Wafahamu Majaji wa Mahakama ya Juu zaidi Kenya

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
Wafahamu majaji wa Mahakama ya Juu zaidi Kenya

Iwapo Raila Odinga atawasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi, itasikilizwa na majaji wa Mahakama ya Juu zaidi

Zoezi la uchaguzi nchini Kenya lilikamilika baada ya raia kupata fursa ya kuchagua viongozi wao wa ngazi mbali mbali na matokeo kutangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Wafula Chebukati.

Kati ya wagombea wanne waliokuwa wanapigania kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta, Wafula Chebukati alimtangaza William Ruto kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo.

Hata hivyo, hali ilibadilika pale mpinzani mkuu Raila Odinga ambaye pia ni kinara wa Muungano wa Azimio la Umoja kutangaza kuwa hakubaliani na matokeo ya urais.

Wakati anazungumza, Raila Odinga alisema kwamba hakubaliani na matokeo hayo kwasababu mwenyekiti wa tume hiyo alikiuka katiba kabla ya kumtangaza mshindi.

Alisema kwamba makamishna wa tume hiyo hawakukubaliana kuhusu hesabu ya mwisho ya matokeo hayo yaliompatia ushindi William Ruto.

''Takwimu zilizotangazwa na Chebukati ni batili, kwa maoni yetu hakuna mshindi kisheria aliyetangazwa kihalali wala rais mteule''.

Na kauli hiyo, inaonesha kuwa moja ya machaguo aliyo nayo Raila Odinga katika kukabiliana na hilo, nikuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya urais katika Mahakama ya Juu Zaidi.

Ombi hilo litakapowasilishwa, litasikilizwa na jopo la majaji saba.

Majaji hao ni Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, William Ouko, Mohamed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u na Isaac Lenaola.

Lakini je, majaji hao ni kina nani?

Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome

Jaji Martha Koome ni wakili na mtetezi wa haki za kibinadamu.

Aliweka historia Mei 21, 2021 kwa kuwa jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo.

Bi Martha aliidhinishwa rasmi kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya mwaka 1986 na baada ya hapo akafungua kampuni yake ya uwakili ambayo aliisimamia hadi 2003.

Pia kuna wakati alihudumu kama mwanachama wa baraza la Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK).

Mnamo mwaka 2012, alipandishwa hadi Mahakama ya Rufaa na Septemba mwaka huo huo, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Kenya.

Hizo, miongoni mwa juhudi zake nyingine kwa ajili ya ustawi wa watoto, alipongezwa kama mshindi wa pili wa Tuzo za Umoja wa Mataifa nchini Kenya 2020.

Koome ni mtetezi anayesifika wa haki za binadamu, akizingatia zaidi haki za wanawake na watoto.

Zaidi ya hayo, Martha Koome ni mtaalam aliyebobea katika masuala ya sheria ya familia, eneo ambalo amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za

Zaidi ya hayo, Martha Koome ni mtaalam aliyebobea katika masuala ya sheria ya familia, eneo ambalo amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za mali katika ndoa, hasa kwa wanawake.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu

Naibu Jaji Mkuu anawajibika kwa Jaji Mkuu katika majukumu yake anayotekeleza.

Jaji Philomena Mwilu ndiye aliyeko katika nafasi hii akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 33 katika taaluma ya sheria.

Aliidhinishwa kama wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya mwaka wa 1984.

Alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kisheria kibinafsi katika mashirika mbalimbali ya mawakili jijini Nairobi kwa miaka saba ya kwanza kufuatia kuidhinishwa kwake.

Baada ya hapo alijitosa katika ulimwengu wa makampuni akifanya kazi kama Afisa Mkuu wa Sheria.

Mnamo Novemba 2012, kufuatia mchujo uliokuwa na ushindani mkali, Mwilu alipandishwa hadi katika Mahakama ya Rufaa ambako alihudumu kama Jaji wa Rufaa hadi kuteuliwa kwake kuwa Naibu Jaji Mkuu, akila Kiapo cha Ofisi tarehe 28 Oktoba 2016.

Tarehe 3 Mei 2017 alichaguliwa na majaji wenzake wa Mahakama ya Juu kuwawakilisha kama Kamishna katika Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Bi Mwilu pia amejihusisha na hatua za kuwa kielelezo kwa mtoto wa kike na amewashauri wasichana na wavulana wengi katika shule za mbalimbali nchini Kenya.

Pia alitunukiwa tuzo ya ‘Moran of the Golden Heart’ na Rais Uhuru Kenyatta mwaka wa 2017.

Jaji William Ouko

Jaji William Ouko amekuwa afisa wa mahakama wa kwanza kupanda kutoka cheo cha chini cha hakimu wa wilaya hadi mahakama ya Juu Zaidi nchini.

Alizaliwa tarehe 21 Novemba 1962, Jaji Ouko alijiunga na huduma ya mahakama mwaka 1987 kama Hakimu wa Wilaya II (Mtaalamu) akipanda hadi kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu mwaka wa 1989.

Baadaye mwaka wa 1997, alipandishwa cheo na kutumikia kama Msimamizi wa Mahakama wa kwanza.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka wa 2004, na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, mwaka wa 2012 na miaka sita baadaye, alichaguliwa kuwa rais wa mahakama iliyo katika nafasi ya pili kwa ngazi baada ya mahakama ya Juu Zaidi.

Pia aliwahi kuwa jaji wa Mahakama Kuu pamoja na Jaji Mohammed Ibrahim na Jaji Isaac Lenaola.

Jaji Mohammed Ibrahim
Jaji Ibrahim aliteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Juu Zaidi ya Kenya mnamo Juni 16, 2011.

Jaji huyo alikuwa wa kwanza kutoka miongoni mwa jamii ya Wasomali wa Kenya kuidhinishwa kuwa Wakili.

Jaji huyo amewekeza pakubwa kibinafsi na kitaaluma katika kupata haki za makundi ya wachache, hasa jamii ya Wasomali, nchini Kenya.

Mnamo 1994, alichaguliwa katika Baraza la Wanasheria wa Kenya kwa muda wa mwaka mmoja.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mnamo Mei 22, 2003, na alihudumu kwa mara ya kwanza katika Kitengo cha Kiraia cha Mahakama Kuu, Milimani, Nairobi kuanzia Juni hadi Julai 2003, alipohamishiwa Kitengo cha Biashara cha Mahakama Kuu ya Milimani.

Mnamo Julai 2009, alihamishwa hadi Mahakama Kuu ya Mombasa, ambako pia alihudumu kama Jaji Mkazi hadi alipopandishwa katika Mahakama ya Juu Zaidi ya Kenya.

Jaji (Dkt.) Smokin Wanjala

Bw. Smokin Wanjala amekuwa miongoni mwa majaji wa Mahakama ya Juu ya Kenya tangu 2011.

Kabla ya kuteuliwa katika Mahakama ya Juu ya Kenya, Jaji Wanjala aliwahi kuwa Mhadhiri wa Sheria na baadaye, Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa takriban miaka ishirini.

Alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Malalamiko ya Umma kuhusu Mazingira kuanzia 2002 hadi 2004.

Aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini (KACC) mnamo Oktoba 2004, ambapo alihudumu katika wadhifa huo hadi 2009.

Anajulikana kwa kusimamia utungaji na uandishi wa kile ambacho kimekuwa maarufu kwa jina la ‘Ripoti ya Ndungu’.

Ilikuwa ni ripoti juu ya ugawaji haramu wa ardhi ya umma.

Pia ana Tuzo ya Urais ya Burning Spear (CBS) ambayo aliopokea 2012.

Jaji Njoki Ndungu ni Jaji wa Mahakama ya Juu ya Kenya.

Pia ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Hapo awali alifanya kazi kama wakili wa serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Afisa Programu katika Taasisi ya Elimu ya Demokrasia, na Afisa wa Ulinzi wa Kitaifa katika Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi.

Pia amefanya kazi kama mchambuzi wa kisiasa katika kudhibiti migogoro katika Umoja wa Afrika.

Njoki Ndungu aliyeteuliwa kuwa mbunge Njoki Ndungu aliteuliwa katika Bunge la 9 na Muungano wa National Alliance Rainbow Coalition - NARC kuhudumu kama mbunge aliyependekezwa kati ya 2003-2007.

Katika Bunge la 9 Njoki Susanna Ndungu alihudumu katika Kamati za Bunge zifuatazo:

1. Kamati ya Idara ya Utawala wa Haki na Masuala ya Kisheria

2. Kamati ya Idara ya Ulinzi na Mambo ya Nje

3. Kamati Teule ya Katiba ya Kenya

4. Kamati ya Migogoro na Ushirikiano wa Kimataifa (PAP)

Njoki Ndungu pia alianzisha miswada kadhaa ya kibinafsi ikiwa ni pamoja na:

1. Mswada kuhusu Mafao ya Uzazi

2. Marekebisho ya Sheria ya Uzazi na Haki za Wazazi wa Kiume na Kike katika Ajira, 2007

3. Marekebisho muhimu ya haki za binadamu kwa Mswada wa Wakimbizi

4. Mswada wa Makosa ya Kijinsia, 2006

Njoki Ndungu pia alipata tuzo za

1. Mtu Bora wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya 2006

2. Tume ya Kimataifa ya Wanasheria - Tuzo la Mwanasheria Bora wa Mwaka 2006.

3. Tuzo kutoka kwa Rais ya kitengo cha the ‘Elder of the Burning Spear’ (EBS) katika mwaka huo huo wa 2006.

4. Jaji Njoki Susanna Ndung’u pia alitunukiwa tuzo la ‘Chief of the Burning Spear’ (CBS)

Jaji Isaac Lenaola

Jaji Isaac Lenaola ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Nairobi na Shule ya Sheria ya Kenya.

Pia aliwahi kuwa mwanachama wa Mahakama inayochunguza mienendo ya majaji wa ngazi ya chini.

Alijiunga na huduma ya mahakama mwaka wa 2003 na kufanya kazi kama Jaji Mkazi katika Mahakama Kuu za Embu, Meru, Machakos na Kakamega.

Jaji Lenaola pia alihudumu kama Kamishna katika Tume ya Huduma za Mahakama.

Hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu Zaidi, Jaji Lenaola alikuwa Jaji Msimamizi wa Kitengo cha Kikatiba na Haki za Kibinadamu katika Mahakama Kuu ya Milimani, Nairobi ambapo alitoa maamuzi yenye mwanga na ya msingi kuhusu haki za binadamu, ugatuzi, na mgawanyo wa mamlaka miongoni mwa maeneo mengine kisheria.

Katika vituo vyote alivyohudumu nje ya Nairobi, anasifika kwa uchapakazi, uadilifu na mara nyingi ametajwa kuwa mfano katika usimamizi bora wa kesi na kuondoa mrundiko wa kesi.

Jaji Lenaola amewahi kuwa Jaji na Naibu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Mwanzo mfano Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kuanzia 2011 hadi 2018 na kama Jaji katika Mahakama Maalum ya Sierra Leone (RSCL) kuanzia 2013 hadi sasa.

Pia ni mwanachama wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Jumuiya ya Madola, (CMJA), Jopo la Uwajibikaji la Tume ya Haki ya Wanyamapori (WJC) na pia Jukwaa la Majaji na Wanasheria wa Afrika (AJJF).

Alitunukiwa tuzo ya Chama cha Wanasheria cha Kenya kwa utumishi mzuri katika Utawala wa Haki (2008), tuzo ya uanachama wa heshima wa Jumuiya ya Wanasheria ya Afrika Mashariki kwa utumishi wa kupigiwa mfano na ukuzaji wa sheria nchini Kenya na Ukanda wa Afrika Mashariki (2015), vile vile na tuzo zinginezo.

Yeye pia nialipata tuzo ya Moran of the Burning Spear (MBS) kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa utumishi wa kupigiwa mfano katika usimamizi wa haki nchini Kenya na Kanda ya Afrika Mashariki.

Mnamo Julai 2022, alitunukiwa tuzo ya Chief of the Burning Spear (CBS).

Pia ametajwa kuwa Mwanasheria Bora wa Mwaka na Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ)
 
Jopo
FB_IMG_1660808133282.jpg
 
Kama Hawa ndio wanasimamia then Odinga atapindua matokeo. CJ Koome ni "bestie" ya Karua na huyo Mwilu Ali sympathize na Odinga 2017.

Let's wait and see
CJ na Karua wote ni wanasheria, mawakili, hakuna kitu kama urafiki kwenye taaluma hiyo.
Alafu maamuzi ya mwisho huwa ni 'by popular vote', kura. Ndio maana kwenye jopo hilo kuna majaji saba, odd no.
 
CJ na Karua wote ni wanasheria, mawakili, hakuna kitu kama urafiki kwenye taaluma hiyo.
Alafu maamuzi ya mwisho huwa ni 'by popular vote', kura. Ndio maana kwenye jopo hilo kuna majaji saba, odd no.
Hii ndio kete ya mwisho kwa Kenyatta kuzuia Ruto asiingie ikulu, believe me intimidation kwa majaji itakua kubwa mnoo whether kwa pesa au ransom ila hiyo 4/7 itapatikana tu kwa risasi au noti.

All in all I don't think Ruto is the right man for the job especially with Rigathi as his right hand man.
 
Kwamba ushahidi na vitu kama hivyo, havitazingatiwa kwenye maamuzi ya mwisho ya mahakama? Mhimili wa mahakama nchini Kenya upo huru na imara zaidi ya unavodhania.

Tena vitu havitafanywa kisirisiri, vikao vya jopo hili vitakuwa live kwenye Tv zote nchini Kenya. Vikifatiliwa hatua kwa hatua, hoja kwa hoja. Kumbuka kwamba kama kulikuwepo na dosari kwenye uchaguzi, kura ndio huwa zinahesabiwa upya au uchaguzi unarudiwa tena. Sio kwamba mmoja huwa anapokonywa ushindi/urais alafu eti unakabidhiwa mtu mwingine. Hizo kikatiba ndio huwa zinaitwa 'checks and balances'.
 
Kwamba ushahidi na vitu kama hivyo, havitazingatiea kwenye maamuzi ya mwisho ya mahakama? Mhimili wa mahakama nchini Kenya upo huru na imara zaidi ya unavodhania.

Tena vitu havitafanywa kisirisiri, vikao vya jopo hili vitakuwa live kwenye Tv zote nchini Kenya. Vikifatiliwa hatua kwa hatua, hoja kwa hoja. Kumbuka kwamba kama kulikuwepo na dosari kwenye uchaguzi, kura ndio huwa zinahesabiwa upya au uchaguzi unarudiwa tena. Sio kwamba mmoja huwa unapokonywa ushindi/urais alafu eti unakabidhiwa mtu mwingine. Hizo kikatiba ndio huwa zinaitwa 'checks and balances'.
Mkuu last time issue si ilikua verification of results mbona uchaguzi ulifutwa ilihali ilipaswa kuhesabiwa upya maana fomu za 34 A Bado zilikuwepo?

Mfano kama issue ya kufuta chaguzi Mombasa na Kakamega ikigundulika ni sabotage ya voter turn out maana ni ngome ya mgombea Fulani hauoni inaweza cancel uchaguzi badala ya recount!!

Kama uchaguzi ukirudiwa gap ya 170 ni ndogo so Mshindi anaweza kuwa yoyote tu sio kwamba Ruto alimzidi kura million 1 ambazo ingekua done and dusted matter!!!
 
Sawa jombaa, acha tungoje maamuzi ya mahakama.
 
Kama vile uhuru na raila walivyopigwa na kitu kizito kwenye BBI, na kwenye hili watatandikwa tena.
 
Mkuu last time issue si ilikua verification of results mbona uchaguzi ulifutwa ilihali ilipaswa kuhesabiwa upya maana fomu za 34 A Bado zilikuwepo?

Mfano kama issue ya kufuta chaguzi Mombasa na Kakamega ikigundulika ni sabotage ya voter turn out maana ni ngome ya mgombea Fulani hauoni inaweza cancel uchaguzi badala ya recount!!

Kama uchaguzi ukirudiwa gap ya 170 ni ndogo so Mshindi anaweza kuwa yoyote tu sio kwamba Ruto alimzidi kura million 1 ambazo ingekua done and dusted matter!!!
Muungano wa Kenya kwanza umezidi kuimarika na ule wa Azimio kuzidi kudhoofika baada ya vyama vilivyokuwa Azimio kujiunga na umoja kwanza, mtanange ukirudiwa raila atapigwa asubuhi sana, na watu wa mlima wamejiapiza uchaguzi ukirudiwa watajitokeza kwa wingi zaidi kupiga kura.
 
UnDhan mahakama za Kenya ni sawa na hapa këtu tz????
Hii ndio kete ya mwisho kwa Kenyatta kuzuia Ruto asiingie ikulu, believe me intimidation kwa majaji itakua kubwa mnoo whether kwa pesa au ransom ila hiyo 4/7 itapatikana tu kwa risasi au noti.

All in all I don't think Ruto is the right man for the job especially with Rigathi as his right hand man.
 
Muungano wa Kenya kwanza umezidi kuimarika na ule wa Azimio kuzidi kudhoofika baada ya vyama vilivyokuwa Azimio kujiunga na umoja kwanza, mtanange ukirudiwa raila atapigwa asubuhi sana, na watu wa mlima wamejiapiza uchaguzi ukirudiwa watajitokeza kwa wingi zaidi kupiga kura.
Wasomali hao hawana kura zaidi ya laki 3!! Then mkataba wa Azimio huruhusiwi kuachana na coalition hadi miezi mitatu baada ya uchaguzi so wakienda kisheria hata kina Mutua Bado ni Azimio la umoja.

Kingine uchaguzi ukirudiwa Wakikuyu ndio watakua wachache zaidi maana hawana Cha kupoteza yeyote akishinda sio kabila lake!! Ila wajaluo na waluhya watajitokeza mpaka waliopo hospitalini Ili kuokoa Urais wa Odinga na kama Kenyatta alikua dhaifu basi atatumia dola kweli kweli kuhakikisha ngome za Ruto wapiga kura hawajitokezi.

Anyway haya yote ni maoni tu, maamuzi ni ya mahakama
 
Kama Hawa ndio wanasimamia then Odinga atapindua matokeo. CJ Koome ni "bestie" ya Karua na huyo Mwilu Ali sympathize na Odinga 2017.

Let's wait and see
Ubesti nyoko.Kama ni hivyo hUyo Jaji mkuu hapatani na kenyata hivyo atamchinjilia mbal kenyata.nakuambia hiii kësi ruto anashinda 5-2.
Odinga anategemea back up ya wale makamishna kitu ambacho kiweledi hawawez kuaminiwa Kabsa. Kumbuka mawakili wa odinga watakuwa wanapambana vikal na mawakili wa tumë na Ruto Kwa wakati mmoja.

Pia hoja nyingne kila kituo azimio walikuwa na mawakala hizo kura zao ziliibwaje???
Kama ziliibwa bas wakuulizwa ni mawakala
 
Hii ndio kete ya mwisho kwa Kenyatta kuzuia Ruto asiingie ikulu, believe me intimidation kwa majaji itakua kubwa mnoo whether kwa pesa au ransom ila hiyo 4/7 itapatikana tu kwa risasi au noti.

All in all I don't think Ruto is the right man for the job especially with Rigathi as his right hand man.
Hivyo ndo watu walikua wanasema kuhusu IEBC kabla Ruto atangazwe kuwa mshindi...
Ikifika pale kwa supreme court hakuna mtu (ikiwemo rais) anauwezo wa ku influence majaji wengi wa supreme court... Kumbuka hawa hawa ndo walitupilia mbali BBI ambayo Rais alikua ywataka Katiba igeuzwe kutengenezwe cheo cha waziri mkuu alafu mkuu wa upinzani (leader of opposition) awe anapokea mshahara kisha anaruhusiwa kuongoza vitu flani bungeni...etc mahakama kuu ikatupilia mbali kesi hio ambayo ndo ilikua kama legacy ya mwisho rais Kenyatta alikua ywataka atuwache nayo...

Lakini Hata hivyo, Njoki Ndungu pekee ndo mimi hua nashuku ako compromised, kama ilivyosemekana hapo, ashawahi kua mbunge... Yani alishawahi kuacha taaluma yake na kujitosa kwa siasa wakati flani...
Hao majaji wengine washawahi kutoa judgement tofauti mara nyingi i.e mara nyengine huegemea upande wa serikali na mara nyengine huegemea upande wa wananchi, kwahivyo inadhihirisha wao hufwata katiba 90% of the time.. Lakini karibu kila judgement ya njoki ndungu huegemea upande wa serekali...
 
Ubesti nyoko.Kama ni hivyo hUyo Jaji mkuu hapatani na kenyata hivyo atamchinjilia mbal kenyata.nakuambia hiii kësi ruto anashinda 5-2.
Odinga anategemea back up ya wale makamishna kitu ambacho kiweledi hawawez kuaminiwa Kabsa. Kumbuka mawakili wa odinga watakuwa wanapambana vikal na mawakili wa tumë na Ruto Kwa wakati mmoja.

Pia hoja nyingne kila kituo azimio walikuwa na mawakala hizo kura zao ziliibwaje???
Kama ziliibwa bas wakuulizwa ni mawakala
Mkuu tusubiri mahakama itaamua, hata 2017 mlisema hakuna ushahidi wakaweka kina PLO Lumumba ila wakaangushwa na wanasheria wa NASA. So tusubiri hii ni last battle ya Uhuru Vs Ruto ndio itaprove kama Deep state is that deep ama ni story tu.
 
Back
Top Bottom