Wafanyabiashara wa nyama na wachinjaji wagoma Dodoma

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
nyama(4).jpg


Shughuli za uzalishaji katika machinjio ya kimataifa ya Kizota Dodoma zimesimama kwa muda kufuatia wafanyabishara wa Nyama kugoma wakiwatuhumu wafanyakazi wa eneo hilo kuiba nyama hali iliyozua taharuki na kukosekana kwa kitoweo kwa muda katika mji wa Dodoma kabla ya jeshi la polisi kuingilia kati na kumaliza mzozo huo.

Mgomo huo ulianza mapema alfajiri ambapo wafanyabishara wa kitoweo hicho muhimu kwa binadamu wanadai wafanyakazi wa machinjio hayo wamekuwa na tabia ya kuiba Nyama huku uongozi ukishindwa kuchukua hatua ambapo wametaka pia kuruhusiwa kusimamia zoezi la uchinjaji.

Kufuatia mgomo huo ikawalazimu askari wa jeshi la polisi wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya OCD Lenard Nyandahu kuingilia kati na kuzungumza na pande zote mbili na kisha kufanya msako katika maeneo mbalimbali ya machinjio hayo kuangalia kama kuna nyama imefichwa ili hatua zaidi zichukuliwe.

Akizungumzia mgomo huo kaimu meneja mkuu wa kampuni ya nyama nchini TMC ambayo inamiliki machinjio hayo Nashon Kalinga anakanusha kuwepo kwa vitendo hivyo huku akiwataka wafanyabishara kuwaripoti wale anaodaiwa kujihusisha na matukio hayo ili wawajibishwe kwa mujibu wa taratibu za kazi.


ITV
 
Back
Top Bottom