Wafahamu wagombea Urais wawili wenye ushawishi mkubwa:Edward Lowassa na Dr. John Pombe Magufuli

Mar 2, 2012
57
17
lowassa-ukawa.jpg

Edward Ngoyai Lowassa in brief.


Edward Ngoyai Lowassa
alizaliwa August 26, 1953,Edward Lowassa ni mtoto wa nne kuzaliwa katika ya Mzee Ngoyai Lowassa ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa muda katika serikali ya Wakoloni (wakati huo). Edward Lowassa alijiunga na shule ya msingi Monduli (ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuitwa Moringe Sikoine) mwaka 1961.Mwaka 1968 alijiunga na shule ya upili Arusha Sekondari na baadae mwaka 1972 akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita shule ya wavulana Milambo sekondari. Alifanikiwa kuendelea na elimu ya chuo kikuu, mamo mwaka 1977 alihitimu Shahada yake ya kwanza ya sanaa ya Ubunifu na Maonyesho chuo kikuu cha Dar es Salaam.Baadae alijiendeleza na kusoma shahada ya uzamili ya maendeleo (Development Studies) katika chuo kukuu cha BATH kilichopo Uingereza.

Edward Ngoyai Lowassa alianza fanya kazi kama waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu kipindicha Mwinyi.Mwaka 1995 akategemewa kuwa mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi ila akaenguliwa mapema na Mwalim J.K Nyerere kwa kile alichoamini kuwa hakuwa mtu sahihi.Aliendelea kuitumikia CCM na kuwa mtu muhimu mpaka mnamo 1997 alipoteuliwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais mazingira na umasikini.Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo,mwaka 2005 hakugombea ila alikuwa campaign manager wa Kikwete na kusababisha ashinde kwa kishindo.Disemba 29, 2005 aliteuliwa na Jakaya Kiwete kuwa Waziri Mkuu na mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali. Lowassa anasadikika kuwa na historia iliyotukuka Bungeni na Serikalini.

Mapema mwaka 2014 Edward Ngoyai Lowassa alifungiwa na chama chake kwa tuhuma za kuanza kufanya kampeni za mbio za Urais mapema. Mai 2015 alifungua rasmi kampeni zake za mbio za Urais huko Arusha akiainisha vipaumbele vyake vya Elimu,kupunguza Umasikini, kukuza Uchumi na kupambana na Rushwa. Hata hivyo kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi haikupitisha jina lake.

Alihamua kukihama chama chake na kujiunga UKAWA ambao ni muunganiko wa vyama vinne na Agosti 4, 2015 alitangazwa kama mgombea nafasi ya Urais kupitia muunganiko huo wa vyama vinne wa UKAWA.

Nyadhifa alizofanyia kazi ndugu Edward Lowassa


  • Mkurugenzi Mtendaji – Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano Arusha 1989-1990

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais (Mahakama na Bunge) 1990-1993
  • Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi 1993-1995
  • Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na umasikini 1997-2000
  • Waziri wa maji na Mifugo 2000-2005
  • Waziri Mkuu 2005–2008 na
  • Mbunge wa Jimbo la Monduli 1900 mpaka sasa ambapo ni mgombea nafasi ya Urais kupitia UKAWA.


    magufuli.jpeg

    Dr John POmbe Magufuli in Brief

    Dr John Pombe Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959. Alianzan elimu ya msingi mwaka 1967 shule ya msingi Chato, mwaka baadae kujiunga na shule ya upili mnamo 1977 shule ya lake Mwanza na baadae 1975 akahamia Katoke seminari ambapo alimalizia elimu yake ya upili. Aliendelea na kidato cha tano na sita mwaka 1979 shule ya sekondari Mkwawa.

    Mwaka 1981 alijiunga na chuo cha elimu Mkwawa ambapo alichukua astashahada ya sayansi ya elimu ya Kemia na Hesabu.Mnamo 1985 akaendelea na masomo ya elimu ya juu ngazi ya chuo kikuu na kufanya masomo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya Kemia na Hesabu. Baadae 1991 akaendelea na shahada ya uzamili katika somo la sayansi ya Kemia katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam,Tanzania na Stanford,Uingereza. Mwaka 2006 akamalizia shahada ya Uzamivu ya sayansi ya Kemia chuo kikuu cha Dar es Salaam.

    Dr John Pombe Magufuli alianza kufanya kazi kama Mwalimu wa Kemia na Hesabu shule ya sekondari Sengerema,jijini mwanza kuanzia 1982 mpaka 1983. Mwaka 1989-95 aliajiriwa kama Mkemia wa Nyanza Co-operative Union Ltd ya Jijini Mwanza. Mnamo 1995-2000 alifanya kazi wizara ya Ujenzi kama naibu waziri,2000-2005 akafanya kazi tena Wizara ya Ujenzi lakini kama Waziri. Mwaka 2005-2/8/2008 aliteuliwa na kufanya kazi wizara ya Ardhi na maeneleo ya Makazi kama Waziri kisha Waziri wa Mifuko na Uvuvi kuanzia 2008-2010.Mwaka 2010-2015 amefanya kazi kama Waziri wizara ya Ujenzi. Dr John Pombe Magufuli ameweka rekodi ya kipekee katika Wizara zote alizofanyia kazi. Anatambulika kuwa Kiongozi madhubuti na thabiti kwa kufanya kazi ipasavyo na kwa uadilifu.

    Mwaka huu Dr John Pombe Magufuli alianza mbioza kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais kwa kutafuta wadhamini Nchi nzima huku alkiendelea na ufuatiliaji wa kazi zake Wizara ya ujenzi akiwa miongoni mwa wagombea waliokuwa hawapewi kipaumbele huku mwenyewe akiainisha vipaumbele vya Kufufua viwanda,Kupambana na Mafisadi (wahujumu Uchumi), kukuta sekta ya Utalii,kuimarisha uwekezaji,kusimamia nishati ya gesi na ujenziwa barabara na reli.

    Julai 12, 2015 Dr John Pombe Magufuli aliteuliwa na kupitishwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea nafasi ya Urais na mpeperusha bendera ya chama hicho.

    Nyadhifa alizofanyia kazi Dr John Pombe Magufuli


  • Mwalimu wa Kemia na Hesabu, shule ya sekondari Sengerema 1982-1983
  • Mkemia wa kiwanza cha Nyanza Co-operative Union Ltd-Mwanza 1989-1995
  • Mwanachama,chama cha wa-Kemia Tanzania 1993 mpaka sasa
  • Naibu waziri wa Ujenzi 1995-2000
  • Waziri wa Ujenzi 2000-2005
  • Chemba ya maendeleo Mtwara 2000-2005
  • World Road Congress (PIARC) delegate 2000-2005
  • Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi 2005-2/8/2008
  • UN-HABITAT Co-chair World Urban Forum (III) 2006 to present
  • Waziri wa Mifugo na Uvuvi 2008-2010 na
  • Mbunge wa Jimbo la chato kuanzia 1995 mpaka sasa ambapo anagombania nafasi ya Urais kupitia CCM.
 
Back
Top Bottom