Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Sina shaka kabisa na dhamira ya Rais Magufuli ya kutaka nchi yetu ibadilike na ipate maendeleo na heshima Duniani. Ninaamini Rais Magufuli anataka kuacha footprints katika nchi hii ili hata wale watakaokuja siku za mbeleni watambue kuna Rais aliitwa Magufuli alitoa mchango wake mkubwa katika Taifa letu. Hayo ni matamanio na si lazima iwe hivyo. Rais Magufuli ili kufikia matamanio hayo ni lazima awe na mipango thabiti kuelekea kwenye matamanio yake. Ni lazima awe na majibu yasiyo na mashaka katika mambo yafuatayo:
1) Nguvu yetu ya ushindani wa kiuchumi iko wapi? Siku zote ukitaka kumshinda adui yako ni lazima utumie kile ambacho adui yako hana au atakipata kwa taabu
2) Maadui wako au vipingamizi vinavyoweza kukuzuia usifikie matarajio yako ni nini
3) Marafiki wanaoweza kukusaidia kuyafikia malengo yako ni nani
4) Nini agenda ya kitaifa
Naacha kuelezea kipengere cha 1 na 4, tujadili 2 na 3.
Kwa sasa adui mkubwa wa mafanikio ya Magufuli, anayeweza kufanya Magufuli asifanikiwe anachotaka kukifanya kwa Watanzania ni CCM. CCM ni adui namba 1 wa Magufuli kwa sababu ni adui anayetembea naye na yupo naye wakati wote.
Wakati Magufuli analiangalia Taifa, wana CCM wanaiangalia CCM na maslahi yake. Mafanikio ya Magufuli yatahitaji sana nguvu ya pamoja ya Watanzania wote bila ya kujali utofauti wa itikadi za vyama lakini tofauti hizo haziondoki kwa kauli bali kwa vitendo.
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Hivi unatarajia ni kwa muujiza gani wananchi wa Zanzibar, wapenzi na wanachama wa CUF wataweza kuunganisha nguvu zao na Rais huku wakiwa wameporwa ushindi wao wa wazi kwa nia tu ya kuhakikisha CCM inatawala daima? Kwenye hili, CCM wamefanya kosa kubwa sana ambalo litarudisha sana nyuma kufikia matarajio ya Rais Magufuli.
CCM nusura wafanye uchafu huo huo jijini Dar es Salaam lakini nampongeza Rais kwa kuwa aliona wazi kuwa hilo anaweza kulishinda, na akachukua hatua. Sasa namwomba awe na msimamo huo huo kuhakikisha kuwa viongozi wa serikali na madiwani kutoka vyama vyote wanafanya kazi pamoja kwa manufaa ya wananchi. Kama kuna kiongozi atafanya kazi kwaajili ya maslahi ya chama kwa gharama ya maendeleo ya wananchi, Rais akemee, aonye na atuambie wananchi maana kila diwani alichaguliwa kwaajili ya maslahi ya umma na siyo chama.
Nazungumza kwa uchungu mkubwa kuhusu zanzibar. Hivi mheshimiwa Rais, ana amani kabisa moyoni mwake kuona Watanzania zaidi ya milioni 45 wanakosa hela ya MCC, na huenda nyingine watakazotamka wabia wa maendeleo kwaajili ya kulinda tu maslahi ya Dr Shein na CCM? Sisi wengine tunaona hiyo ni dhuluma kubwa kwa umma wa Watanzania. Utawala wake unahitaji mchango wa kila namna, iwe ni msaada, mkopo, ukusanyaji wa kodi, ujenzi wa miradi mipya ya kiuchumi, n.k. ili tuweze kusimama na kukimbia. Tanzania kama Taifa tunahitaji kuwa na msimamo kwenye mambo ya msingi lakini siyo kwa mambo haya yaliyotokea Zanzibar ambayo kila mwenye akili anajua kuwa siyo sahihi.
Kwa bahati mbaya watanzania wengi ni wanafiki hasa wanapokuwa na mkubwa. Hawatamwambia ukweli ila sisi tulio nje tunamweleza ukweli. Mheshimiwa Magufuli hii nchi haijawa na nguvu na kusimama yenyewe bila ya mahusiano mazuri na jamii ya kimataifa. Kwenye hili la Zanzibar tumefanya kiburi cha kijinga, na wengi hatuungi mkono. Mataifa karibia yote Duniani yanapata misaada, yanakopa na yanavutia uwekezaji toka mataifa mengine. Ubaya wa kujitenga na jamii ya kimataifa wanaujua wananchi wa Zimbabwe, Korea Kaskazini, Iran na hata Urusi. Bado tunahitaji sana uwekezaji, misaada, mikopo na mashirikiano ya kiuchumi.
Ushauri wangu Rais Magufuli awasikilize sana walio nje ya CCM maana ndiyo wenye uwezo wa kumweleza ukweli katika kila eneo bila ya unafiki. Anatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana anapopewa ushauri na wana CCM na viongozi wao maana Magufuli anapofikiria Taifa kwanza, wenzake ni CCM kwanza.
Kipengere cha 4 ni kirefu na kinahitaji mjadala mpana. Kuna mambo amefanya Rais mpaka sasa ni mazuri na muhimu kwa Taifa letu lakini tunataka mambo hayo yaendelee na hayataendelea bila kuwemo kwenye katiba/sheria. Rais anahitaji nguvu ya wananchi wote na taasisi zote ili kutimiza ndoto zake lakini hilo halitatokea kama agenda ya kitaifa haifamiki kwa kila mwananchi. Agenda ya kitaifa haitakiwi Rais atembee nayo mfukoni bali ifahamike kwa wananchi wote. Ikifahamika kwa kila mtu, elimu yetu italenga mafanikio ya agenda, taasisi za utafiti zitalenga utekelezaji wa agenda, mahakama na sheria zetu zitalenga agenda ya kitaifa, vyombo vya dola navyo vitafanya kazi zaidi kwa kulenga utekelezaji wa agenda, mifumo ya uzalishaji italenga utekelezaji wa agenda ya Taifa, n.k. Mpaka sasa hilo halijaonekana