Wafadhiri wadondosha machozi baada ya kuona wanafunzi wanaketi chini

Umkondo wa Swize

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
282
89
MBUNGE wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga (CHADEMA) na maofisa wa Benki ya NMB Tawi la Kilombero, wamejikuta wakidondosha machozi baada ya kushuhudia wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye tope huku wakiendelea na masomo.

Tukio hilo lilitokea juzi katika shule za msingi Ntyangimbole na Kidete, zilizopo wilayani hapa wakati viongozi hao walipopeleka msaada wa madawati.Pia viongozi hao walilazimika kuchangishana fedha papo hapo kwa ajili ya kununua mbao mbili za kuandikia walimu darasani.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ntyangimbole, Emmanuel Njavike, kusema kuwa mbali na watoto kukaa kwenye tope, hakuna vifaa vya kufundishia kama mbao za kuandikia, meza na vitabu, hivyo kuwalazimu walimu kufundisha kwa uzoefu.

Katika risala ya Shule ya Msingi Nyangimbole iliyosomwa na Mwalimu Asunta Mbuja, mbele ya ujumbe huo uliotoa madawati 38 kwa kila shule, walimu hao walisema ukosefu wa madarasa imara umetokana na serikali kutelekeza nguvu kazi za wananchi waliojitokeza kujenga vyumba viwili vya madarasa.

Wakijibu madai hayo kwa nyakati tofauti, Mbunge Susan aliahidi kufikisha kilio hicho bungeni kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kulishawishi baraza la madiwani katika halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa upendeleo maalumu kuziwezesha shule za pembezoni kuwa na majengo imara ili wanafunzi wapate elimu bora.

Source: Wafadhili waangusha chozi wanafunzi kukaa chini
 
Mirahaba ya madini ni mitaji ya wakubwa, mikataba mbali mbali ni mitaji ya wakubwa, hayo ndiyo Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania tuliyo ahidiwa, KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
kazi ni kutukana tu bungeni wanaacha mambo ya msingi watoto wanabaki kukalia tope hovyoooooooooooo
 
Habari za kusikitisha kama hizi muwe mnaziongeza nguvu kwa kuweka picha.

Very good mkuu!!! Maana kitendo cha mtu mzima kutoa machozi si kitendo kidogo. Maana kama kuna picha tunajionea wenyewe ili kuondoa shaka ya propaganda maana watu tumezidi mno kuweka chumvi kwenye threads zetu.
 
Inakadiriwa kwamba ghalama ya kununua kamera na kumtuma Afisa wa usalama wa Taifa mmoja kwenda kufunga kamera kwenye kikao cha Chadema ni zaidi na madawati 80

Unaandika utumbo sasa.................
 
Kwani picha ngapi hadi leo zimewekwa? Bado tu unataka picha zaidi ili iweje?

Nyie waandishi wa habari MLIPANDA pilipili, na sasa ndiyo mavuno yake.

Unapotaka picha za kusikitisha, unanipa ile maana ya INSANITY (doing the same again and again and expecting different results.)

images
images
images

images
images
images

images
images
images

Habari za kusikitisha kama hizi muwe mnaziongeza nguvu kwa kuweka picha.
 
alietoa machozi mnafiki mzandiki,MBUNGE wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga (CHADEMA) na maofisa wa Benki ya NMB Tawi la Kilombero yeye unaona gari alipaki hapo? linaendana na hapo shule? ameliazima? wabunge wapuuzi sana
 
Kwani picha ngapi hadi leo zimewekwa? Bado tu unataka picha zaidi ili iweje?

Nyie waandishi wa habari MLIPANDA pilipili, na sasa ndiyo mavuno yake.

Unapotaka picha za kusikitisha, unanipa ile maana ya INSANITY (doing the same again and again and expecting different results.)

images
images
images

images
images
images

images
images
images

Hizi picha hazihusiani na mada. Ni za zamani sana na tulikwisha ziona......Tunahitaji picha ya "wafadhili" na mbunge wanalia kama mada inavyosema....!!!!!
 
Kwani tofauti itakuwa ipi? Unataka kuona wafadhili wanalia au unataka kuona watoto wamekaa chini?

Naomi%20lia.jpg
[h=2]Supermodel Naomi Campbell weeps[/h]From: Home

Hapo ilikuwa baada ya kuona hii hali:

article-0-0733CA59000005DC-875_468x686.jpg

Hizi picha hazihusiani na mada. Ni za zamani sana na tulikwisha ziona......Tunahitaji picha ya "wafadhili" na mbunge wanalia kama mada inavyosema....!!!!!
 
hao wafadhili wakizunguukia shule zote watarudi wamemaliza machozi yote maana ni hatari huko vijijini.
 
Sikuhizi miradi wanasimamia wenyewe

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hizi picha hazihusiani na mada. Ni za zamani sana na tulikwisha ziona......Tunahitaji picha ya "wafadhili" na mbunge wanalia kama mada inavyosema....!!!!!

Kwani hata hizo picha za Sikonge wewe binafsi haziwezi kukutoa machozi? 2013 hayo ndio mazingira ya kusomea? chini ya mbuyu? Mungu atulinde lakini hii serikali haiwezi kupata hata baraka za mungu kwa hali hiyo
 
Haya nyie CHADEMA hebu tuonesheni japo darasa moja tu la "shule ya kata" lililojengwa na ninyi ili tuone tofauti............
 
Kwani tofauti itakuwa ipi? Unataka kuona wafadhili wanalia au unataka kuona watoto wamekaa chini?

Naomi%20lia.jpg
Supermodel Naomi Campbell weeps

From: Home

Hapo ilikuwa baada ya kuona hii hali:

article-0-0733CA59000005DC-875_468x686.jpg

Wafadhili wenyewe hawalii ila huyo mbongo analia kisanii ili wafadhili waone huruma na watoe fungu kubwa ili liliwe na wajanja!!! Ndo CHADEMA wanachokisubiri wakiingia madarakani......Ni wizi kwa kwenda mbele!!!!!!!!!!!!
 
Tukisema nchi haina serikali wala watawala tunapigwa ban. Huyu kiwete na pinda wake wanafanya nini kama sii kuifilisi nchi na maliasili tu? Hivi hii mikataba ya kugawa madini yetu bure tutsikomesha lini? Hayo majeshi yetu ysmepoteza uzalendo kiasi vha kuiachia nchi iliwe na majangili ili hali tumefika hapa? Wajukuu zetu wataishije kama sisi tumefilisika kiasi hiki. Watanzania tuamke kumekucha.
 
Haya nyie CHADEMA hebu tuonesheni japo darasa moja tu la "shule ya kata" lililojengwa na ninyi ili tuone tofauti............
Hivi ndivyo nyie watu mnavyoiharibu Nchi hii, badala ya kusimamia kwa uadilifu mnachotakiwa kusimamia nyie mnafanya blunder then mnaona wabaya wenu Chadema. Mimi nazungumzia mazingira ya kujisomea ya chini ya mbuyu, wewe unahusisha uchama, vipi ww? Mi nasikitika nchi yangu wanafunzi kukaa chini 2013, badala ya kuona ni challenge na kama ww ndio Kawambwa uchukue hatua unaleta siasa za uvyama. Kifupi ni kwamba, rasilimali za nchi hii haziwezi kwa mara moja kufanya kila mtanzania kuwa tajiri, lakini inawezekana kufanya kila mtanzania apate elimu bora, tiba bora ya afya, chakula bora na makazi bora, ni ujinga tu unaofanywa na Serikali yako kuweka viapumbele Mashangingi na kuweka vipau nyuma elimu
 
Back
Top Bottom