Wafanyabiashara Iringa wamkimbia Pinda, msafara wake magari yagongana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyabiashara Iringa wamkimbia Pinda, msafara wake magari yagongana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 8, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  SHEREHE ZA MIAKA 35 YA CCM IRINGA NI MKOSI MTUPU,
  WAFANYABIASHARA WAMKIMBIA PINDA  SHEREHE za miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa ni mkosi mtupu ni baada ya wabunge waliokuwemo katika msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda magari yao kugongana eneo la Kinyanambo Mafinga pamoja na baadhi ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Iringa kukwepa kukabidhiwa vyeti vya pongezi na waziri mkuu Mizengo Pinda katika sherehe fupi ya iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Iringa mjini kwa lengo la kuwakabidhi vyeti hivyo kutokana na misaada yao mbali mbali ambayo wamekuwa wakijitolea kwa ajili ya kusaidia kufanikisha shughuli za chama mjini Iringa.

  Hatua ya wafanyabiashara hao kususia sherehe hiyo jana ambayo awali ilipangwa kufanyika Ikulu ndogo ya mkoa wa Iringa na kubadilishwa ghafla kwenda kufanyika katika viwanja vya ndege Nduli ilijitokeza muda mufupi baada ya uongozi wa CCM wilaya ya Iringa mjini kubadili ratiba na kuwataka wafanyabiashara waliokuwa wamekusanyika eneo hilo kuendesha magari yao kwenda uwanja wa ndege Nduli suala ambalo lilionekana kuwa gumu kutekelezwa kwa baadhi ya wafanyabiashara hao.

  Mmoja kati ya wafanyabiashara hao ambaye hakupenda jina lake kutajwa ktk mtandao alisema kuwa uamuzi huo wa CCM kuwaandalia sherehe ya kukabidhiwa vyeti vya pongezi ulikuwa mzuri kwa maana ya kuthamini mchango wao kwa chama ila hawakupendezwa na hatua ya chama kuwakalisha kwa muda mrefu katika viwanja vya Ikulu na baadae kuwataka kwenda uwanja wa ndege nduli.

  "Tulichokiona hapa ni kama kupotezeana muda zaidi kwani haiwezekani CCM wilaya ya Iringa mjini ikafanya sherehe hizo bila kuwasiliana na uongozi wa mkoa na kupanga ratiba ya pamoja......kweli zaidi ya wafanyabiashara 30 hawakuweza kufika kupokea vyeti hivyo vya pongezi "

  Hata hivyo alisema kuwa iwapo CCM itaendelea na ubabaishaji huo katika shughuli zake upo uwezekano mkubwa wa baadhi ya wadau wa chama ambao wamekuwa mbele kujitolea kwa ajili ya kazi za chama kuvunjika moyo kufanya hivyo.

  Msafara wa Picha wapata ajalli, Magari ya Wabunge yagongana.
  Wakati huo huo Magari ya wabunge wa CCM waliopo katika msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda yaligongana mjini Mafinga eneo la Kinyanambo ,wakati msafara huu ukielekea Iringa ukitoka katika Sherehe za miaka 35 ya CCM zilizofanyika kimkoa kijiji cha Ifwagi kata ya Ifwagi wilaya ya Mufindi .

  Wabunge walionusurika ni Ritta Kabati ,Lediana Mng,ong,o wote wa viti maalum mkoa wa Iringa ,mwenyekiti wa wabunge wa CCM mkoa wa Iringa na mbunge wa jimbo la Kalenga Dr wiliam Mgimwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigolla pamoja na waandishi wahabari wa Chanel Tena Daud Mwangosi na mwandishi wa habari hizi Francis Godwin ambao wote wamenusurika kifo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea sasa saa 10 .00 jioni .

  Chanzo cha ajali hiyo ni mmoja kati ya magari yaliyokuwemo katika msafara huo kusimama gafla katika eneo hilo lenye mteremko mkali huku upande wa kulia kukiwa na msululu mrefu wa mabasi ya abiria ,malori na magari madogo ambayo yalikuwa yamezuiliwa ili kupisha msafara huo wa waziri mkuu.

  Katika ajali hiyo gari la mbunge Mng'ong'o lenye namba za usajili T 758 APJ Toyota Land Cruse lililigonga kwa nyuma gari la mbunge wa jimbo la Kalenga lenye namba za usajili T 162 AHN Nisani gari ambalo wabunge wawili mbunge Kabati na Kigolla pia walikuwemo.

  Awali msafara huo wa waziri mkuu wakati ukielekea mjini Mafinga gari la katibu wa CCM mkoa wa Iringa ambalo pia lilibeba waandishi wa habari ,viongozi wa jumuiya za CCM mkoa ,katibu mwenezi wa CCM mkoa na mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa Deo Sanga liliangusha begi la mbunge huyo eneo la Ihemi ,begi ambalo lilikuwa limewekwa juu ya kelia ya gari hilo bila kufungwa .
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,329
  Trophy Points: 280
  Du!. Hii kali!
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  huu ni mwanzo tuu
  the worst to come
  only time will tell
   
 4. A

  Alfred Ngowi Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Tulichokiona hapa ni kama kupotezeana muda zaidi kwani haiwezekani CCM wilaya ya Iringa mjini ikafanya sherehe hizo bila kuwasiliana na uongozi wa mkoa na kupanga ratiba ya pamoja......kweli zaidi ya wafanyabiashara 30 hawakuweza kufika kupokea vyeti hivyo vya pongezi " sasa wamemkimbia Pinda au ni mkorogano wa ratiba na sehem ya kufanyia hio shughuli???? nna ,mashaka na unacholenga hasaa... unadhamiria kupotosha maana nzima ya hio habari... lakini nisikulauma kwakuwa inaonekana uwezo wako mdogo saanaaa... pole...
   
 5. z

  zamlock JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  cha moto bado
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maumivu ya kichwa huanza polepole.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hiyo raba nyeupe kwa mkuu chini baada ya black trouser na green shirt balaa
  Duh hizo mchanganyiko wa colour
   
 8. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  huyu dingi "mokasin"
  kajifunza kuvaa majuzi
  baada ya kinajoti kumcheka.na bora hao wafanyibiashara
  wamesepa zao wakaendelea kusaka ngawira kuliko
  kupotezewa mda
  usawa huu mgum
  uliosababishwa na haohao ccm!!
   
 9. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Bila shaka hii Habari ni kutoka Tanzania Daima
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Taswira hiyo umeisoma vema, kwani kuchanganyikiwa kwa mtu si lazima kuokota makopo. Hata Mama Pinda alishindwa kumtonya mzee avae vipi, hapa nisawa na kuvalia zile kata mbuga miguuni wakati katilia ile western professional suit.

  Kiongozi wetu anaonekana asivyoweza kuweka sawa mambo katika shughuli zake za kawaida ndivyo inavyoashiria katika mvao wake pia.

  Angekuwa mtu anayeweza kupangilia mambo kwa busara mgomo wa madaktari usingefikia hapa ulipo leo. Hii ndiyo sawa na kutilia mguni snicker isiyoendana na mfumo wa mvao wa mavazi aliyovaa.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Habari hii haitoki Tanzania daima, viginevyo husomi vizuri chanzo cha habari hii kipo wazi kama utabofya kichwa cha habari. Mwandishi wa habari hii ni shuhuda kati ya wale waandishi waliokataa kulazwa na CCM kwenye guest ya wafanya ufuska.
   
 12. MANI

  MANI Platinum Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280

  Mkuu Rock unadhifu una asili !
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sina cha kuongeza
   
 14. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hivyoo mgomo wa madaktari upo wapi vile? kenya nini, hawezekani watu wafwile wewe uende kwenye sherehe
   
 15. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  cheki yule mama pembeni anavotembea majesticallyt utadhani mkulu anaeza mpa hata ukuu wa wilaya,sijui lakini ajitahdi mana mkulu nae haeleweki
   
Loading...