Wafadhili wameamuje kuhusu suala la misaada kwa tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafadhili wameamuje kuhusu suala la misaada kwa tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Dec 30, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika siku za karibuni, kulifanyika mkutano baina ya wafadhili na serikali ya Tanzania, kwa lengo la kutathmini hali ya utekelezaji wa mipango mbali mbali ya kuimarisha uchumi. Wakati wa mkutano huo, wafadhili hao walielezea kutoridhisha na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kupewa bajeti iliyo tofauti na ile iliyopitishwa na bunge. Kutokana na hayo wafadhili hao walihairisha kwa wiki mbili, kutangaza uamuzi wao, kuhusu kiwango cha misaada itakayotolewa kwa Tanzania katika mwaka ujao. Kwakuwa hizo wiki mbili tayari zilikwishapita, je hao wafadhili wamekwisha tangaza uamuzi wao au ndiyo tumekwenda na maji? /
   
Loading...