The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 508
- 968
Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wamehoji juu ya usahihi wa takwimu alizopewa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa jengo la ghorofa lililoanguka Kariakoo Novemba 16, 2024 lilikuwa limebeba mizigo ya tani 850.
Akizungumza leo Februari 04, 2025 katika uzinduzi wa Balozi Jengo, Fredrick Lutindi ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo amesema “wakati Mheshimwa Rais anaongea kuna takwimu alizitaja mimi na wafanyabiashara wengi tulishtuka kidogo kwamba jengo lile lililodondoka lilikuwa limebeba tani 850 sasa tani mia nane kwa kawaida Kariakoo hatuna jengo lenye uwezo wa kubeba tani hizo”
Wafanyabiashara hao wamemuomba Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda kusaidia kufuatilia ili Rais apewe taarifa zilizo sahihi hasa hizo za kiwango cha mizigo kilichobebwa kwenye jengo lililoanguka.