Wafanyabiashara Ufaransa watua Tanzania kutafuta fursa za biashara

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83
Chemba ya viwanda, biashara na kilimo nchini (TCCIA ) imepokea ugeni wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wenye lengo la kujadili na kupanua mianya ya biashara kati ya Tanzania na Ufaransa Ugeni huo kutoka nchini ufaransa umeambatana na wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa makampuni makubwa ambapo lengo kuu la mkutano ni kutaka kutengeneza urafiki wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kubadilishana uzoefu wa kibiashara pamoja kupanua fursa za uwekezaji baina ya Tanzania na Ufaransa

q06O3TheYb8Q6hgpXOyXGZpmIYQjo9HYHq4MvKBPRZajoq6G0HNWXCkLo6hXcv_uxLEJ79VjzC3iVMstSWyattjpThg8AbGPQ8yNN9767eB3gmGX6wRNm-t6Lwh-QyirJb8fv5qF0JjHaMPnbA


Makamu wa Rais wa TCCIA Ndg. Octavian Mshiu (katikati), kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA Ndg. Gotfid Muganda,pamoja na wafanyabiashara kutoka ufaransa wakati wa mkutano

Makamu wa Rais wa TCCIA Bwana Octavian Mshiu amesema Tanzania imekuwa nchi yenye bahati ya kutembelewa na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi mbalimbali na hii ni kutokana na Tanzania kuwa na sifa kubwa kimataifa kama nchi yenye malighafi nyingi za kibiashara

YSkZuIs5X1uby7lwSgZafqufHgv1ZnNG4G-yxQYSgDVgcH1dmdU1L5ythI7OdyS_CGQAjaXO7gnmXglKf6CAOxr2GU4xa5lyj2ne_uplxUbgWNygk9hSUUp8IAP9fOJNTYfm9oDOabJFGobqbw


Makamu wa Rais wa TCCIA Ndg. Octavian Mshiu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano na wafanyabishara kutoka ufaransa.Aidha Mshiu amesema kuwa ziara hii inatoa fursa nyingi kwa wafanya biashara nchini kutanua biashara zao kwenda kimataifa zaidi.Mshiu amewataka wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutumia ujumbe huu wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa kama njia ya kukuza biashara zao kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

 
Wamekosea njia, bora wangeenda Kenya au Rwanda...coz Tanzania walioiskia zaman sio ile tena....
 
karibuni Tanzania Ya Vi-wonders ila wananchi wake hatuna hela vyuma vimekaza kila sekta sijui hizo bidhaa zenu mmekuja kutuuzia au kutuletea misaada?
 
Back
Top Bottom