Wafanyabiashara wataka uchunguzi kiini moto sokoni, wadai ni njama

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Mbuyuni katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha moto ulioteketeza maduka matatu katika eneo la Stendi ya Mboya, huku wakidai tukio hilo ni njama.

Wafanyabiashara hao wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai kuunda tume hiyo itakayokuja na majibu ya uhakika kuhusu chanzo cha moto huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Simon Maigwa alithibitisha ajali hiyo ya moto ilitokea Februari 15, 2022.

FLyCIxFXMAA0ixM.jpg
 
Ajali za moto zimekuwa nyingi nyakati hizi, watu wamepoteza mali, mitaji na maisha yao yamekuwa magumu kwaajili ya watu wachache yamkini wanaolinda maslahi ya wachache na tume na chunguzi hazielezi kinagaubaga nini vyanzo na namna gani Mambo haya yatakomeshwa.
 
Hata wakati ule zilikuwa nyingi pia tena kwenye shule hasa za jamii flani,

Na hata watoto walikufa na mali kuteketea

Na mpaka leo mie sijasikia matokeo ya tume za uchunguzi zaidi ya hitilafu za umeme,

Na hata saa hii majibu yatakuwa ni Hayo hayo so tuvumilie tu kwani ukichunguza kwa undani utagundua ni hitilafu za umeme kweli
 
Hivi kamati iliyoundwa soko la kko
Majibu yake yalitoka

Ova
 
Back
Top Bottom