Wafanyabiashara wachekelea kurudisha walichopoteza. Bei ya mafuta/petrol yazidi kupanda kuumiza maskini/watu wa kipato cha chini

Ukweli ndio huo, ila wnasiasa wetu kila kukicha wanatoa false hopes kuwa "Rais Samia amesema atapunguza bei ya mafuta" kwa kuwaongopea watanzania ili ijuliaken kuwa Rais Samie ni yeye tu anatatua kila tatizo.
Wenzako wanawaza 2025 hakuna kingine kuendelea kupiga pesa za umma kwa kisingizio cha kutumikia wananchi
 
This is what they hated Magufuli for! Alijua njia zao kisha akapachika gunzi katika kila tobo njaa ilivyokithiri wakaanza kumletea upuuzi! Wanamtukana sana yani😅

Sahizi mama kaachia wajipigie hela kila mtu sahizi amegeuka mpambe nuksi. Eti mama anaupiga mwingi
Kweli mkuu
 
Katika kinachoonekana kuwa ni survival of the fittest beii ya mafuta ya gari /petrol imezidi kupanda na kufika tsh 2510 kwa lita moja mwezi huu. Unapotoa tsh 20,000 unapata lita 7.9, kitu ambacho ni kuendelea kumuumiza Mtanzania huyu wa kipato cha chini maana yeye ndiye atakayekuja umia katika suala la upandaji wa bidhaa mbalimbali nchini pamoja na usafiri kwa ujumla.

Hawa wabunge, mawaziri na viongozi wa kiserikali hawatalalamika maana wanatumia kodi zetu katika kuhudumia hayo magari. Kwa wao hata lita moja ikiuzwa tsh 5,000 hawaathiriki sababu ofisi inawajazia magari yao ma V8 full tank na maisha yanaendelea. haya ndiyo maisha tuliyoyachagua.

Jamaa yangu mmoja amenipigia simu leo akinambia huku akicheka," nilikwambia mafuta lazima yapande maana kuna pesa nyingi tulipoteza kipindi kile"

Serikali imewasahau wananchi wanyonge watu wanaendelea kujipigia kila kinachowezekana kwa nafasi zao.
Ndio. mkiambiwa tunahitaji taasisi madhubuti kulinda maslahi ya umma muwe mnaelewa,
Dai Katiba mpya acha kulia lia!
 
This is what they hated Magufuli for! Alijua njia zao kisha akapachika gunzi katika kila tobo njaa ilivyokithiri wakaanza kumletea upuuzi! Wanamtukana sana yani😅

Sahizi mama kaachia wajipigie hela kila mtu sahizi amegeuka mpambe nuksi. Eti mama anaupiga mwingi
Upo sahihi kabisa... Jamaa walikuwa wanamchukia sana. Sasa wanafurahi sana kwa sababu wamepewa nafasi ya kula.
 
Masikini tena? Si mpo uchumi wa kati na mliambiwa mtembee kifua mbele nyinyi ni matajiri?

Yani 0.97$ ndio inawatoa jasho? Kweli awamu ile propaganda zilishamiri
 
Upo sahihi kabisa... Jamaa walikuwa wanamchukia sana. Sasa wanafurahi sana kwa sababu wamepewa nafasi ya kula.
Sahizi anasifiwa hata kwa kusafiri hovyo, wanyonge kazi tunayo wafanyabiashara bei wanajipangia watakavyo! Hamna mwenye habari tena na nyie mnaoteseka mtaani!

Watu wanakusanya per diem zao na kunyofoa mamilion kadri wawezavyo mama yupo angani anazunguka dunia!
 
Nchi hii inabidi utumike ubabe.... Bila hivyo haiendi. Anatakiwa Rais kama alivyokuwa Magufuli. Kuna watu wameweka miziz kwenye wizi wa mali ya umma na kuibia wananchi maskini.
Ubabe ndio namna pekee ya kuongoza taifa hili sababu watu wengi wapo kimaslahi yani ukijipindua unapigwa! Magu alijitahidi kuwabana japo kwa 70% ila still 30% waliobaki walikuwa wanapiga!
 
Sahizi anasifiwa hata kwa kusafiri hovyo, wanyonge kazi tunayo wafanyabiashara bei wanajipangia watakavyo! Hamna mwenye habari tena na nyie mnaoteseka mtaani!

Watu wanakusanya per diem zao na kunyofoa mamilion kadri wawezavyo mama yupo angani anazunguka dunia!
Akirudi wanampangia safari nyingine tena...akirudi hajakaa sawa anapigwa safari nyingine. Ili wao wabaki wanaibia wananchi maskini. Wafanyabiashara wezi wanafurahi kwa sasa wanasema wanacheza na bei watakavyo. Hakuna wa kuwasumbua. Wanakubaliana na watu kadhaa kila mtu anachukia kamisheni yake...maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom