Wafanyabiashara kugoma kulipa kodi: RC Mbeya asema, mkisikia mlio tulieni tu. Mjue wanaume wako kazini na sitaki kuulizwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuna watumishi wanaoshirikiana na wafanyabiashara kuhujumu mapato ya Serikali mkoani hapa, kuapa kuwashughulikia kuanzia sasa.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Oktoba 9, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa idara, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mbeya katika kikao kazi kilichofanyika mjini hapa.

Amesema kuna wafanyabiashara wanajiita ‘vidume’ na hawataki kulipa kodi na kila anapowaita kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo wamekuwa na majibu yasiyofurahisha.

Amesema lazima afanye jambo kuonyesha kuwa Serikali ipo na haijaribiwi.

“Unawaita tuzungumze wanajibu ‘So arrogantly’ halafu wanam-copy barua Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), Rais (John Magufuli) na makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan). Sasa ili kudhihirisha kwamba Serikali ipo, nimempigia simu Suleimani Jafo (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),” amesema.

“Nikampigia Waziri Mkuu nikawaambia mkisikia mlio tu nyie kaeni kimya. Kwa hiyo na nyie mkisikia mlio tulieni tu. Mjue tu wanaume wapo kwenye kazi za kawaida na sitaki kuulizwa.”

Amesisitiza, “ni shoo ambayo itaonekana…, mnasema Mbeya pagumu? Mbeya pagumu hakuna ugumu wagumu ni sisi wachache tuliojigeuza kuwa wezi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kuhujumu. Na huu ndio ukweli kinashindikana vipi kama sheria zipo?”

Alisema tangu 2007 lilipoungua soko la Mwanjelwa, wafanyabiashara hawajawahi kulipa kodi na hata walipohamia soko la Sido, kwamba hataweza kuvumilia suala hilo na atachukua hatua stahiki ambazo hatapenda kuona analalamikiwa kwa uamuzi wake.

“Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya haijakusanya kodi katika soko la Mbalizi tangu mwaka 2016 mpaka leo, ukiwauliza kwa nini eti walipandishiwa kodi kidogo halafu wao (wafanyabiashara) wakapeleka mapingamizi yao mahakamani wakipinga kupandishiwa kodi kwenye nyumba ya halmashauri,” amesema.

Amesema soko la Sido halijawahi kuingiza chochote kwenye halmashauri ya Jiji tangu mwaka 2007 lilipoungua soko la Mwanjelwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema miaka ya nyuma Mkoa ulikuwa ukikusanya mapato kwa asilimia 80 lakini mwaka huu wamekusanya kwa asilimia 71.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika amesema, “mamlaka na madaraka vyote vinavyo hivyo nilikuwa nasubiria tu kauli yako mkuu wa mkoa, na sasa nakwenda kuchukua hatua dhidi ya wale wote ambao hawataki kulipa kodi.
 
Hizi kauli ngumungumu kama tupo jeshini,

Embu jaribuni kuwa na staha kwenye mazungumzo, sio kutishatisha watu na kuonesha wewe ni katili au mwamba!!
 
Wewe mteule wa maraika MKUU dai kodi kwamjibu wa Shelia sio unavyotaka wewe kununulia wanasiasa pesa ya walipa kodi ni uhujumu uchumi
 
“Nikampigia Waziri Mkuu nikawaambia mkisikia mlio tu nyie kaeni kimya. Kwa hiyo na nyie mkisikia mlio tulieni tu. Mjue tu wanaume wapo kwenye kazi za kawaida na sitaki kuulizwa.”
Hii kauli mbaya sana kutolewa na kiongozi kwenye nchi inayojinasibu kuendeshwa Kidemokrasia. Hawa CCM sijui ni kujiamini ama ndiyo wazimu unawapanda!!
 
“Unawaita tuzungumze wanajibu ‘So arrogantly’ halafu wanam-copy barua Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), Rais (John Magufuli) na makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan).
====
Hao wafanyabishara kiboko.!
 
“Unawaita tuzungumze wanajibu ‘So arrogantly’ halafu wanam-copy barua Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), Rais (John Magufuli) na makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan).
====
Hao wafanyabishara kiboko.!
Hawawezi kugoma hivi hivi tu bali watakuwa na sababu za msingi na ambazo zinapuuzwa.
 
Hii kauli mbaya sana kutolewa na kiongozi kwenye nchi inayojinasibu kuendeshwa Kidemokrasia. Hawa CCM sijui ni kujiamini ama ndiyo wazimu unawapanda!!
Hivyo hujamsikia mwenyewe akijinadi kule mkoani Mara kuwa yeye ni kichaa na anateua vichaa wenzake katika serikali yake??

Hivi unategemea kauli gani imtoke huyo Mkuu wa Mkoa?
 
Karibu Mbeya kichwa nazi....Hawataishia hapo,watakupa kichapo na watam-copy rais,makamu wa rais na waziri mkuu.
 
swala la kod halikwepeki wafanyabiashara walipe kodi
Hakuna anekataa kulipa kodi. Sheria za kodi zipo. Hivyo anatakiwa awaachie wataalam wa kodi. Usipolipa kodi TRA wanakuandikia barua usipoitikia wito unaandikiwa nyingine na kupewa siku 7 au 14. Baada ya hapo sheria inachukua mkondo wake yaani kuna kufungiwa sehemu ya biashara na kupelekwa mahakamani. Mkuu wa mkoa siyo mtaalamu wa kodi ndio maana kuna idara mbali mbali. Lkn kwa vile serikali hii ni ya maguvu wakuu wa mikoa, wilaya ndio wamegeuka TRA na kuacha kazi zao za ukuu wa mkoa
 
Baadhi ya ma-RC na ma-DC wa awamu hii, ni moja ya sababu kubwa ya CCM hii ya Magu kuchukiwa na wananchi na kwa hakika watachangia anguko la CCM kwasababu wenye mamlaka wameamua kuwalinda na kuwaacha wafanye watakavyo hata kama wanavunja sheria.
Huyu RC hata muonekano wa kichwa chake haionyeshi kama ni mtu mwenye akili timamu
 
Back
Top Bottom