Wafanyabiashara kuweka mawe na mchanga kwenye chakula sio uungwana kabisa!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,159
11,466
Wavuvi wa dagaa, uvua dagaa wakiwa wasafi kabisa kwenye maji baharini au kwenye maziwa. Chakushangaza huku wakijua kabisa hao dagaa ni kitoweo cha binadamu ambaye ndiye mteja wao na kwamba binadamu hali mchanga wala mawe, lakini huenda na kuwamwaga mwaloni kwenye mchanga au nchi kavu ili kuwakausha! Wanashindwaje kuandaa mazingira rafiki na salama wakawaanika juu ya nyasi au mabati kuthamini walaji? Sio uungwana kabisa kuchafua kitoweo cha wateja kwa kuweka mchanga wakati unawavua wakiwa wasafi.

Hali kadhalika wauzaji wa maharage na mchele, hayo mawe na mchanga huwa vinatoka wapi kama sio nyie wafanyabiashara kuweka mchanga na mawe (kokoto) ili kuongeza uzito wa kumpiga mlaji? Umeuziwa gunia la kilo 100 la maharage au mchele ukiwa safi lakini kutokana na uroho na tamaa za kutafuta utajiri wa haraka anaondoa kilo kama 20 za maharage au mchele anajazia mchanga na vikokoto vidogo vya mawe.

Unaenda dukani kununua kilo moja ya maharage au mchele kumbe asilimia 20% mchanga na mawe! Huu sio uungwana kabisa! Tunaomba serikali ifuatilie vyanzo vya mazao shambani, kwenye maghara, na hatimaye kwa wauzaji wa rejareja kubaini wafanyabiashara wasio waungwana na ambao hawajali afya ya walaji.

Mchanga na mawe ni hatari kwa afya ya binadamu kwa kuharibu (kukoboa) meno, kujaza appendix, n.k ambapo mwisho wa siku unaingia gharama za upasuaji!
 
Wabongo kwenye biashara utu unawatoka kabisa. Ukipeleka nguo kwa fundi kama kuna namna ya kuiba ataiba, ukipeleka gari garage kama anaweza akabadilisha spare akuwekee mbovu atafanya hivyo, ukimpa kazi fundi ujenzi akipata nafasi ya kukuibia hata misumari au cement ataondoka nayo, ukimpa kibarua akulimie shamba kama kuna uwezakano akafanya hila uone kalima kumbe kafukia majani atayafukia na kukuzuga. Tanzania kila unaetaka kufanya nae muamala hua anafakiria namna ya kukupiga. Imekua utamaduni wetu
 
zinginary,
Acha kutetea ujinga! Maharage yakivunwa ni uhamuzi wa mkulima kuyapiga (ili yatoke) sehemu salama na sio kwenye mawe na mchanga! Kuwa muungwana kwa wateja wanaokufanya ulime!
 
Back
Top Bottom