka aliomba kuwa agent wa TRA??!!!!
Au analazimishwa na haoni faida ndio maana.anagoma??!!!!

Nimekuuliza ATM ikipelekwa wilayani manunuzi huchangiwa na halmashauri husika???!!
Mkuu unanichekesha sana, sheria za nchi ndizo zinazotubana katika kila tufanyalo. Kila mwananchi ana wajibu wa kulipa kodi. Kila mfanyabiashara analazimishwa kisheria kulipa kodi.
 
bado upo gizani hujaelewa wanagomea wao ni bei ya machine. 1,000,000/- ni hela nyingi sana kumbuka hiyo machine itawasaidia TRA kukusanya noti nyingi, ni kitendea kazi chao

Kwa nini wasiwe kama TANESCO wanaogawa mita ? Bora ya TANESCO wanakupa umeme TRA waleta nini kwa gharama ya 1M?

Mkuu,
kwa kusema nilichokisema haimaanishi kua sielewi kinachotokea.
Najua wafanyabiashara wanazigomea mashine hizo kwa kisingizio cha bei huku ukweli ukiwa wazi kuwa wanajaribu kuleta janja ya nyani(to use a poor term) kujaribu kukwepa kulipa kodi stahiki kwani wamezoea kuwapatia maafisa wa TRA kitu kidogo ili wapigiwe mahesabu tofauti.
Nimeshauri serikali iangalie uwezekano wa kupunguza bei ya mashine hizo.
Pia wafanye utaratibu wa kuwapatia wafanyabiashara mashine hizo kama mkopo halafu wakusanye hela yao kidogo kidogo(kwa awamu) bila kuwaumiza wafanyabiashara.
Pia huwezi kuwalazimisha maagent waziuze mashine hizo kwa 50 wakati wameziagiza kwa $300.
Tutakua hatuwatendei haki.
 
Kuna Shida ya uelewa na Siri kubwa iliyojificha kwa baadhi ya wafanyabiashara kariakoo ambao wanitumie majina ya watu ambao hawapo kwenye kusajili biashara zao , mfano inakuta Mtu anasajili biashara moja kwa jina lake la kwanza na ukoo then biashara nyingine anasajili kwa jina lake na la baba yake then nyingine kwa jina la ukoo na la baba!
Shida na balaa imeanza pale unapotakiwa kuweka biometric zako ( vidole na Picha yako kwenye system ya TRA) Mtu Huyu hawezi kujibadili lazima achague jina moja na kubwa zaidi unamkuta Ana leseni ya gari ambayo hizo biometric zimechukuliwa anakuwa blocked kujisajili Mara ya pili na system ndio mambo ya technology !! Sasa baadhi ya watu wenye Shida hii ndio wanaimiza mgomo kariakoo nakubaliana bei iko juu lakini kwa wafanyabiashara aw kariakoo wanashida ya kulipa kodi ndio maana hata Mwaka huu waliliwa baada ya kuagiza Mizigo ilipokamatwa bandarini waliikimbia maana walikuwa wamefanya udanganyifu mwingi sana ! Wafanyakazi wanalipa kodi kwa uaminifu sana ni time ya business people.

Ahsante mkuu kwa kuona mbali.
 
hizo machine ni noma hukwepi kodi sasa hao wafanya biashara wamezoea kuiibia serkali sasa mwisho wao umefika .majambazi wakubwa
 
Mkuu usipende kuzuwa wapi nimewatukana Chadema weka qoute yangu ya matusi.
Sijazua chochote, ila ishangai wewe leo kupinga. Anyway, matusi ni relative (kwako weye inaweza usione kuwa ni matusi kama hiyo ni lugha yako uliyoizoea)!
 
Naona la mgambo limelia,

Imeshatangazwa vitaa,

Dhidi ya CCM walafi na wafanyaji magendoo,

Walanguuziii,,

Wasiowajibikaaa,

Na wanaohujumu uchumi wa taifaa,Bravo sana,vema hii ikasambaa kote nchin
 
TRA kuna barua zaidi ya 1000 kuhusu malalamiko ya mashine feki.

Huku Mbeya mashine ikiharibika mtengenezaji ni mmoja tu,naye anachaji laki tano ya matengenezo...Nahisi mashine feki zinauzwa kwa makusudi ili kuwatengenezea ulaji watu fulani...Serikali inatakiwa kuchukua hatua kudhibiti hali hii.
 
Mkuu unanichekesha sana, sheria za nchi ndizo zinazotubana katika kila tufanyalo. Kila mwananchi ana wajibu wa kulipa kodi. Kila mfanyabiashara analazimishwa kisheria kulipa kodi.

Cheka.ukimaliza njoo kwenye hoja ya msingi as kucheka ni sehemu ya kupumzisha ubongo na oia hutumika kuficha confusion!!!!

Mimi nafanya kazi na ninafanya biashara na kote nalipa kodi,sisi wafanya kazi inakatwa juu kwa juu hata wewe muhusika hujashika hayo malipo yako!!!!!

Nakuhakikishia hakuna mfanyabiashara mwenye ubavu wa kugoma kama huu mchakato ungekuwa smooth,feasible,justy and sustainable!!!!!Watu hawa miongoni mwao wanasafiri sana nje na wanajua mengi juu ya kodi kuliko labda hata hao wakusanya kodi wa "hapo mikocheni" hawa ndio wanaingiza samasung na sumsang na wanajua bei za kuzalishia na kuuzia ndio maana wanasema they are damn too expensive!!!!!!!!!!

Hivi umejiuliza kwa nini TRA hawajaleta mashine wenyewe na kusema kuwa tutapita madukani na kufunga na monitoring iwe centrally administered with field supervisors on and off????!!!!!Was not this the prooer way of enforcing the law you are talking about?????!!!!!Rather than bargaining on wether one should buy and to be paid later on????!!!!!!! Utekeleze sheria kwa pesa ya mlengwa wa sheria hiyo tena unamkopa kwa lazima,lazima ushindwe tu!!!!!!!!
 
Bravooooooo! Kiukweli huu ni wizi! unaweza kupata home theater au flat screen tv ya maana kwa laki 6 tu! sasa hiki kimashine hiki laki 9?

Kariakoo ndio Tanzania sasa tuone jeuri ya TRA!!!
Hapa nahisi Maccm yanatafuta hela.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom