Wafahamu Wanefili (majitu makubwa) walioitesa dunia hadi Mungu akaamua kuwaangamiza

Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,652
8,542
Wanefili ni nani? wanefili maana yake ni majitu makubwa, hawa majitu kama Goliathi, Ahimani, sheshai, Talmai, Safu, Lahmi nk walijulikana katika agano la kale.

Hawa walikuwa ni wanadamu waliozaliwa kutokana na mahusiano ya kimapenzi kati ya wana wa Mungu na binadamu, wana wa mungu hawa walikuwa ni malaika walioanguka(mapepo) ambao walioa wanawake binadamu waliwapata kwa nguvu za giza za mapepo hayo uhusiano huu ulisababisha kuzaliwa watoto Wanefili (MAJITU MAKUBWA) mwanzo 6:4.

Wanefili walikuwa kizazi kikubwa sana cha mashujaa maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa sana. Ukubwa na nguvu zao ulitokana na mchanganyiko wa chembe za damu ya mapepo na binadamu.

Hata hivyo kizazi hichi kiliangamizwa na gharika wakati wa NABII NUHU

View attachment 411514
neph1.jpg
neph3.jpg
nephilim-giants.jpg
 
Na Chakula cha kuwalisha wanyama waliokuwa kwenye safina katika kipindi chote cha gharika kilitoka wapi? Au nani aliyekuwa anawahudumia ikiwemo kusafisha kinyesi chao?
Kitabu cha mwanzo kinaeleza wazi Mungu ndie alimwambia nuhu atengeneze sana akampa na vipimo na jinsi yakuingiza wanyama mle ndani!!! Ukisoma kirabu cha daniel kinaonyesha wazi Mungu alivifunga vinywa vya simba wasiwadhuru akina daniel!!! Mungu ndie muumbaji hashindwi na lolote
 
Hivi siku ya kujifungua huyo mama ambaye ni binadamu anakuwaje?Na je malika wana jinsia gani?Maana hao malaika walioasi waliwaingilia binadamu ambao maumbo yao ni madogo.Nyume zao zilipenyaje katika sehemu za wanawake binadamu?Mtoto aliyezaliwa alikuwa na ukubwa gani na alizaliwa kawaida au kwa upasuaji?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom