Wafanyabiashara 36 waliouza sukari tofauti na bei elekezi wakamatwa katika Mikoa 6

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas ameeleza Jeshi la Polisi nchini linaendelea kufanya Operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wanaouza sukari kinyume na bei elekezi ya serikali

Operesheni hiyo ambayo ilianza kufanyika 25/04/2020 ikiongozwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Bodi ya Sukari, Tume ya Ushindani pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo hadi sasa imefanikiwa kuwakamata Jumla ya watuhumiwa 36 katika mikoa ya Dar Es Salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga huku jumla ya tani 106,939 za sukari zikiwa zimekamatwa katika mikoa hiyo.

Aidha, Kamishna Sabas amesema kuwa, hali ya nchi yetu kwa sasa ni shwari hakuna matishio yoyote ya kiuhalifu na kwamba operesheni mbalimbali ikiwemo misako bado zinaendelea huku akiwataka wananchi kutokuogopa vipima joto vinavyotumiwa na Jeshi la Polisi wawapo vituoni kwa ajili ya kukabiliana na janga la Virusi Corona.
 
Hivi bei elekezi ni sh. ngapi nchi nzima? Maana huku 1 kg ni sh. 4000/=
Mimi huku nilipo bei elekezi ni 3000 japo kuna sukari ya Zambia bei ni 2700 madukani ila kuna wanaopitisha majumbani hao wanauza 2500 @kg
JPEG_20200430_141051_1519759748.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamishna Sabas amesema kuwa, hali ya nchi yetu kwa sasa ni shwari hakuna matishio yoyote ya kiuhalifu na kwamba operesheni mbalimbali ikiwemo misako bado zinaendelea huku akiwataka wananchi kutokuogopa vipima joto vinavyotumiwa na Jeshi la Polisi wawapo vituoni kwa ajili ya kukabiliana na janga la Virusi Corona
TUNAWAPONGEZA SANA SANA SANA MAKANDA WETU. HEBU TUSAIDIENI KUTUTETEA WANYONGE SIE JAMANI.

YAANI KILA MWAKA IKIINGIA RAMADHANI TU, BEI YA SUKARI NDIO MSIMU WA KUPANDA NA HAISHUKI !!! KWA KWELI MNAFAFANYA KAZI NZURI SANA.
 
Hawa jirani zetu wanatumia techolojia gani kupata sukari toshelezi na bei rahisi kiasi hichi?
Tanzania tunakwama wapi?
Kwakweli sijui tunakwama wapi sasa hapa mimi nipo city centre ila kuna jamaa anasema hiyo sukari ya Zambia Tunduma bei kwakilo moja ni 1800 kwa jumla na 2000 kwa rejareja. nazani tunahitaji kujifunza toka kwa majirani zetu waliofanikiwa
 
Leo mmenifurahisha ila vip wao walinunua kwa bei gani na kati yao wapo watakao pata kesi za uhujumu uchumi baada ya kukutwa hawana risiti za manunuzi
 
Back
Top Bottom