Wafahamu wagombea ubunge na watia nia katika majimbo mbalimbali Tanzania ifikapo 2020

H

HABARI TANZANIA

New Member
Joined
Jul 16, 2019
Messages
1
Points
20
H

HABARI TANZANIA

New Member
Joined Jul 16, 2019
1 20
Habari mwanaJF. The home of great thinkers.
Duniani kote katika nyanja ya siasa kuna mambo na mikakati ambayo ni lazima ipangwe na kutekelezwa ili kuweza kufanikisha matokeo chanya kwa wapanga mipango hao.Siasa ni Mikakati ya kivita, Siasa ni sanaa iletayo utekelezwaji endapo watekelezaji watadhamiria kufanya hivyo.

Kutokana na suala hilo, HABARI TANZANIA kama chombo huru cha habari kimeamua kufanya utafiti na kuujuza umma wa Watanzania kuhusu watu tofauti walioweka nia kupitia vyama mbalimbali vya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao.

Orodha ya Majina hayo ni kama ifuatavyo.
Morogoro.
Jimbo: Morogoro kusini mashariki- FABIAN PETER - Huyu kwa mujibu wa uchunguzi wa HABARI TANZANIA ni kijana muhitimu kutoka chuo kikuu cha Dodoma lakini bado hatujafanikiwa kujua amesomea traaluma gani. Chanzo chetu cha taarifa kimetujuza kuwa kijana huyu ni kutoka chama cha mapinduzi (CCM) na walio wengi wanaomfahamu wanasema kuwa ni kijana aliye na misimamo inayofanana na upinzani hivyo ndani ya chama chake anao upinzani mkubwa katika kura za maoni.

Katika jimbo hilohilo mbunge aliye madarakani ni Mohamed mgumba ambaye inaonekana atagombea tena katika uchaguzi wa 2020 hivyo ni wazi kuwa watashindana na Kijana FABIAN PETER.

Jimbo: Musoma Mjini- Chadema-Vincent Nyerere, Kwa mujibu wa taarifa za awali inaonesha wazi kuwa mbunge aliyeshindwa mwaka 2015 V. Nyerere atagombea katika uchaguzi mkuu ujao.Katika chama Cha Demokrasia na maendeleo kuna watu kama.Ndani ya Chadema inaonekana Nyerere anaweza kuwa mgombea pekee.

Kwa upande wa CCM ni Mathayo Manyinyi mbunge wa sasa japo inasemekana kuwa yeye mwenyewe hana nia ya kugombea uchaguzi wa 2020. Chama cha mapinduzi kina uwezekano wa kupokea ujio wa Msomi Dr. Eliud Eseko Tongola a.k.a Mkorea ambaye wananchi walio wengi wanyo imani kuwa anaweza kuwafanikishia jitihada mbalimbali za maendeleo.

Kutokana na kuwa HABARI TANZANIA inaendele na kufatilia kuhusu watia nia wa majimbo mengine tutaendelea kuwajuza wakuu.

Jioni njema.
 

Forum statistics

Threads 1,335,212
Members 512,271
Posts 32,499,239
Top