Wafahamu wapinzani wa sera za CCM

Mlanga

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,023
467
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1990
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania chini ya CCM (mfumo wa chama kimoja cha siasa)
iliamua , baada ya kura za maoni zilizokuwa na matokeo haya:
  1. 80% ya wananchi hawakutaka mfumo wa vyama vingi
  2. 20% ya wananchi waliafiki kuwepo kwa mfumo wa uongozi wa vyama vingi.
Muasisi wa CCM (Hayati Baba wa Taifa-Mwl.J.K.Nyerere)
akiwa hai alifanya kampeni za mwanzo za uchaguzi wa Rais
chini ya mfumo wa vyama vingimwaka1995
kwa kumnadi Mhe .Benjamin W. Mkapa .

Mpaka hapo ni dhahiri kuwa sera hii iliyoanzisha mfumo wa uongozi wa vyama vingi
ni sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Sera hii haikufikiwa na kudumu hadi leo bila ya gharama (kuanzia mchakato wa kura ya maoni ruzuku za vyama, chaguzi nk)

Hivyo basi leo hii akitokea au watu kutoka CCM au vyama vingine anayesema
  • hataki kusikia upinzani/wapinzani au
  • atahakikisha upinzani unakufa
Mtu au watu hao moja kwa moja ni mpinzani/wapinzani wa
Chama Cha Mapinduzi
 
Hao asilimia 80 waliokataa vyama vingi walikiwa mbumbumbu ndiyo maana Mwl Nyerere aliona bora awasaidie tu. Viongozi wa kiafrika wanatumia sana umbumbumbu wa raia wake kuwatawala kimabavu na kuwaonea. Wanajua hakutokuwa na reaction yoyote kwa wananchi wasioelewa sana mambo.

Nikirudi kwa hao wanaotaka upinzani ufe hao ni madikteta uchwara tu wanasumbuliwa na inferiority complex.

Ukiwa kiongozi mkuu halafu mshamba ni tabu sana.

Mwambieni hatumuogopi hata kidogo. Yeye kama ilivyokuwa kwa wengine atapita kama upepo
 
Back
Top Bottom