Wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki watakiwa kuomba leseni TCRA

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watu wote wanaofanya biashara ya uingizaji, usambazaji na uuzaji wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kuwa na leseni kutoka mamlaka hiyo yenye dhamana ya kusimamia sekta ya mawasiliano nchini.

TCRA imeeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ha Mawasiliano ya Kielektroniki ya mwaka 2010 (EPOCA 2010), kila muingizaji, msambazaji na muuzaji sa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki anatakiwa kuwa na leseni ya kufanya shughuli hiyo, na kwamba kutokuwa nayo adhabu ni faini isiyopungua TZS milioni 5 au kifungo cha muda usiopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo ya Oktoba 26, 2020, wafanyabiashara hao wametakiwa kuomba leseni ndani ya siku 30 kwa kupeleka maombi ambayo hufanyika kwa njia tovuti ya TCRA, www.tcra.go.tz, na kulipa gharama stahiki.

Mamlaka hiyo imesema watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya muda tajwa watafungiwa biashara zao na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.
 
Nijuzeni waungwana
FB_IMG_16048208101758210.jpg
 
Mkipata mtu anataka badilishana uraia mni shtue

I need to left this country
 
Tunarudi kule kuleeee.
Wachache watakumbuka kwamba zamani tv zilikua na kadi Kama kadi ya gari. Na ulikua unailipia tv Kodi kila mwaka na serekali ilikua inamjua kila mmiliki wa tv ispokua Mimi.
Wamefunga social media tumegundua VPN. wamesema tusajili simu kwa vidole na. Majina ya NIDA.
Nadhani hii haiwahusu wauzaji wa Tecno huku vijijini
 
Back
Top Bottom