Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,229
2,000
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo Kariakoo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale. Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF.


Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000, 8000, 12000 lipo maeneo ya Nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee Msimbazi Kota, karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa Congo na Aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka Aongo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k, 25k, 28k, 30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo Mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh, pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy

Mkuu heshima kwako aisee huyu mchina wa Veta huna mawasiliano yake mamiiii...?

Na anauza kwa piece hata 1 au mpaka uchukue kwa jumla...?

Thanks a lot my.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom