Wafanyabiashara kutoka Tanzania kufuata mizigo ya bei nafuu Uganda, imekaaje?

Pili ukichukua nguo maybe China unangalia interest za wa Tz unaleta nyingi namwengine hivyo hivyo. Sasa waganda wanagalia interest zao. Kinachotokea ukienda uganda unaleta nguo unique ambazo hazitokua nyingi yani sare. Ukileta tz watu wanaona nguo unique kwasababu haziko huku ziko sehem nyingine.
Cjui nimeeleweka
Titty, lakini inakuwaje sasa kwamba UG hawana bandari lakini bado wanafikisha mzigo hapa kwa bei nafuu kiasi kwamba wafanyabiashara wetu wanatoka Dar/Mza na kununua hapa; na wakifikisha TZ wanauza na kupata faida!! Something is not connecting well here. Kwa mantiki hii, ingebidi wafanyabiashara wa UG ndio waje TZ kununua mzigo.

Nimeelewa point yako; lakini hili la mzunguko wa mzigo hadi ufike Kampala na bado ukaweza kununuliwa kwa faida na Mfanyabiashara wa TZ limekaaje???
 
Wanajamvi,

Hapa Niko katika kituo cha Bus liitwalo FRIENDS jijini Kampala (Uganda) nikielekea nyumbani Tz. Ninachokiona hapa ni wafanyabiashara wa Ki-Tz toka Dar na Mwanza wamefungasha mizigo ya nguo, viatu, na vifaa vya MAGARI kuvileta Tz.

Najiuliza inakuwaje vitu ni bei nafuu zaidi Uganda ijapokuwa hawana bandari? Mizigo yao yote hupitia Bandari ya Dar na Mombasa lakini bado vitu ni bei nafuu kiasi kwamba watanzania wanavifuata huku!!

Naomba wanauchumi mlioko hapa mtuelewesha Tz kuna tatizo gani? Hii bandari ya Dar, Tanga na nyinginezo zinatunufaishaje??

Mungu Ibariki Tanzania
MODS, ASANTENI KWA KU - EDIT KICHWA CHA HABARI. NILIANDIKA NIKIWA NA HARAKA! YOU ARE DOING GREAT JOB GUYS...!! LONG LIVE JF.
 
Mkuu ni kuwa ukadiriaji wa kodi kwetu ni wa kukomoa kitu unanunua $10 wao wanasema $20 sasa ukilipa kodi kwa kiwango hicho lazima bei itapanda. Hakuna kuaminiana kati ya mwagizaji na tra.
I HOPE WATAWALA WETU WANAONA HILI...!!
 
umeonaaa eeeee yaani kodi inakuwa kubwa kushinda bidhaa uliyonunua sasa hapo kuna nini cha ziada kama sio wanakutukomoa hawa serikali
.
Sasa kama ni suala la kodi kwetu kuwa kubwa, je ukiingiza hiyo mizigo Tz kutoka Uganda hulipi kodi?
 
Kodi inalipwa kama kawaida. Uganda wananunua nguo toka ulaya na bei ni nzuri. Wafanya biashara wengi Dar hununua nguo za bei ya China na quality ya chini. Wakifikisha Dar bei huwa haina tofauti na nguo toka ulaya kupitia Uganda ambayo qualify yake ipo juu mno.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Wafanya biashara wengi hununua nguo za bei ya chini China na quality huwa chini. Wakifikisha mzigo Dar bei zao huwa juu sawa na nguo za quality ya juu toka ulaya kupitia Uganda na hatimaye Tanzania. Ushuru na kodi husika hulipwa mpakani kama kawaida. Nawapongeza TRA mipakani kwa kazi nzuri.
 
Serikali ya uganda inawasaidia sana wafanya biashara kwa kuondoa kodi zisizo na msingi ndio maana bidhaa zao bei rahisi sana.hata yard ya magari za uganda unapata kwa bei ya japan.

Wafanya biashara wengi wa tz hasa wa nguo wanachukua bidhaa uganda lkn huko dar utawasikia wakiwaambia wateja wao kua wanaenda china,hong kong,thailand,uturuki nk kuchukua mzigo kumbe yupo majestic plaza huko uganda.

Na bidhaa zao kusema ukweli ni quality haswa na wanajua kwenda na fashion.kitu cha mwaka jana huwezi kipata mwaka huu!
Vipi ukinunua gari Uganda ukija Tz unatozwa kodi kama ile ungetozwa bandarini?
 
Hapo kila mtu anambinu yake yakuyingiza mzigo. Kingine kwa mfano Toyota harrier unaweza kuyinunua hela ya uganda milion 15 ambao ni sawa sawa na million 10. Inategemea na model. Kwahiyo sisi tunacheza tu na dollar wapi chini. Unanua huko

Sent from my GT-N7100 using JamiiForums mobile app
Naomba exchange rate kati ya Uganda na Tz .......tsh :......ug sh

Kwa hiyo unashauri tununue magari uganda
 
Nilimanisha. Mganda na mTZ wakienda kuchukua nguo say kwa dola 5. Either guangzo au shangai wareva.
Mtanzania 5×2500= 12000 TZ sh
Uganda pia dollar ina range kwenye 2500 itakua pia 12000 ug sh.
Sasa inamaana ukibadilisha 12000 itakuja 8000 ya tz kuliko uyichue kwa 15000 bora uende ug ununue kwa 8000. Cjui kama tupo sawa. Mwenye kufanya biashara mwengine atowe uzoef tafadhali

Sent from my GT-N7100 using JamiiForums mobile app
Nipe exchange rate ya Uganda na tz
 
Wanajamvi,

Hapa Niko katika kituo cha Bus liitwalo FRIENDS jijini Kampala (Uganda) nikielekea nyumbani Tz. Ninachokiona hapa ni wafanyabiashara wa Ki-Tz toka Dar na Mwanza wamefungasha mizigo ya nguo, viatu, na vifaa vya MAGARI kuvileta Tz.

Najiuliza inakuwaje vitu ni bei nafuu zaidi Uganda ijapokuwa hawana bandari? Mizigo yao yote hupitia Bandari ya Dar na Mombasa lakini bado vitu ni bei nafuu kiasi kwamba watanzania wanavifuata huku!!

Naomba wanauchumi mlioko hapa mtuelewesha Tz kuna tatizo gani? Hii bandari ya Dar, Tanga na nyinginezo zinatunufaishaje??

Mungu Ibariki Tanzania
Tumefundishwa vibaya kudhibiti shughuri za Bandari zetu. Ushauri wao umetupeleka chaka, sawa bidhaa zinazopitia bandari za tanzania hazinunuliki kwa ukali wa bei, wafanyabiashar wote wanazikimbia. Wawe wa Tz au hata wale wa nchi za SADIC na COMESA.
Tutafakari udhibiti wetu na kustakabari wa shughuri zatu za kiuchumi.
 
Mani, hiyo concept ya Kodi kubwa inabidi kuifikiria zaidi.

Ukisema hivyo ina maana wafanya biashara wengi hawalipi Kodi wanapoingiza mzigo kuja Tanzania. Je hii ni kweli.
Sometimes kuwa soft kwenye ukusanyaji wa kodi kunasaidia kujenga uchumi wa nchi. Ndio maana jamaa alikuwa soft kwenye kukusanya kodi, lakini kila MTU alifurahia maisha. Huyu wa sasa yuko very tight ila kila MTU anachukia maisha. It is just a matter of strategies tu basi.
The same ndio ambayo inatumika na Uganda, ambayo pia hutumika mpakani MUTUKULA.
Kwepesha kodi ili maisha(multiplically) yaendelee
 
Titty, lakini inakuwaje sasa kwamba UG hawana bandari lakini bado wanafikisha mzigo hapa kwa bei nafuu kiasi kwamba wafanyabiashara wetu wanatoka Dar/Mza na kununua hapa; na wakifikisha TZ wanauza na kupata faida!! Something is not connecting well here. Kwa mantiki hii, ingebidi wafanyabiashara wa UG ndio waje TZ kununua mzigo.

Nimeelewa point yako; lakini hili la mzunguko wa mzigo hadi ufike Kampala na bado ukaweza kununuliwa kwa faida na Mfanyabiashara wa TZ limekaaje???
Ni walaini kwenye masuala ya ukusanyaji wa kodi, jambo ambalo linaruhusiwa kiuchumi ni kiforodha. Watu wa forodha wao wanatakiwa wafacilitate trade na sio kuwa chanzo cha kujusanya kodi. Kuwa Laini kwenye kukusanya kodi za kiforodha ili maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom