Ilianza kama utani Shirika moja la enzi hizo za utawala wa mwalimu Nyerere lilokuwa na ukwasi wa kutosha enzi hizo lilipokea taarifa kutoka kwa wezi kuwa siku ya tarehe_ _ mwezi wa _ _ wangefika kufanya wizi wa fedha kidogo hapo kwenye jengo la shirika hilo
Basi viongozi wa shirika waliichukulia hii taarifa kwa uzito wakaiwasilisha kwa vyombo vya ulinzi na usalama nao bila hiyana wakaongeza askari wa kutosha wa kulinda jengo la shirika hilo bila kusubiria tarehe tajwa na wale wezi
Basi masaa yakapita siku zikapita mwisho tarehe tajwa na wale wezi ikafika,ulinzi ukaimalishwa,ziara za viongozi wa juu wa jeshi la polisi za kulitembelea jengo tajwa zikaongezeka.Kwa tathmini iliyofanywa na wakubwa wa jeshi la police ilionekana hakutakuwa na uwezekano wa mwizi kwenda kufanya wizi eneo hilo
Masaa yakapita,yakapita na kupita mara ghafla ikafika gari ya police ikiwa na maafisa wenye vyeo vya juu.Salute zikapigwa,pongezi zikatolewa halafu wakaingia ndani kuangalia hali ya usalama.Wameingia ndani mpaka kwa meneja,wamepewa viti wakae badala ya kukaa wakachomoa vyuma( mitutu) na kumpatia amri meneja ya kuyajaza mabegi waliyokuwa nayo pesa,meneja kafanya alivyoamriwa na kuwakabidhi mabegi yao,akapatiwa amri ya kuwasindikiza nje tena akiwa na tabasamu la maana
Maafisa na nyota zao wakafanikiwa kutoka wakiongozwa na mateka wao mpaka nje wakaingia kwenye gari lao wao na meneja haoooooo,meneja wakamtelekeza mahali fulani,wao haooo wakajiendea zao sehemu isiyojulikana bila hofu yoyote ya kuiba pesa za shirika la umma
Taarifa za wizi wa mapesa rundo ya shirika la umma zikamfikia Nyerere,mbinu iliyotumiwa na wezi akaelezwa,mwalimu Nyerere akajikuta ametabasamu na kuwamwagia pongezi tele wezi wenye akili zao