Wafanyabiashara: Njia nzuri ya Kumiliki website kwa gharama nafuu zaidi


Elimubomba

Elimubomba

Senior Member
Joined
Jul 27, 2017
Messages
157
Likes
37
Points
45
Elimubomba

Elimubomba

Senior Member
Joined Jul 27, 2017
157 37 45
Habari za leo! Natumaini unaendelea vizuri.
Leo nimeona ni vema niwashirikishe jambo hili ambalo baadhi ya watu hawalifahamu, ni kuhusu kumiliki website. Wengi wanajua jinsi gani website zilivyo muhimu katika biashara hasa katika karne hii tuliyopo.
Na kama ulikuwa haujui basi website ni njia nzuri ya kujenga brand yako online (mtandaoni) kwani watu wengi sasa wanatumia mtandao wa intaneti na hivyo njia nzuri ya kuwafikia ni kupitia mtandao. Ukiwa na website ni sawa na kuwa na ofisi yako mtandaoni ambayo watu watakuwa wanaitembelea kujua wewe ni nani, biashara yako inahusu nini na vitu gani unauza na wanaweza kuagiza vitu moja kwa moja kupitia website yako. Makala hii haijalenga kueleza umuhimu wa website katika biashara hivyo nimeeleza kwa uchache sana kuhusu umuhimu wa website katika biashara.

Unawezaje kumiliki website kwa gharama ndogo kabisa?
Ni kawaida kuwa gharama za chini kabisa za website mara nyingi huanzia Tsh 200,000/= (laki mbili) na kuendelea hadi Milioni kadhaa. Hiki ni kikwazo kikubwa kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao mitaji yao ni chini ya milioni moja. Hivyo watu wengi wamekuwa wakiyumbishwa na kikwazo hiki.
Nitoe ufafanuzi juu ya website ili iwe website inahitaji nini. Kuna vitu vya msingi au mambo ya msingi manne yanayohitajika katika kudesign website;
Kwanza; Domain, hii ni anuani ya website yako. Domain inaweza kuwa www.jina.com au www.jina.co.tz (NB: jina = jina la website yako). Domain inapatikana kwa kusajili katika makampuni mbalimbali yaliyopo hapa nchini au nje. Gharama za domain mara nyingi huwa ni kati ya Tsh 25,000/= hadi 35,000/=.

Pili; Hosting, hii ni huduma itakayowezesha domain yako ifanye kazi, yaani iruke hewani na ndio huduma ambayo inakupa nafasi ya kuhifadhia taarifa za website yako. Huduma hii mara nyingi inalipiwa kwa mwaka na baadhi ya makampuni yanaruhusu kulipa kila baada ya miezi mitatu. Gharama za hosting hutofautiana kulingana na kiasi cha nafasi (MB au GB) za kuhifadhia taarifa zako na vitu vingine vya kitaalamu (nahofia kuwachanganya nikiviorodhesha hapa lakini ni vya kawaida tu). Gharama za hosting zinaanzia Tsh 48,000/= kwa mwaka hadi 600,000/= kwa mwaka au zaidi ya hapo inategemea na aina ya kampuni.

Tatu; Website Design: Baada ya kulipia Domain na Hosting sasa utatakiwa uende kwenye hatua ya tatu nayo ni website design ambapo utatumia Cpanel au Interworx kwa ajili ya kuistall (kusakinisha) Huduma itakayokuwezesha kuweka taarifa za website yako pamoja na design mfano Wordpress, Joomla, Drupal na kadhalika. Hapa ndipo kuna tofauti kubwa ya gharama kwani kila kampuni au mtu wana gharama walizojipangia.
Nne: Maintainance; Hii ni huduma ya kuihudumia website yako kwa mwaka mzima pale inapopata tatizo pia hutegemea na mtu au kampuni itakavyojipangia.

Ninachoweza Kukusaidia!

Kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wangependa kuwa na website kwa ajili ya kuendesha biashara zao naweza kuwasaidia kwa kuwarahisishia kupata webiste zao kwa Tsh 60,000/= tu. Ndio hii ni Ofa maalumu kwako ili uweze kuendana na mtaji ulionao.

1
Domain .com au .co.tz
Tsh 25,000/= (mwaka 1)

2
Hosting
Tsh 12,000/= (kila baada ya miezi mitatu)

3
Website Design
Tsh 23,000/= (inalipwa mara moja tu)

4
Maintanance
FREE! (kwa mwaka wa kwanza)


TUWASILIANE WhatsApp: 0685658299


Nimeambatanisha na pdf kwa wale wataohitaji kwa kuirejea baadae.
 

Attachments:

ray57

ray57

Member
Joined
Oct 29, 2013
Messages
87
Likes
28
Points
25
ray57

ray57

Member
Joined Oct 29, 2013
87 28 25
Kuna Hosting zinazolipiwa kwa kila mwezi?? I mean nahitaji site ikae kwa mwez 1 tuu.
So kwa bei hiyo ya 12000 unaifanya kwa shared hosting au unanipa na panel yangu??
 
Elimubomba

Elimubomba

Senior Member
Joined
Jul 27, 2017
Messages
157
Likes
37
Points
45
Elimubomba

Elimubomba

Senior Member
Joined Jul 27, 2017
157 37 45
Kuna Hosting zinazolipiwa kwa kila mwezi?? I mean nahitaji site ikae kwa mwez 1 tuu.
So kwa bei hiyo ya 12000 unaifanya kwa shared hosting au unanipa na panel yangu??
Ndio unaweza kulipa kwa mwezi mmoja tsh 5,000/= ya hosting, Unapatiwa Cpanel yako ambayo itakluwa www.jinalawebsiteyako.com/cpanel
 

Forum statistics

Threads 1,250,502
Members 481,371
Posts 29,735,823