Wafanyabiashara: Tumieni hii miezi kuweka akiba, msijisahau kuwa Januari inakuja

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,919
Katika miezi nikiri wazi biashara hazilali mimi naonaga ni hii miezi,sehemu nyingi sana biashara hasa sisi tunaolenga wahitaji wa "kila siku" biashara zimechangamka sana sana, unajisikia raha hata kufanya biashara.

Yes ni raha kwasababu unapata faida, tusiwe tunalia tu kila siku biashara zikiwa mbaya hata zinapokua nzuri pia tuseme.

Miezi hiii watu kama kina Zero IQ ndio miezi hesabu wanafunga 50k per day, wauza nguo, viatu na vitu vinavyowahusu wanawake na wanafunzi miezi hiii ni mizuri sana, kikubwa katika kipindi hiki tuhakikishe tunafukia makorongo yaliyotokea ile miezi migumu tuliyopitia, lakini pia tuanze kujipanga kwa miezi bubu kama "January" haipo mbali tumebaki na December tu then tunakuja kuivaa January.

Tusiwe wa kulalamika sasa hivi ndio wakati kama unajua unaingiza kuliko kawaida basi ufahamu ndio wakati wa kuweka akiba kuliko kawaida maana itakapofika January kila mtu utamsikia akilia na kilio chake, usitake kilio cha January uwepo.

Jitahidi January ya 2020 (kama tukifika) basi kilio chako kiwe kingine kabisa, sio kila mtu alie biashara mbaya hela hamna na wewe ulie hivyo hivyo.

Pambana ila usisahau kutumia kibubu chako, kitakuokoa JANUARY.
 
Umesema kweli kabisa mkuu aiseee Hesabu ya sasa hivi sio ya kitoto japo mtu ukilala unakuwa hoi
hata mimi naona mkuu sio kwako tu,Hali saivi imechangamka mpk unatamani hii november ingekua na siku 51 halafu december iwe 71,kuanzia january ndio calendar iendelee na utaratibu wake wa siku 31.

Muhimu kwa sasa ni saving tu mkuuu,huku kuchoka ni lazima hatuna namna nyingine.
 
November hata watumishi wa serikali wanakuwa katika hali nzuri kuna viposho mshenzi kiasi chake... Japo inawezakana sio katika idara zote
 
Back
Top Bottom