Wafanya kazi wa halmashauri wawe wanahamishwa ili wasijisahau na kuota miziz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanya kazi wa halmashauri wawe wanahamishwa ili wasijisahau na kuota miziz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ISOPOWER, Oct 17, 2012.

 1. I

  ISOPOWER Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  CHANZO cha Halmashauri ya Ngara kupata hati chafu kwa miaka miwili mfululizo imeelezwa kuwa imesababishwa na watumishi kufanya kazi kwa mazoea.
  Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Constantine Kanyasu, alibainisha hayo mwishoni mwa wiki katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ( RCC) Mkoa wa Kagera wakati Mwenyekiti wa kikao hicho, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alipotaka kuelezwa sababu za halmashauri hiyo kupata hati chafu.
  Kanyasu alisema wafanyakazi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kisingizio kuwa watumishi ni wachache, jambo ambalo halina ukweli.
  “Binafsi nimeshuhudia baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kwa mazoea wala hawamheshimu mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wao,” alisema.
  Alisema serikali inapaswa kuwa na utaratibu wa kuhamisha viongozi mara kwa mara, ili kuepukana na tatizo la kufanya kazi kwa mazoea katika halmashauri mbalimbali nchini.
  Alisema watumishii katika halmashauri hiyo wana zaidi ya miaka 10 hawajahamishwa, hali ambayo inachangia kuwapo kwa hali hiyo
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Utaratibu wa serikali kuhamisha watu hautumiki sana siku hizi wanaogopa gharama za kumhamisha mtumishi. Uhanmisho rahisi siku hizi ni ule wa kujihamisha au kujigharimia ndio maana watu wanazoea vituo vya kazi.
   
Loading...