Wafanyabiashara wa Korosho waanika malalamiko yao kwa serikali, walia na kodi kubwa na tozo wao kushindwa kununua korosho wadai serikali inawahadaa

Hiyo barua halisi iko wapi? Mtu ameamua kutype hapa ili atuaminishe kuwa walipeleka barua kwa rais wakati siku ya kikao na rais walitoa shida zao pale na zikatatuliwa palepale. Sasa haingii akili kuja na madai mapya au kuna remote control haikuwepo kwenye kikao. Sasa waamue kusuka au kunyoa yamebaki chini ya masaa 24.

Tuna comment tuki - assume kuwa ni halisi....

Kama siyo halisi, mtu kajiandikia tu basi itabaki kuwa hivyo hivyo kama ilivyokwisha amuliwa....
 
Barua hii inadaiwa kuwa imeandikwa na Umoja wa Wanunuzi wa zao la Korosho kwenda kwa Rais Magufuli

> Wameeleza mitazamo yao kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa Korosho

======

TCTA
P.O.BOX 1494
MTWARA
30/10/2018

MH:JOHN POMBE MAGUFULI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
YAH: KIKAO CHA RAIS NA WANUNUZI WA ZAO LA KOROSHO KUJADILI BEI YA ZAO LA KOROSHO .

Tafadhali husika na somo la hapo juu,
Kwa heshima kubwa na tahadhima sisi wanunuzi wa zao la korosho tunapenda kutoa pongezi zetu kwako Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usikivu wako na usimamiaji wako uliotukuka wa Serikali yetu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kuudhulia kikao kilichofanyika siku ya tarehe 28/10/2018 katika ukumbi wa mwalimu Nyerere Conversation center siku ya Jumapili.

Katika kikao kile tunakushukuru Mh. Rais kwa kukubali kupunguza baadhi ya tozo ambapo uliitaka Bodi ya korosho ipunguze tozo yake kutoka shilingi 17/= kwakilo na kurudi shilingi 10/= kwa kilo, pia ulitaka ushuru wa Halmashauri/Manispaa ulipwe mara moja hivyo kuondoa tozo ya 0.3% ambayo Manispaa ya Mtwara mikindani uwalipisha wanunuzi wote, wanaotuma bandari ya Mtwara kiasi hicho ni sawa na shilingi 9/= kwa kilo endapo bei ya korosho itakuwa shilingi 3,000/= kwa kilo kama ilivyo shauriwa.

Hata hivyo punguzo ambalo umetupatia wanunuzi la jumla ya shilingi 16/= kwa kilo kwa kuondoa tozo hizo mbili kiasi hicho kimekuwa kidogo wanunuzi kuweza kuifikia bei ya shilling elfu tatu (3,000/=) kwa kilo kama ulivyopendekeza.

Kwa kutambua usikivu wako sisi Wanunuzi tunaomba/tunashauri yafuatayo ili kuweza kuifikia bei ya shilling elfu tatu (3,000/=).

Tunaomba Serikali iondoe Ushuru wa korosho ghafi kiasi cha 15% ya thamani ya korosho ikiwa bandarini (15% FOB Value) kwa dharula kwa mwaka huu ambapo bei ya korosho katika soko la Dunia imeshuka kwa kiasi kikubwa.

Kiasi cha 15% ya FOB ni sawa na shilling 561.75 kwa kilo kwa bei ya kununulia na shilling 3,000/= hivyo endapo tutanunua kwa bei ya shilling 3,000/= tutashindwa kuuza kulingana na hali ya soko la sasa ulimwenguni.

Kwa kutambua sasa hivi wanunuzi wengi wanauwezo wa kununua korosho kwa wastani wa shilingi 2,500/= ambayo 15% ya FOB yake ni shilling 486.75/=
Hivyo endapo Serikali itaondoa tozo ya Ushuru wa korosho ghafi ya 15% ya FOB baadhi ya Wanunuzi wataweza kufika bei ya shilling elfu tatu (3,000./=) kwa kilo kama ulivyoshauri iwe siku ya tarehe 28/10/2018.

Hata hivyo kwa kuwa tunatambua Serikali inahitaji Kodi kwa ajili ya kuhudumia Wananchi wake, tunaomba endapo itashindikana kuondoa kabisa, basi ipunguzwe kwa walau asilimia 50% na wanunuzi tuachiwe huru kushindana kwani bei zitakaribia shilling 3,000/= na zitakuwa zikipanda kulingana na ushindani utakao kuwepo.

Kwa hali ilivyo sasa wanunuzi wengi hatuwezi kurudi Mnadani kwa kuwa hatuna uwezo wa kununua kwa shilling 3,000/= kwa kilo na kulipa gharama za ziada,
na kwa kuwa Mh. Rais umetamka bei ya korosho isinunuliwe chini ya shilling 3,000/= hivyo tusingependa kwenda kinyume na kauli yako, na ili kufanikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi ambacho ni Chama cha Wakulima na wafanyakazi, tunaiomba Serikali yako tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoa kwa dharula tozo ya ushuru wa korosho ghafi kiasi cha 15% ya thamani ya mzigo bandarini ili kuweza kufikia bei ya shilling 3,000/= kwa kilo.

Ni matumaini yetu kwamba ombi letu litafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo ili tuweza kushiriki Minada itakayorejea tarehe 02/11/2018
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwako wewe mwenyewe na kwa Serikali yako tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wasalaam,

SALUM MKEMI
MWENYEKITI WA WANUNUZI WA KOROSHO TANZANIA.

NAKALA:
MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA (MB)
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CHARLES TIZEBA (MB)
WAZIRI WA KILIMO NA USHIRIKA

MKURUGENZI MKUU
BODI YA KOROSHO TANZANIA
P.O.BOX 533,
MTWARA.
Nawaapia hapa hili saga likitulia tutegemee kuona ndani ya miezi mitatu mfanya biashara mmoja mmoja akotekwa kama Mo
 
Back
Top Bottom