Wafanyabiashara, TCCIA waotesha Miti 10,000 katika jiji la Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na Kilimo, TCCIA Mkoa wa Arusha kimepanda miti zaidi 10,000 ya vivuli katika jiji la Arusha katika kipindi Cha mwaka mmoja ikiwa ni hatua nzuri ya kuimarisha sekta ya utalii katika jiji hilo ikiwemo kuzuia upepo mkali uliokuwa ukiezuwa mapaa ya Nyumba.


Hayo yamebainishwa na afisa Mazingira jiji la Arusha,Maico Ndaisaba wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya miti iliyooteshwa katika kata ya Muriet, Them, Ngarenaro na Kata ya Kati jijini Arusha.


Ndaisaba pamoja na kukipongeza chama hicho Cha Wafanyabiashara kwa hatua ya kijitolea kuotesha kiasi hicho Cha Miti alisema mahitaji ya miti katika jiji hilo ni milioni moja na nusu hivyo ipo haja Kwa wadau wengine kujitokeza Katika utunzaji wa mazingira.


Naye afisa wa TCCIA Mkoani hapa, ,Charles Makoi alisema wamefarijika kuona miti walioiotesha kuanzia Oktoba mwaka jana ikistawi vema na hivyo wameonyesha nia zaidi ya kuendelea kuotesha miti maeneo mengine yenye uhitaji.


'Leo tupo kwenye ziara ya kutembelea miti tuliopanda kuona maendeleo yake na pia tumeotesha miti aina ya mikaratusi itakayosaidia kukausha Maji yanayotuama katika shule hiyo na kuwapa Kero wanafunzi"alisema


Alisema TCCIA imekuwa mdau mkubwa wa mazingira katika jiji la Arusha na imejiwekea utaratibu wa kugawa miche ya miti Kwa wanachama wake waweze kuotesha katika maeneo yao ya kazi na majumbani.


Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Muriet, Dominic Gado na Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Msasani wamekishukuru chama Cha wafanyabiashara hao Kwa kupanda miti kwenye maeneo ya shule zao kwa kuwa itasaidia kuhifadhi mazingira.








IMG_20210916_133452_288.jpg
IMG_20210916_113709_250.jpg
 
Back
Top Bottom