Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo
CC: charty.
CC: charty.
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000, 8000, 12000 lipo maeneo ya Nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee Msimbazi Kota, karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa Congo na Aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka Aongo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k, 25k, 28k, 30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo Mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh, pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Ndugu Yangu, usidanganywe. Duka LA maana Tanzania nzima Kwa vifaa halisi na bei halali no TRONIC. Lipo Barbara ya Bagamoyo kule city center. Hata Kariakoo wengi wanatoa kwake na kuwakamua wanunuzi. Nilipigwa bei kariakoo lakini baada ya kuwajua hawa tronic ni kama nimeokoka au kusilimu. Nenda utaamini maneno yangu.