clion dismas
Senior Member
- Aug 6, 2017
- 185
- 170
Wanabodi
Naomba niwaletee kwenu hawa wataalam kwenu, dondoo juu ya wakifanyacho na umuhimu wao kwa wale wote wanaofanya kazi, karibuni.
OSHA, kwa kirefu ni Occupational Safety and Health Authority. Ni taasisi ya kujitegemea, iliyoko chini ya ofisi ya waziri mkuu, sera,bunge,kazi,ajira,vijana na walemavu.
Taasisi hii iliundwa chini ya sheria ya wakala wa serikali Na.30 ya mwaka 1997 ambayo majukumu yake yamechanganuliwa katika sheria ya usalama na afya mahala pa kazi Na.5 ya mwaka 2003.
Rasmi ilianzishwa tangu tarehe 31/08/2001 chini ya shwria ya wakala Na.30 ya 1997 kwa minajili ya :-
1. Kuboresha hali ya usalama na afya mahala pa kazi, ikijumuisha;
2.Kufanya kaguzi za afya na usalama;
3. Kufanya chunguzi za afya kwa wafanyakazi mahala pa kazi;
4. Kufanya mapiyio ya tathmini za athari za kiafya na kiusalama mahala pa kazi;
5. Kutoa leseni baada ya kukidhi matakwa ya sheria ya afya na usalama mahala pa kazi;
6. Kusajili mahala pote pa kazi na kuwasaidia kupata lesini na kufikia viwango vya kukidhi kupata leseni ya ubora;
7. Kuhakiki ramani na michoro yote ya majengo sehemu za kazi kabla ya ujenzi kufanyika;( kwa mujibu ya sheria Na.5, ibara ya 16 ibara ndogo ya 1 ya mwaka 2003, " mtu yeyote anapaswa kusajili kiwanda/eneo la kufanyia kazi kabla ya kuanza kufanya kazi hapo".;
8. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusiana na maswala ya afya kazini pamoja na kutia elimu juu ya umuhimu wa usalama mahala pa kazi.
Jambo jema ni hili, usajili wa eneo la kazi ni bure kabisa, hakuna tozo yoyote ile. Punde unaposajili eneo lako la kazi utapewa cheti cha osha.(mfano wa cheti ni hiki hapa)
Aidha, OSHA inatoa huduma ya kozi mbalimbali ambazo ni lazima kwa mujibu wa sheria Na.5 ya 2003 ili kurahisisha usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi kama vile:-
1. Huduma ya kwanza na kamati za afya na usalama mahala pa kazi(Industrial first aid, safety and health representative respectively). Mafunzo mengine kwa ajili ya afya na usalama uhusisha;
2. OHS Risk assesment
3. OHS in construction industry
4. Accident investigation
5. Workplace exposure assesment strategy
6. Safe use of chemicals at work place and
7. Working at height.
Haya yote yanafanyika ili mfanyakazi mahala pa kazi awe katika usalama na ajali au hatari yoyote ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kuzuiliwa au kupunguza madhara pale itakapotokea.
Kaguzi zinazofanya na wataalamu wa osha ni pamoja na:-
1. General safety inspection
2. Electrical inspection
3. Plant inspection
4. Medical inspection
5. Industrial hygiene
6. Ergonomics inspection
Kila kaguzi tajwa juu hapo ina gharama zake.
Zaidi ifahamike kwamba OSHA inafanya kazi karibu sana na shirika la kazi la kimataifa (ILO).
KUMBUKA
NI HARAMU KUFANYA KAZI BILA KUISAJILI KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA NA. 5 YA MWAKA 2003, IBARA YA 16 IBARA NDOGO YA KWANZA.
Ofisi za osha zimejengwa katika kanda tofauti tanzania, zikihusisha:-
1.Kanda ya ziwa
2.Kanda ya pwani
3.Kanda ya kaskazini
4.Kanda ya kati
5.Kanda ya ndanda ya juu kusini
6. Kanda ya kusini
( zaidi tembelea, www.osha.go.tz)
SAJILI LEO ENEO LAKO LA KAZI KUEPUKA USUMBUFU BAADAYE UKIBAINIKA ULIKWEPA KIUJANJA. WENYE VITAMBULISHO KWA UMACHINGA HAWAJISAJILI NA OSHA, YAANI, MWENYE MTAJI CHINI YA MILIONI 4 KWA MWAKA.
"USALAMA NA AFYA NA MSTAKABALI WA KAZI KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA".
Barikiwa