Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 20,517
- 30,587
Ni jambo jema kwa mheshimiwa rais kutokumtua Juliana Shonza maana muda wote alikuwa anamuwaza Mbowe tu na kufungua wasanii badala ya kuwaza namna gani ya kuwahudumia watanzaniaBaada ya Rais Magufuli kuteua Baraza jipya la Mawaziri atakalofanya nalo kazi baada ya kuwa Rais katika muhula wa pili. Katika Baraza hilo jipya, Rais amewatema Mawaziri 7 na kuchagua wengine
Waliotemwa ni;
1. Aliyekuwa Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa
2. Aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
3. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla
4. Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi, Isaac Kamwelwe
5. Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Josephat Hasunga
6. Aliyekuwa Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu
Manaibu Waziri walioachwa kwenye Baraza Jipya la Mawaziri ni;
1. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza
2. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
3. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stellah Manyanya
4. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni
5. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
6. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
7. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atashanta Nditiye
8. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Sima
9. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa
10. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu
11. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji
12. Aliyekuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Sinkamba Kandege