Yaani aggre/nyamwezi unafanya kama unapandisha kurudi congo ni mkono wa kushoto duka la pili kabla ya linalouza nguo za ndani
La kwanza Lina viatu
Upande wa kulia kuna matv

Ila suruali zimeisha mzigo upo njiani hopefully next week kama bandarini hawatazingua
Suruali unaleta na za watoto miaka 10 -12?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Karibuni kampuni yetu itaanzisha Huduma za kuwatafutia wafanyabiashara wa mikoani bidhaa wanazohitaji hapa DSM, au nje ya nchi. Tutachukua oda zenu, tutawapa bei, mtatuma pesa, tutanunua na kuwasafirishia mlipo. Tutawatoza ada kidogo tofauti na gharama ungezitumia kuna DSM na kurudi. Stay tuned!
Mmeshaanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo.
NAOMBA KUELEKEZWA CHIMBO LA BIDHAA ZIFUATAZO, CHUPI ZA WATOTO, WAMAMA, WABABA KWA KARIAKOO KWA BEI YA JUMLA NI WAPI.
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!

Mkuu Naomba unisaidie Machimbo yalipo ya Nguo za Jeans za mitumba hasa hasa makoti ya Jeans na Suruali za Jeans..za kike na kiume.

Asante
 
NAOMBA KUELEKEZWA CHIMBO LA BIDHAA ZIFUATAZO, CHUPI ZA WATOTO, WAMAMA, WABABA KWA KARIAKOO KWA BEI YA JUMLA NI WAPI.

Chupi zipo mtaa wa duka kubwa la selo
Pale wana bei nzuri kuliko haya ya juu

Mengine upande wa pili wa kituo cha Msimbazi B
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa. Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Samahani dada mabegi ya shule biowang yale yanapatikana mitaa gani kwa jumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom