Wafahamu Sutherland’s Seven sisters: Sehemu ya Pili 2

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,563
2,045
Tuendelee tulipoishia....

Mara baada ya kufariki kwa wazazi wao, basi ule usemi wa “wazazi ni nguzo; zikidondoka basi nyumba haina faida tena” ukachukua maisha ya mabinti hawa.
IMG_5852.jpg

Walitumia fedha zao kujenga jumba kubwa lenye vyumba kumi na nne, jumba la kisasa (kwa lugha ya sasa ni sawa na kusema self contained rooms) lakini hawakutambua kuwa chuki imeanza kuwajongea taratibu.
Walinunua kila aina ya urembo ili kutia nakshi vyumba vyao.
IMG_5859.jpg

Hawakutembea tena kwa miguu bali walinunua magari ya safari weupe wasio na doa hata kwenye kwato. Farasi hao walivalishwa vipini vya dhahabu huku mito ya kukalia ndani ya magari hayo ikiwa ni vitambaa vya rangi ya dhahabu tu. Mbwa walifugwa ila walifanyiwa treatment sio ya hadhi ya chini Kwani hata mkanda wa shingo na cheni zilikuwa ni dhahabu.
IMG_5853.jpg

Lakini walikuja kukosea na kuamsha laana ya mizimu ya Mama yao ni pale waliajiri wanawake wa kuwachana nywele, kila dada alikuwa na mfanyakazi wake as kumtengeneza nywele asubuhi na usiku kabla ya kulala.
IMG_5863.jpg

Naomi kwa bahati mbaya alifariki akiwa na Miaka 40 na hakubahatika kufurahia maisha matamu ya Jumba Lao. Hapo ndo wadada hawa walipoanza kuvurugwa na maisha.
Walianza kufanya sherehe na kualika watu, kunywa pombe na starehe za usiku kucha, hiyo ikaleta kiburi baina yao na kuanza kutokuongea na Wakati Mwingine kugombana (matokeo hasi ya Pombe).
IMG_5858.jpg

Kama ilivyo Kawaida kwa mtu kuwa na fedha na akili haijatulia, basi harufu ya muwa yenye kiherehere umfanya mlaji kung’atwa na nyuki. Ndivyo hivyo kwenye jumba la madada hawa.
Kijana mmoja Mwenye Miaka 27 tu aitwaye Frederick Castlemaine.
IMG_5866.jpg

Dogo mmoja hivi mfaransa ambaye alimtongoza Dora ila mwishoni akafunga ndoa na Isabela Mwenye Miaka takribani arobaini. Kijana alikuwa anataka fedha hakuwa na mahaba wala nini! Mwaka 1897, akiwa anawasindika kwenye matembezi mashemeji zake pamoja na mke wake, Bwana Castlemaine alijiua, hivyo wadada hawa waliuchukua mwili wa Marehemu Castlemaine na kuupeleka ndani ya chum a kimoja ndani ya jumba lao, waliuweka kwenye jeneza la kioo kisha wakawa wakiiba nyimbo zake pendwa wakati wa uhai wake.
IMG_5862.jpg

Mamlaka ya mji kupitia idara ya afya iliingilia kati na kuwalazimisha kuuzika mwili wa Castlemaine. Kwa Miaka miwili iliyofuata, mke wa Marehemu, Bibiye Isabella alitembea zaidi ya maili tatu kwenda makaburini kila ifikapo usiku kukaa na kuimba. Mpaka siku moja alipokutana na Dogo mmoja anayeitwa Alonzo Swain, kijana mjanja Mwenye Miaka 24. Huyu bi mdada alikuwa anapenda Dogo Dogo tu.
IMG_5856.jpg

Upande wa Dada Mkubwa, Victoria alichukua Dogo mmoja Mwenye Miaka 19, wakati huo Victoria akiwa 50. Huyu alifukuzwa na wadogo zake nje ya jumba baada ya kumaliza mgawo wake kwa Dogo Janja. Alifariki mwaka 1902.
IMG_5860.jpg

Upande wa Isabella, alichukua Dogo mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Swain, Huyu Dogo alimkosanisha Isabella na Dada zake kisha Isabella aliondoka na kwenda nje ya mji, lakini mwaka 1914 Isabella alifariki baada ya Dogo kuchukua fedha alitoweka na kumuacha Isabella mwenyewe, na mwaka 1919 Sarah alifariki.

Mwaka 1926, wadada watatu waliobakia, Grace, Dora pamoja na Mary walisafiri kuelekea Hollywood, wakiwa na tumaini la kuuza hadithi yao ya maisha. Ila Safari yao iliingia doa baada ya Dora kufariki katika ajali ya gari.
IMG_5855.jpg

Upande wa Mary ambaye alikuwa ana ugonjwa wa akili, alitumia muda Mwingi akiwa amefungiwa chumbani kwake na alifariki mwaka 1939. Na Grace alifariki mwaka 1946 na jumba lao lilishika moto na kuungua lote mwaka 1938.
IMG_5853.jpg

Huo ndo mwisho wa historia fupi ya Sutherland’s Seven sisters, kuanzia kuishi maisha ya kifukara, kufanikiwa kimaisha mpaka kudondokea pua. Ingawa maneno ya wajuzi wanadai ni kuwa laana ya wazazi wao imewatafuna Kwani Bi Mkubwa aliwakataza kutokuchana nywele zao.

Asanteni kwa kufuatilia historia hii. Karibuni tena mpaka Wakati Mwingine tena.
Nipo

PIA SOMA:
- Wafahamu Sutherland’s Seven sisters: Sehemu ya Kwanza 1
 
Aisee. Kulikuwa na nn kwenye nywele had bi mkubwa kuwazuia kuzichana? Nahis hapa kuna siri
 
Tuendelee tulipoishia....

Mara baada ya kufariki kwa wazazi wao, basi ule usemi wa “wazazi ni nguzo; zikidondoka basi nyumba haina faida tena” ukachukua maisha ya mabinti hawa.
View attachment 1887146

Walitumia fedha zao kujenga jumba kubwa lenye vyumba kumi na nne, jumba la kisasa (kwa lugha ya sasa ni sawa na kusema self contained rooms) lakini hawakutambua kuwa chuki imeanza kuwajongea taratibu.
Walinunua kila aina ya urembo ili kutia nakshi vyumba vyao.
View attachment 1887148

Hawakutembea tena kwa miguu bali walinunua magari ya safari weupe wasio na doa hata kwenye kwato. Farasi hao walivalishwa vipini vya dhahabu huku mito ya kukalia ndani ya magari hayo ikiwa ni vitambaa vya rangi ya dhahabu tu. Mbwa walifugwa ila walifanyiwa treatment sio ya hadhi ya chini Kwani hata mkanda wa shingo na cheni zilikuwa ni dhahabu.
View attachment 1887149

Lakini walikuja kukosea na kuamsha laana ya mizimu ya Mama yao ni pale waliajiri wanawake wa kuwachana nywele, kila dada alikuwa na mfanyakazi wake as kumtengeneza nywele asubuhi na usiku kabla ya kulala.
View attachment 1887150

Naomi kwa bahati mbaya alifariki akiwa na Miaka 40 na hakubahatika kufurahia maisha matamu ya Jumba Lao. Hapo ndo wadada hawa walipoanza kuvurugwa na maisha.
Walianza kufanya sherehe na kualika watu, kunywa pombe na starehe za usiku kucha, hiyo ikaleta kiburi baina yao na kuanza kutokuongea na Wakati Mwingine kugombana (matokeo hasi ya Pombe).
View attachment 1887159

Kama ilivyo Kawaida kwa mtu kuwa na fedha na akili haijatulia, basi harufu ya muwa yenye kiherehere umfanya mlaji kung’atwa na nyuki. Ndivyo hivyo kwenye jumba la madada hawa.
Kijana mmoja Mwenye Miaka 27 tu aitwaye Frederick Castlemaine.
View attachment 1887152

Dogo mmoja hivi mfaransa ambaye alimtongoza Dora ila mwishoni akafunga ndoa na Isabela Mwenye Miaka takribani arobaini. Kijana alikuwa anataka fedha hakuwa na mahaba wala nini! Mwaka 1897, akiwa anawasindika kwenye matembezi mashemeji zake pamoja na mke wake, Bwana Castlemaine alijiua, hivyo wadada hawa waliuchukua mwili wa Marehemu Castlemaine na kuupeleka ndani ya chum a kimoja ndani ya jumba lao, waliuweka kwenye jeneza la kioo kisha wakawa wakiiba nyimbo zake pendwa wakati wa uhai wake.
View attachment 1887153

Mamlaka ya mji kupitia idara ya afya iliingilia kati na kuwalazimisha kuuzika mwili wa Castlemaine. Kwa Miaka miwili iliyofuata, mke wa Marehemu, Bibiye Isabella alitembea zaidi ya maili tatu kwenda makaburini kila ifikapo usiku kukaa na kuimba. Mpaka siku moja alipokutana na Dogo mmoja anayeitwa Alonzo Swain, kijana mjanja Mwenye Miaka 24. Huyu bi mdada alikuwa anapenda Dogo Dogo tu.
View attachment 1887154

Upande wa Dada Mkubwa, Victoria alichukua Dogo mmoja Mwenye Miaka 19, wakati huo Victoria akiwa 50. Huyu alifukuzwa na wadogo zake nje ya jumba baada ya kumaliza mgawo wake kwa Dogo Janja. Alifariki mwaka 1902.
View attachment 1887158

Upande wa Isabella, alichukua Dogo mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Swain, Huyu Dogo alimkosanisha Isabella na Dada zake kisha Isabella aliondoka na kwenda nje ya mji, lakini mwaka 1914 Isabella alifariki baada ya Dogo kuchukua fedha alitoweka na kumuacha Isabella mwenyewe, na mwaka 1919 Sarah alifariki.

Mwaka 1926, wadada watatu waliobakia, Grace, Dora pamoja na Mary walisafiri kuelekea Hollywood, wakiwa na tumaini la kuuza hadithi yao ya maisha. Ila Safari yao iliingia doa baada ya Dora kufariki katika ajali ya gari.
View attachment 1887156

Upande wa Mary ambaye alikuwa ana ugonjwa wa akili, alitumia muda Mwingi akiwa amefungiwa chumbani kwake na alifariki mwaka 1939. Na Grace alifariki mwaka 1946 na jumba lao lilishika moto na kuungua lote mwaka 1938.
View attachment 1887157

Huo ndo mwisho wa historia fupi ya Sutherland’s Seven sisters, kuanzia kuishi maisha ya kifukara, kufanikiwa kimaisha mpaka kudondokea pua. Ingawa maneno ya wajuzi wanadai ni kuwa laana ya wazazi wao imewatafuna Kwani Bi Mkubwa aliwakataza kutokuchana nywele zao.

Asanteni kwa kufuatilia historia hii. Karibuni tena mpaka Wakati Mwingine tena.
Nipo
Kwa hiyo hao hawakuacha hata watoto kuendeleza kizazi chao??
 
Kumbukumbu zilizopo zinaonesha Naomi kuwa ndo aliolewa na Joseph Henry Bailey na kuzaa Watoto hawa: Harry Sutherland Bailey, Fletcher S Bailey pamoja na Isabelle Victoria Bailey
Hao wengine chali tu
 
Aisee. Kulikuwa na nn kwenye nywele had bi mkubwa kuwazuia kuzichana? Nahis hapa kuna siri

Ingawa yalikuwa ni mafuta yanayonuka balaa..... Labda bi Mkubwa aliweka mambo yetu yale @Mshana Jr Njoo utuchambulie hayo mafuta
 
Back
Top Bottom