Wafahamu Sutherland’s Seven sisters: Sehemu ya Kwanza 1

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,240
2,000
Habari ya uzima wanaJF, natumaini mko wazma sana. Kazi iendelee. Nimepokea jumbe nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiomba niweke bandiko kuhusu Sutherland’s Seven sisters, Kwani niliwagusia juu kwa juu katika moja ya mrejesho wa bandiko moja ndani ya jukwaa. Naomba msamaha kwa kuchelewa.
Karibuni sana!

Katikati ya Miaka ya 1800 kulitokea kundi la wadada saba kutoka kaunti ya Niagara, jimbo la New York ambao walitoa watu macho na vinywa wazi kwa nywele zao ndefu. Walitambulika kama The Sutherland sisters.

IMG_5840.jpg

Kundi lililokuwa na warembo kama Sarah, Victoria, Isabella, Grace, Naomi, Dora, pamoja na Mary. Mkubwa kuliko wote alikuwa ni Sarah na Mdogo ni Mary.

Walitoka kwenye familia ya kimasikini Kabsa, walikuwa ni wenye hali ya chini yenye kufuga mifugo kama Kuku, pamoja na Baba Mzinga. Mama wa warembo hawa ndo Mwenye kupewa sifa kwa kibarua cha kutengeneza mafuta ya asili ya nywele kwa ajili ya mabinti zake, mafuta ambayo yalikuwa yana harufu Kali sana, ajabu ni kuwa nywele zao zilikuwa kwa urefu usio Kawaida.

IMG_5847.jpg

Mama yao aliwapiga marufuku mabinti zake kuchana nywele zao wenyewe kwa sababu zitakatika ovyo ovyo.
Ulifika wakati Naomi pamoja na Dada zake walikuza nywele zao kufikia mita 11.3 Ingawa Bwana Mkubwa Burnam aliongeza chumvi kuwa nywele zao zilikuwa ni mita 15.

IMG_5841.jpg

Burnam ni maarufu kama umeangalia filamu ya “The Greatest Showman” ambapo alikusanya watu wenye sifa na vipaji vya ajabu na kuanzia misafara pamoja na maonyesho.

Wazo la mwanzo kabsa la wadada hawa ilikuwa ni kuwa wanamuziki na Mungu aliwajalia vipawa vya kuwa na sauti nzuri za kuimba. Watu walijaa kwenye matamasha yao sio kwa ajili ya kuwasikiliza wakiimba bali ni kushangaa nywele asilia zenye urefu wa Kipekee sana.

IMG_5842.jpg

Walitoa burudani ya muziki wakiwa jukwaani huku wakiwa wamevaa magauni ya rangi nyeupe, wakiimba, kuimba nyimbo za kwaya, na Wakati Mwingine husimulia hadithi, kisha mwisho hufungua vitambaa vichwani mwao na kuziachia nywele zao zianguke chini na kugusa sakafu.

IMG_5840.jpg

Ilivutia sana Kwani katika Miaka ya 1800 Mwanamke kuwa na nywele nyeupe tena ndefu ilikuwa ni fahari sana; baadhi ya watu walienda kuona mubashara nywele nyeupe za asili.

Mwaka 1882, Familia ya wadada ilianza kutumia zawadi ya kuwa na nywele nyeupe ndefu kuingiza sokoni mafuta ya nywele huku wakiyapatia mafuta yao jina la “hair fertilizer” kwa tafsiri ya isiyo rasmi ya Kiswahili ni mafuta ya kukuza nywele.

IMG_5837.jpg

Waliwaogopea watu kuwa hiyo ndo siri ya wao kuwa na nywele ndefu kiasi hicho ingawa Mama yao alikuwa amekwisha kufariki na hakuna aliyefahamu mchanganyiko wa vitu gani ulitengeza mafuta yaliyofanya nywele zao kuwa ndefu namna ile!

Ingawa watu walipigwa changa, familia hii iliingiza fedha zaidi ya dola elfu tisini kupitia soko Lao la mafuta ya nywele, pamoja na sabuni za kuoshea nywele ndani ya mwaka mmoja wa kwanza.

Sarah ndo alikuwa na nywele fupi kuliko wote, huku akiwa na nywele zenye urefu wa futi tatu, wakati wadada wote wakiwa na urefu wa jumla ya mita 11.3 za nywele.

IMG_5849.jpg

Victoria alikuwa na nywele zenye urefu wa futi saba, huku Naomi akipendelea kusuka nywele zake mfano wa Rasta ingawa zilikuwa ni futi nne. Mdogo wao wa mwisho, aitwae Mary alikuwa na matatizo ya kiakili, na baadhi ya watalaamu wa afya ya akili waliwalaumu wazazi kuwa nywele za Mary ambazo zilikuwa ni futi sita kuwa ndo chanzo.

IMG_5846.jpg

Baba yao, Bwana Fletcher Sutherland alijizolea umaarufu Mkubwa sana, Ingawa kazi kubwa ilikuwa inafanywa na mabinti zake. Kiukweli Baba yao aliwatengeza kuwa Wanawake matajiri kwa karne ya 19.

IMG_5844.jpg

Mwaka 1888 Bwana Fletcher Sutherland alifariki dunia, na kuwaacha mabinti zake wakiwa kwenye utajiri sana. Mwaka 1893 wadada hao walirejea nyumbani walikolelewa na kujenga jumba kubwa lenye vyumba kumi na nne ambapo waliishi pamoja. Ingawa ni wadada wawili tu ndo waliofanikiwa kuolewa.

IMG_5841.jpg

Naomba mnivumilie Kwani hatma ya maisha ya hawa wadada iko kwenye sehemu ya Pili. Shukrani sana kuchukua muda wako ili usome bandiko hili.

Cc: @Mshana Jr @Malcom_X @daVinci XV @Kigizo jr na wengine

PIA SOMA:
- Wafahamu Sutherland’s Seven sisters: Sehemu ya Pili 2
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom