Wafadhili warejesha msaada Uganda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
110512122549_jp_uganda512x288_nocredit.jpg

Wahisani wamesema wameridhika na kazi ya serikali mwaka 2012/13

Mapema mwaka huu wafadhili kadha walikata msaada wao wa bajeti kupinga sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja iliyopitishwa Februari.
Wiki jana serikali ilitoa andiko linalojaribu kubainisha sheria hio dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Mnao siku ya Jumanne, wafadhili hao walionyesha kuridhika na kazi ya serikali mnamo mwaka wa fedha 2012/13, baada ya uhakiki wa kila mwaka kuhusu matendo ya serikali.

Uhakiki huo unakusudiwa kuwapa fursa wafadhili kuamua ikiwa au la waendelee kugharimia bajeti ya Uganda kwa mamilioni ya dola.
Kwa jumla kasoro ya 20% ya bajeti ya Uganda inategemea misaada ya wafadhili.

Wafadhili hususan kutoka Ulaya ambao husaidia bejeti ya Uganda walisitisha msaada wao kufuatia ripoti za ufujaji wa pesa za serikali pamoja na kupitishwa kwa sheria ya kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.
Nchi hizo kiwawakilishwa na Denmark pamoja na beki ya dunia wanaonekana kushawishika kuendelea kusaidia Uganda baada ya kukutana na waziri mkuu Amama Mbabazi
140403190005_uganda_hiv_aids_512x288_getty_nocredit.jpg

Nyingi ya pesa inazopata Uganda kama msaada hutumiwa katika miradi ya afya

Katika taarifa yao ya pamoja, wahusika wote walitambua jukumu la Uganda katika kuweka amani na uthabiti katika kanda nzima na kuhimiza uhuru wa kujieleza pamoja na uwazi katika masala ya usimamizi wa pesa za msaada.

Wamejitolea kuendelea kufadhili Uganda kwa kima cha dola milioni arobaini katika siku zijazo.
Marekani pamoja na nchi nyinginezo kutoka Ulaya zilisitisha msaada wa mamilioni ya dola baada ya Rais Museveni kutia saini sheria ya mapenzi ya jinsia moja mapema mwezi huu.

Nchi hizo zinataka Uganda ifutilie mbali sheria hio kabla ya kuanza kuipa tena msaada.

Wiki jana waziri wa mambo ya nje wa Uganda alitoa taarifa kusema kuwa sheria hiyo ilitafsiriwa visivyo kwani lengo lake ni kuwalinda watoto bali sio kumbagua yeyote, wala haijulikani ikiwa tamko hilo ndilo lililoifanya wahisani kuanza tena kutoa msaada.

Chanzo; BBC
 
Back
Top Bottom