Wafanyabiashara wasioboresha Mashine za EFD kuchukuliwa hatua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Dkt Edwin Mhede amesema kuwa mamlaka hiyo haiongezi muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD badala yake itachukua hatua za kisheria kwa ambao bado hawajaboresha.

Dkt. Mhede aliyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa nusu mwaka wa mamlaka hiyo ambapo alipokea dodoso la kuombwa kuongezwa muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD.

Alisema kuwa jambo la kuongeza muda haliwezekani kwani zoezi hilo linaweza kufanyika kwa muda mfupi na walipewa muda wa kutosha kuanzia Desemba 7, 2020 hadi Januari 7,2021.

Alieleza kuwa ombi hilo amelikataa na wafanyabiashara wote ambao bado wachukuliwe hatua kwani wakianza kutengeneza mazingira ya kuongeza muda watakuwa wanacheza na hawatafikia lengo la uboreshaji huo.

“Suala la EFD mashine zenye protocol 2.1 sio chagua la mfanyabiashara bali ni lazima kila mfanyabiashara awe amefanya maboresho haya maboresho ni lazima yaendane na aina ya mashine tunazozitumia hivi sasa na upatikanaji wake ni wa dakika chache kwahiyo nasema kuongeza muda ni jambo ambalo haliwezekani inajulikana wazi kuwa utiifu wakati mwingine lazima watu walazimishwe,” Alisema Dkt Mhede.

Alifafanua kuwa kama upatikanaji EFD hauzidi masaa mawili au matatu na waliwapa mwezi mzima ni kwanini waongeze muda, ambapo aliagiza baada ya kutoka katika mkutano huo wakachukue hatua kwani hawatakuwa na namna nyingine zaidi ya kwenda kuwapa motisha watii kwa mujibu wa sheria lakini suala la kuongeza muda hicho kitu hakitakuwepo.

Naye naibu kamishina wa mamlaka ya mapato Tanzania, (TRA) Msafiri Mbibo alisema kuwa mkutano huu utasaidia kuweza kujua namna ya kutatua matatizo yaliopo katika sekta yao, pamoja na kupanua mikakati itakayo saidia kupata mapato mengi yatakayo wezesha kufikia malengo waliojiwekea.

Alibainisha kuwa kazi ya taasisi hii ni kuweza kusaidia serikali kujenga taifa linalojiweza kiuchumi pamoja na kimaendeleo.

Aliongeza kuwa mkutano huu utasaidia kuwawezesha kujadili njia bora itakayosababisha utendaji kazi kuwa mzuri ,ambapo pia watajadili namna ya kutatua matatizo waliyonayo ikiwemo upungufu wa idadi ya Wataalam wa mamlaka hiyo , upungufu wa vitendea kazi pamoja na ukosefu wa nyumba za Wataalam wanaoishi maeneo ya mipakani.
 
Ulaji mwingine kwa maafisa wa Tra, na kilio tena kwa wafanyabiashara .Kuna mashine ziligoma kabisa kuwa updated na hii itamlazimu mfanya biashara kununua mashine nyingine kwa gharama zake.
 
Ulaji mwingine kwa maafisa wa Tra, na kuliko tena kwa wafanyabiashara .Kuna mashine ziligoma kabisa kuwa updated na hii itamlazimu mfanya biashara kununua mashine nyingine kea gharama zake.
Yeah wale ambao mashine zao haziwezi kuwa upgraded inabidi wanunua mpya. Ila kama uko VAT registered hela yote unai claim kwenye VAT
 
Yeah wale ambao mashine zao haziwezi kuwa upgraded inabidi wanunua mpya. Ila kama uko VAT registered hela yote unai claim kwenye VAT
Sawa lakini kwa nini Efd supplier asiwajibike kwa kuuza products ambazo hazikubali updates ?

Lakini pia wameshindwa namna ya ku update hii kitu online bila kwenda kwa supplier ? Mbona smartphones , DStv decoder huwa Zina ji update zenyewe ?
 
I have no idea
 
Ujue viongozi wa nchi Kuna wakati Kama wanakurupuka.
Hilo zoezi la kuapdate efd wametangaza lini?...
Mimi nilisikia dukani kwa mhindi flani , kuwa bila ku update Efd Kuna fine , kiufupi inatakiwa ile barcode pale chini ya receipt,

Nimeshangaa hii ya kusema mwisho ilikuwa tarehe 7 January , hata taarifa ya zoezi lenyewe sikuipata , Siku mbili December nimeshinda ofisi za tra hakuna hata kipeperushi Cha zoezi hilo.
 
Siku hizi TRA nao wamekuwa wababe.
Nao wanatoa matamko.
Ngoja tuone mwisho Wake.
Mimi nilisikia dukani kwa mhindi flani , kuwa bila ku update Efd Kuna fine , kiufupi inatakiwa ile barcode pale chini ya receipt ,
Nimeshangaa hii ya kusema mwisho ilikuwa tarehe 7 January , hata taarifa ya zoezi lenyewe sikuipata , Siku mbili December nimeshinda ofisi za tra hakuna hata kipeperushi Cha zoezi hilo.
 
Mimi nilisikia dukani kwa mhindi flani , kuwa bila ku update Efd Kuna fine , kiufupi inatakiwa ile barcode pale chini ya receipt ,
Nimeshangaa hii ya kusema mwisho ilikuwa tarehe 7 January , hata taarifa ya zoezi lenyewe sikuipata , Siku mbili December nimeshinda ofisi za tra hakuna hata kipeperushi Cha zoezi hilo.
Pole mkuu. Hii taarifa ilitoka hata humu JF Miss Natafuta aliweka thread yake.
 
TRA ni waviziaji.Inabidi tu ukiwa mfanya biashara muwe ma magroup ya telegram ili kupeana taarifa mbali mbali muhimu. Ukitegemea hawa jamaa,utaumia. Si ajabu alienda ITV kile kipindi cha asubuhi,watu ndio tuko njiani kuelekea kazini, na wanaosikia ni watu wasio na majukumu asubuhi.
 
Moja ya sababu ya biashara kuwa ngumu , ni Tra kuwa na uncontrolled rogue officers , na ni ngumu sana kukomesha maafisa Hawa , maana mosi wanafanya kazi ya kukusanya mapato kwa serikali na wakati huo huo wanatumia jukumu hilo Kama stepping stone ya kuwaumiza wafanyabiashara .

Taarifa ya ku update Efd , imepita uchochoroni sana , na lengo ni kuumiza watu kwa ma fine.

Ungetegemea ofisa wa kitengo Cha taarifa awajibishwe kwa hilo , lakini wapi
 
Mimi nilisikia dukani kwa mhindi flani , kuwa bila ku update Efd Kuna fine , kiufupi inatakiwa ile barcode pale chini ya receipt ,
Nimeshangaa hii ya kusema mwisho ilikuwa tarehe 7 January , hata taarifa ya zoezi lenyewe sikuipata , Siku mbili December nimeshinda ofisi za tra hakuna hata kipeperushi Cha zoezi hilo.
Daaah! Huo ni wizi kabisa. Mashine nimenunu mwezi April lakini natakiwa ku-update! Maana na mimi mashine yangu haina barcode mwisho wa risiti. Ingawa sijasajiliwa kwa VAT. Hapa inakuwaje wakuu?
 
Tra ilitoa tangazo la kuhuisha taarifa za mashine za EFD lakini kwa mtazamo wangu taarifa hii haikuwafikia wafanyabiashara wote na hasa wa Vijijini. Ni vyema ilitakiwa watumishi wa Ofisi za Tra kule wilayani kuzunguka kwa wafanyabiashara na kuwatangazia juu ya umuhimu wa taarifa hii.

Pili, binafsi gharama ya kuhuisha taarifa hizi ni ghali sana. Inakuwaje kuhuisha taarifa mfanyabiashara anatozwa Tshs.80,000 na ikumbukwe wengine tulinunua mashine hizi kwa gharama ya Tshs.800,000. Tatu, nasikia Kampuni zinazomiliki taratibu zote za EFD siyo za Kitanzania na hivyo kufanya lolote wanalotaka.

Ninashauri Tra kuwa utaratibu wa kuhuisha taarifa za EFD zingekuwa bure bila gharama yeyote kwa wafanyabiashara. Wanyabiashara ni watu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu na wasionekane kama maadui.
 
Tra ilitoa tangazo la kuhuisha taarifa za mashine za EFD lakini kwa mtazamo wangu taarifa hii haikuwafikia wafanyabiashara wote na hasa wa Vijijini. Ni vyema ilitakiwa watumishi wa Ofisi za Tra kule wilayani kuzunguka kwa wafanyabiashara na kuwatangazia juu ya umuhimu wa taarifa hii. Pili, binafsi gharama ya kuhuisha taarifa hizi ni ghali sana. Inakuwaje kuhuisha taarifa mfanyabiashara anatozwa Tshs.80,000 na ikumbukwe wengine tulinunua mashine hizi kwa gharama ya Tshs.800,000. Tatu, nasikia Kampuni zinazomiliki taratibu zote za EFD siyo za Kitanzania na hivyo kufanya lolote wanalotaka.
Ninashauri Tra kuwa utaratibu wa kuhuisha taarifa za EFD zingekuwa bure bila gharama yeyote kwa wafanyabiashara. Wanyabiashara ni watu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu na wasionekane kama maadui.
Hata wangeweza mabango kwenye ofisi zao ambazo karibu wengi wetu tunakwenda kwa makadirio na huduma nyingine ingesaidia !
Kimya kabisa kumbe Kuna kitu kinaendelea na kina deadline !!! Ni balaa!
 
Kwa maoni yangu, suluhisho la kudumu la haya yote ni kama nilivyopendekeza hapa chini lakini inaonekana TRA wana ubia na wauza EFD machines.
 
Yeah wale ambao mashine zao haziwezi kuwa upgraded inabidi wanunua mpya. Ila kama uko VAT registered hela yote unai claim kwenye VAT
Sisi tumenunua mpya, lakini tumeambiwa hela unayoclaim ni kwa machine tuliyonunua mara ya kwanza tu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom