Wafanyabiashara watuhumiwa kuhonga viongozi wa kisiasa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,846
Je, Muungwana alichukua bulungutu toka kwa wafanyabiashara hawa katika kinyang'anyiro cha kugombea kuwa mgombea wa CCM? Alichukua kiasi gani na toka kwa akina nani? Na hao walioshindwa nao walichukua kiasi gani na kutoka kwa akina nani?

Posted Date::10/22/2007
Wafanyabiashara watuhumiwa kuhonga viongozi wa kisiasa
Na Tausi Mbowe
Mwananchi

WAFANYABIASHARA na wamiliki wa makampuni makubwa nchini wametuhumiwa kuwahonga viongozi wa vyama vya siasa ili watoe maamuzi yasio sahihi.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Alex Mfungo, alisema jana kwenye mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa, Msajili wa vyama hivyo, Takukuru na Mkurungenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa mara nyingi rushwa za siasa zinatokea katika kipindi cha uchanguzi ambapo wafanyabiashara hutumia mwanya huo kwa kutoa ufadhili ili kuviwezesha kwenye shughuli za uchaguzi.

" Mara nyingi inahusisha rushwa kubwa, ambapo wafanyabishara wakubwa huwatumia viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwapa fedha ili wawafanyie upendeleo watakaposhinbda, hali ambayo inayokiuka msingi wa demokrasia ...," alisema.

Mfungo alisema aina hii mpya ya rushwa inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya siasa yaliyojitokeza nchini baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao umeleta changamoto mpya kwa jamii.

Kauli hiyo ya mfungo imetolewa baada ya vyama vya upinzani nchini kuwashutumu viongozi mbalimbali wa serikali kuhusika na vitendo vya ufisadi, ambapo jumla ya majina kumi na moja ya viongozi yalitajwa na Katibu Mkuuwa Wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, Dk Wilibrod Slaa kuhusika katika ufisadi.

Mfungo alisema Sheria ya Kuzia na Kupambanana Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 inamamlaka ya kuwashughulikia watu wote wanaojihusisha na vitendo rushwa wakiwemo na viongozi wa vyama vya siasa kama inavyoanishwa katika kifungu cha tatu cha sheria hiyo.

Alisema kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, vyama vya siasa vinawajibika kuweka mikakati ya dhati katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa nguvu zote.

Mkutano huo wa siku moja ulikuwa na lengo la kuzungumzia masuala ya rushwa na usalama wa raia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ambapo walikutana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Robert Manumba na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom