Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,321
- 11,410
Katika kinachoonekana kuwa ni survival of the fittest beii ya mafuta ya gari /petrol imezidi kupanda na kufika tsh 2510 kwa lita moja mwezi huu. Unapotoa tsh 20,000 unapata lita 7.9, kitu ambacho ni kuendelea kumuumiza Mtanzania huyu wa kipato cha chini maana yeye ndiye atakayekuja umia katika suala la upandaji wa bidhaa mbalimbali nchini pamoja na usafiri kwa ujumla.
Hawa wabunge, mawaziri na viongozi wa kiserikali hawatalalamika maana wanatumia kodi zetu katika kuhudumia hayo magari. Kwa wao hata lita moja ikiuzwa tsh 5,000 hawaathiriki sababu ofisi inawajazia magari yao ma V8 full tank na maisha yanaendelea. haya ndiyo maisha tuliyoyachagua.
Jamaa yangu mmoja amenipigia simu leo akinambia huku akicheka," nilikwambia mafuta lazima yapande maana kuna pesa nyingi tulipoteza kipindi kile"
Serikali imewasahau wananchi wanyonge watu wanaendelea kujipigia kila kinachowezekana kwa nafasi zao.