Wafanyabiashara Nkasi waigomea Serikali kutofungua biashara za maduka yao kupinga ongezeko la kodi ya pango la biashara

VYEMELO

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
347
459
Wafanyabiashara ya maduka katika mji mdogo wa Namanyere yalipo makao makuu ya wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa wamekubaliana kutofungua biashara za maduka yao kesho tarehe 20/01/2021 ikiwa ni mgomo baridi kupinga ongezeko la kodi ya pango la biashara.

Wafanyabiashara hao wanadai kuwa kodi hiyo ya vibanda vya biashara siyo halali kwani kwa mujibu wa mkataba wa awali waliokubaliana na Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ni kuwa viwanja hivyo baada ya kugawiwa katika soko kuu la Namanyere, wafanyabiashara waliwajibika kujenga kwa gharama zao na baada ya hapo vibanda hivyo vinakuwa mali yao.

Wafanyabiashara wanashangaa kwa nini Serikali imegeuka na kukiuka mkataba wa awali huku ikidai kuwa mkataba huo wa awali umetenguliwa na mkataba mpya unaohalalisha kuwa mmiliki halali wa sasa wa vibanda vya biashara katika soko kuu hilo ni Halmashauri ya Wilaya.

Wafanyabiashara wanahoji kwa nini hawakushirikishwa katika kuandaa mkataba huo mwingine unaodaiwa kutengua ule wa awali ambao kila mfanyabiashara alikabidhiwa nakala yake. Huu wa pili hawakupatiwa nakala isipokuwa kwa wachache wanaodai walisaini mkataba huo kwa kutishwa na watumishi wa Halmashauri wakishirikiana na vyombo vya dola.

Kwa jumla, mahusiano kati ya wafanyabiashara na Serikali yanazorota siku hadi siku wilayani Nkasi. Serikali inaoneka kutojali maendeleo na changamoto wanazokabiliana nazo wafanyabiashara. Moja ya changamoto ni mauzo madogo yanayotokana na mzunguko mdogo mno wa pesa unaosababishwa pamoja na mambo mengine kuanguka kwa bei ya mazao mbalimbali yanayozalishwa wilayani hususani mahindi.

Wafanyabiashara wengi wamefilisika mitaji na baadhi wamefunga biashara zao. Wengine wameuza rasilmali zao kama nyumba na mashamba kulipa madeni wanaodaiwa na taasisi zinazotoa mikopo ikiwemo benki.

Kwa jumla, hali ni mbaya ya biashara wilayani na Serikali inaonesha kutojali na haifanyi jitihada zozote kunusuru hali hiyo isipokuwa kuendelea kuwakamua wafanyabiashara hao kodi na ushuru.

Mwenyekiti wa soko kuu la Namanyere alipoulizwa juu ya hatua waliyochukuwa alisema mgomo wa kutofungua maduka kesho ni wa amani na maduka yataendelea kufungwa hadi pale Serikali itakapokubali kukaa katika kikao cha pamoja na wafanyabiashara ili kukubaliana mambo ya msingi.

Mwenyekiti aliendelea kusema tayari wamemfahamisha Mbunge wao, Mheshimiwa Aida Kenani kuhusiana na mambo yalivyo ili ikiwezekana aweze kuwatetea Serikali isipore haki yao. Mheshimiwa Aida yupo jijini Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge.
 
Mkataba wa maandishi wa hayo nakubaliano si upo? Watafute mwanasheria Waishtaki serikali kwa kutaka kuvunja mkataba. Wasigome kwa kutofungua maduka wanawaumiza wengine kabisa.
 
Mkataba wa mahandishi wa hayo nakubaliano si upo? Watafute mwanasheria Waishtaki serikali kwa kutaka kuvunja mkataba. Wasigome kwa kutofungua maduka wanawaumiza wengine kabisa
Hahahahaa!!! Kwa serikali hii eti ukaishitaki mahakama za hapa! Utegemee kupata haki?!! Hata siku hiyo MUNGU, akiwa upande wako ukapewa ushindi, haitekelezwi utafanya nini, unarudi mahakamani kukazia hukumu, unaambia, basi kama imekataa mimi sina la kufanya, kamuombe Mungu tu!
 
Mkataba wa mahandishi wa hayo nakubaliano si upo? Watafute mwanasheria Waishtaki serikali kwa kutaka kuvunja mkataba. Wasigome kwa kutofungua maduka wanawaumiza wengine kabisa
HESLB nayo unaizungumziaje kwa kukiuka mkataba wa 8 percent?
Unaijua serikali wewe?
 
Tatizo huko kuna mbunge wa CHADEMA yule Aida Kenani, wapinzani wanakwamisha maendeleo si ndio wajumbe?
 
Serikali dhalimu hutokana na uporaji wa haki na tamaa ya kupora haki iliyopitiliza.
 
Hebu tuliea, kuna kipande fulani tunataka tukamalize kule nanii , tukishajenga tu kila kitu kitakuwa shwari, au nyie hamuoni kulivyopendeza ndugu zangu?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom