“Wafadhili wa Kimataifa = Mafisadi Wakubwa”:: Kuliko Mafisadi waliondani ya nchi ..

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,363
1,130
“Wafadhili wa Kimataifa wanaweza kuwa Mafisadi Wakubwa”:: Kuliko Mafisadi waliondani ya nchi kama kina Lowasa,Balali etc???

Ni nani Fisadi zaidi ya Mwingine? Mzazi anaye mpa mwanae kiasi kikubwa cha fedha ambazo atazitumia vibaya na hatimaye baadaye kumpelekea kuwa fisadi mkubwa asiyeweza kujitegemea? Ni nani fisadi zaidi ya mwingine Yule anaye Mkopesha mwenzie kiasi kikubwa cha fedha ambacho anajua fika atazichezea na kumpelekea kuwa fisadi na kuzichezea kifisadi tu!

Tuwaeleweje Wahisani na wafadhili wetu Wanojua fika kuwa Watanzania hatuna mapungufu ya kweli ya Kifedha kama tunavyolalamika; lakini wanaendelea kuzidi kutupa misaada na hatimaye tunashindwa kujitegemea.Wafadhili wetu wanaelewa Fika Kiasi kikubwa cha fedha tunachochezea kifisadi kama Kile cha BOT, ‘RICHMan’ etc lakini bado wanatupumbaza, wanaendela Kutupa misaada.

Nani Fisadi wa kweli: Yule anyekulemaza kwa ufisadi wa ndani kwa Kukupamba kwa miasaada ya kiini macho kama vile hakuna Ufisadi unaondelea nchini?

Rais amevunja baraza la Mawaziri lililojaa mafisadi. Rais hana cha kufanya kwa baraza la Wafadhili/Donors na wahisani wengine? Watanzani wazalendo wa kweli hawana cha kumshauri Rais na serekali kwa hili?

Furaha za Watanzania wanazozionyesha kwa kutikiswa kwa mafisadi wachache ndani ya taifa bila kutikiswa mafisadi wanaotulemaza kwa misaada ni kiini amcho? Ni furaha na shangwe za kitoto?

Wafadhili wa nje wakituonyesha umakini, uwajibikaji na Upendo wa kweli kwa Kutukatalia Misaada ya kijinga inayotupumbaza..Hii itatufanya kuwa makini na Fedha nyingi inayochezewa na wachache nchini?

Kama kweli tunataka kupigana na mafisadi, Tuhoja na ikibidi kukataa Baadhi ya Misaada toka mataifa mbalimbali?
 
Tuanze kwanza kuangalia boroti lililopo kwenye jicho letu kabla ya kuangalia la wengine. Mimi siamini kama tunaweza kutatuta tatizo la kuangalia hao wengine, hao wengine ukiangalia unaweza kuona kuwa rushwa zao ni za kimaendeleo, na za kwetu ni za kubomoa!
 
Ni kweli kabisa. Moja ya mikakati ya mifisadi wa kimataifa kama IMF na WB ni kukumwagia pesa na kuzipa nchi maskini ambazo ni corrupt kama Tanzania,vyanzo kemkem vya pesa ili viweze kuendesha serikali bila ya kutegemea mapato ya ndani ambayo kwa kiasi kikubwa ni pesa za wavuja jasho. Hii inafanyika kwa makusudi makubwa mawili: moja kuondoa uwajibikaji wa moja kwa moja wa serikali hizo kwa wananchi wake, kwani hata kama wananchi watalalamika, lakini Bw. Mkubwa akifurahi kule DC basi tutapata pesa za kutesea; Mbili kuzifanya serikali zetu kuwa vilema wa kutumia rasilimali zake kwa ajili ya uzalishaji na kuwa income ambayo inaweza kutupa kiburi cha kuwekeza kokote tunakotaka bila ya kuwauliza Mabwana wakubwa.
 
Azimio Jipya,

Hawa wafadhili toka nje sidhani kama tuwaite mafisadi kwani ndio kazi yao sawa sawa na mchezesha kamari. Haramu ni kamari yenyewe na hakuna anayekushika shati kuwa ni lazima ukaicheze.
Hawa jamaa kama hutawaita ama kuwataka msaada hawawezi kufanya kitu na masharti yao ni wazi kabisa ila sisi wenyewe ndio tunachagua kucheza kamari hiyo.
Nitakupa mfano mmoja wa chumabni labda tutaelewana vizuri hapa.
Ni sawa na mtu uliyeshindwa kumpa mimba mkeo ukaagiza mtu wa nje IMF aje ashughulike na mkeo kwa mategemeo ya kupata mtoto, sasa mimba isipotungwa kweli ni uungwana unamlalamikia yule uliyemwita kujaribu Kamasutra zake hali hakuna ushahidi wa DNA kuwa huyu jamaa ana mbegu hai na ushahidi wa matunda yake...
Kosa ni letu sisi wenyewe waagizaji sio la IMf wala sio la mke (kuitwa tasa) kama wanavyodai baadhi viongozi wetu mafisadi kuwa Tanzania maskini haiwezi shika mimba...

Now, mbaya na fisadi ni huyu ndugu yetu tunaye ishi naye nyumba moja kumbe mchezo wake ni kuzengea mke kila tunapompa mgongo!...Mafisadi wamo ndani Tanzania, ni mawaziri ambao JK mwenyewe kawa create kutokana na kile alichokuwa akia amini kuwa atayaendeleza ya Mkapa - UFISADI, nasi hatukutaka kuchunguza zaidi ya kuitazama sura yake na kuikubali kuwa ni kigezo tosha cha kutunga mimba - mtoto atakuwa handsome!..
 
Mkandara:

Nimeshukuru kwa jibu la KIKUBWA!!

Una mtoto mtukutu, umehisi anacheza kamari,umefanya uchunguzi na kamati imedhibitisha kuwa ni kweli kabisa mwanao anacheza kamari lakini anaporudi nyumbani ni mtakatifu kabisa..anaonekana safi, mwanao huyu ulimbatiza jina EL au "Richard wa Monduli". Kumbe anacheza kamari na Karamagi,Hosea,Masabaha, Mkapa, Balali, Yona etc na umegundua kuwa ninani Mfadhili wa kijiwe cha mchezo huo..WB, IMF na wenziewenye mapesa ya kutetemesha dunia.

Nilivyokuelewa ni kuwa mwanao EL na marafiki zake hao Ni kweli wana makosa ya kucheza kamari "UFISADI" lakini wamefanya kuufuwata mchezo huo kijiweni na huko kijiweni hela za kuchezea nyingingi zinatoka mfadhili WB, IMF nk.

Umegundua yote hayo ..na umefanya harakati na mikakati na umemwajibisha mwano Lowasa na baadhi ya marafiki zake kwa mujibu wa sheria za nchi...na bado unaendelea na safisha safisha..

Ninavyoonamimi..ulikuwa na mihimili miwili ya TATIZO. Mwanao Lowasa na Kundi lake, tuliite Mhimili wa kwanza Wa UFISADI..

Lakini muhimili wa PILI ni Wachezeshaji kamari. Nakuelewa umesema tusiwaite Mafisadi..lakini kundi la kwanza tunakubaliana tuwaite mafisadi. Sawa: Mimi nisema kuwa Wachezesha kamari ..Ni mafisadi wabaya zaidi ya Kina Lowasa na kundi zima la muhimili wa kwanza. Nikiwa na maana kuwa katika kupambana na tatizo la ufisadi ..haiatakuwa busara kuwaacha hawa wachezeshaji kamari!!

Watanzania wako kwenye shamrashamra na shangwe kwa Lowasa na wenzake wachache kuwajibishwa..Lakini Watu haohao wanoshangilia kwa mbwembwe nyingi bado wanacheza kamari, bado wacheza kamari wanakaribishwa na wanawapumbaza watanzania wanakuwa magoigoi akili zao zote ni kuwazia kwenda vijiweni kuomba kucheza kamari nakulipwa vijipesa vya kifisadi/kikamari na HAWAJITEGEMEI.Watanzania hawajiamini kabisa bila Kamari kijiweni..cha ajabu wanasherhekea kubwagwa kwa Lowasa na kundi lake!!
Sisawa tukapigana vita vya Ufisadi kwa kujaribu kuangamiza Mihimili yote miwili???
 
Ni kweli kabisa. Moja ya mikakati ya mifisadi wa kimataifa kama IMF na WB ni kukumwagia pesa na kuzipa nchi maskini ambazo ni corrupt kama Tanzania,vyanzo kemkem vya pesa ili viweze kuendesha serikali bila ya kutegemea mapato ya ndani ambayo kwa kiasi kikubwa ni pesa za wavuja jasho. Hii inafanyika kwa makusudi makubwa mawili: moja kuondoa uwajibikaji wa moja kwa moja wa serikali hizo kwa wananchi wake, kwani hata kama wananchi watalalamika, lakini Bw. Mkubwa akifurahi kule DC basi tutapata pesa za kutesea; Mbili kuzifanya serikali zetu kuwa vilema wa kutumia rasilimali zake kwa ajili ya uzalishaji na kuwa income ambayo inaweza kutupa kiburi cha kuwekeza kokote tunakotaka bila ya kuwauliza Mabwana wakubwa.

Mafuchila:

Nimekubalina na wewe kiasi kikubwa. labda niweke tatizo langu wazi kidogo. Kulingana na mtizamo wako wa msingi wa ufsisadi. Nataka Uone kinachoendelea nchini kwa sasa. Limetokea tuko la Lowasa na Mafisasi wenzie hapa....Ninsahanganzwa na Vigelegele na shangwe ..kule bungeni,anmagazetini, Tv na mitaa yote ya Tanzania! Ninapata picha kuwa watanzania wanafikiri kuwa Kwa Kuwaondoa hawa Mafisadi KAMA LOWASA Na tukaendelea kuwa Na mahusiano NA WAFADHILI kama ulivyoyaeleza kuwa Wana "makusudi makubwa mawili"""..WATANZANIA WANAFIKIRI WAMEUSHINDA UFISADI.NI KWELI? Hivi ni kweli tumeshafikia hata hatua moja ya kuanz akufurahia ushindi dhidi ya Mafsadi?
 
"Wafadhili wa Kimataifa wanaweza kuwa Mafisadi Wakubwa":: Kuliko Mafisadi waliondani ya nchi kama kina Lowasa,Balali etc???

Ni nani Fisadi zaidi ya Mwingine? Mzazi anaye mpa mwanae kiasi kikubwa cha fedha ambazo atazitumia vibaya na hatimaye baadaye kumpelekea kuwa fisadi mkubwa asiyeweza kujitegemea? Ni nani fisadi zaidi ya mwingine Yule anaye Mkopesha mwenzie kiasi kikubwa cha fedha ambacho anajua fika atazichezea na kumpelekea kuwa fisadi na kuzichezea kifisadi tu!

Tuwaeleweje Wahisani na wafadhili wetu Wanojua fika kuwa Watanzania hatuna mapungufu ya kweli ya Kifedha kama tunavyolalamika; lakini wanaendelea kuzidi kutupa misaada na hatimaye tunashindwa kujitegemea.Wafadhili wetu wanaelewa Fika Kiasi kikubwa cha fedha tunachochezea kifisadi kama Kile cha BOT, ‘RICHMan' etc lakini bado wanatupumbaza, wanaendela Kutupa misaada.

Nani Fisadi wa kweli: Yule anyekulemaza kwa ufisadi wa ndani kwa Kukupamba kwa miasaada ya kiini macho kama vile hakuna Ufisadi unaondelea nchini?

Rais amevunja baraza la Mawaziri lililojaa mafisadi. Rais hana cha kufanya kwa baraza la Wafadhili/Donors na wahisani wengine? Watanzani wazalendo wa kweli hawana cha kumshauri Rais na serekali kwa hili?

Furaha za Watanzania wanazozionyesha kwa kutikiswa kwa mafisadi wachache ndani ya taifa bila kutikiswa mafisadi wanaotulemaza kwa misaada ni kiini amcho? Ni furaha na shangwe za kitoto?

Wafadhili wa nje wakituonyesha umakini, uwajibikaji na Upendo wa kweli kwa Kutukatalia Misaada ya kijinga inayotupumbaza..Hii itatufanya kuwa makini na Fedha nyingi inayochezewa na wachache nchini?

Kama kweli tunataka kupigana na mafisadi, Tuhoja na ikibidi kukataa Baadhi ya Misaada toka mataifa mbalimbali?

Kwangu mimi dhana unayoielezea juu ya Ufisadi wa Wafdhili ni duni.

Ukishikwa shikamana.
Sisi tukishikwa tunataka anayetushika atubebe kabisa.
Sisi WaTZ tangu tujitawale ni watu wa kuomba misaada katika kila jambo. Hakuna jambo tuwezalo kufanya bila kusaidiwa hata kama tuna uwezo wa kulifanya jambo hilo.

TZ tuna matatizo makubwa ya Vision kama Watanzania na kama viongozi wa vyama vya kisiasa na serikali.
Mambo yote ya Ufisadi yaendeleayo sasa hivi ni matokeo ya sisi WaTZ na viongozi wetu kukosa Vision,kila mtu anataka kuwa fedha kibao mfukoni ili aingie kwenye kudni la watu walio endelea.
Kama unatembea kwa juhudi zote na hujui uendako lakini bado unakendelea kuchanja mbuga ni wazi kwamba miguu yako na siyo akili yako ndiyo itaamua wapi uelekee. Sisi waTZ ni kama mtu anaye tembea bila kujua wapi hasa anapaswa kwenda.

Tatizo la kutegemea misaada ni tatizo ambalo chanzo chake kikubwa kimo ndani ya familia zetu WaTZ.
Kwa mfano,Mzazi humsomesha mtoto wake kwa juhudi zote, mtoto akihitimu na kupata kazi mzazi anageuka kuwa omba omba na kuacha kuendeleza juhudi zake za kujitafutia liziki.
Siyo hivyo Mzazi mara kadhaa hufikia hatua ya kumlundikia kijana wake wadogo zake wote kwamba awasaidie kwa sababu yeye ni mzee sasa.
Cha ajabu mzee huyo huendelea kuzaa na wanawake wengine kila kona na kufanya mambo mengi ya aibu.
Kinachoendelea hapo ni tabia chafu ya kujenga tabia ya kutegemea kwamba mtu fulani mahali fulani ni lazima akusaidie kwa sababu wewe zamani uliteseka kwa sababu yake.
Tunalilia na kudeka mbele za wafadili kwa sababu tunadhani zamani babu zetu waliteseka sana kiuchumi na kijamii kwa sababu yao.

Sisi watanzania tunapenda makuu katika kila jambo.
Wakati wa kuoa tunafanya sherehe kubwa kuzidi uwezo wetu, nani analipia gharama za harusi? Wafadhili.
Sherehe za Ubatizo kipa imara na Birthday zinatia kinyaa.
Watu tunafanya sherehe hizo kana kwamba kiama kinakuja leo jioni, kwa nini tusisherhekee kwa kiasi? Kuna wafadhili watalipa gharama.
Hata wenyewe wa dunia ya kwanza wanao abudu sana sherehe za Birthday huzifanya kwa mahesabu ya fedha zao za mfukoni.
Kwa nini Watanzania wanatumia fedha nyingi kugharamia upuuzi, jibu ni kwamba tunaamini kwa dhati kwamba katika kila jambo ni lazima tufadhiliwe.

Watanzania tuna tabia nyingine mbaya sana ya kuiweka fedha kwenye mafungu ya ujinga ujinga, na kuishi kwa kufuata mipaka ya mafungu hayo ya fedha.
"Napata fedha ya kula tu."
"Hii ni fedha ya bia tu."
"Yule demu nimemtengea fedha lazima aingie laini."
"Hii nifedha ya matanuzi."
"Natafuta fedha ya nguvu ya kujengea nyumba sijapata."

Kuna watu wanatengeneza Tshs 10,000 a day na kudai hiyo nifedha ya kula unadhani ukitengeneza 15,000 elfu 5 ya juu utaiita fedha ya kuweka savings?

Unatengeneza fedha na kuiita fedha ya bia kwa nini sisikii mtu akisema leo nimetengeneza alfu 5 ya savings tu?
Hatusemi hivyo kwa sababu mawazo yetu ni kwamba kuna fedha kutoka mahali fulani kwa watu fulani tusio wajua inatakiwa kuja ili tuitenge kwa ajili ya maendeleo yetu leo na kesho.

Kama kuna kundi la wazee wetu walikaa kitako na kuanzisha mapambano ya kumfukuza mkoloni Tanzania na sisi leo hii miaka 48 baada ya uhuru tunawalaumu wafadhili kwamba ni mafisadi zaidi ya akina Lowassa na team yake, ni wazi kwamba hatujui tunasema nini na tumeshindwa kuendeleza nguvu iliyoanzishwa na wazee wale kupambana na ukoloni.

Sababu zilizo wafanya wazungu waje kututawala kwa urahisi miaka ya 1800 mpaka leo bado zipo pale pale.
Wazo la kumfukuza mkoloni katika himaya yetu ni wazo la kudumu kinacho badilika ni mbinu za kuendelea kupambana na masalia ya ukoloni wa ndani.

Wakoloni wa nje walipo fukuzwa tulianza kuwaenzi na kuwatukuza wakoloni wa ndani wenye sura na rangi kama zetu.
Wakoloni wa ndani wameweza kuteka vyama vyetu na ofisi nyingi za serikali na kutawala kana kwaamba wana nchi nyingine hapa duniani kuliko Tanzania.

Wakoloni wa nje wameweza kurudi leo kwa nguvu zote kwa sababu ya kupewa ushirikiano na wakoloni wa ndani, wenye nguvu nyingi mno za ajabu.

Mikataba ya madini na ya kufua umeme imeandikwa na Wa TZ wenye elimu ya kutosha na mawazo ya kikoloni. Kifupi uchuro wote wa kuandika mikataba ya kilevi umefanywa na wakoloni weusi ambao ni ndugu zetu wa damu lakini wenye mawazo ya kunyonya, kuharibu na hatimaye kuua juhudi zote za kujitawala kiuchumi.

Wakoloni wa nje wanatumia udhaifu wetu wa kukumbatia wakoloni weusi wa ndani kujisimika upya katika vyanzo vyote vya mapato ya uchumi wetu.

Wakoloni wa nje si tatizo hata kidogo tatizo ni wakoloni wa ndani wanaotumia Polisi Mahakama Usalama wa Taifa na hata uwezo wao wa kuua hadharani bila kuchukuliwa hatua, kulinda na kudumisha Uharamia wao, uongo wao, Uzinzi wao na zaidi wizi wa Kimafia wa fedha za Waatanzania.

Wafadhili wa nje wengi wao wanatoa fedha kwa nia njema, nia yao njema pekee haisadii kama sisi wapokeaji tumejaa mawazo yenye nia ya kujinufaisha katika ubinafsi wetu.

Ukiiba fedha za wafadhili zilizo kusudia kujengea madaraja 10 ukajenga hotel 10 za kisasa ukaajiri watu 2000. Sidhani kwamba walengwa wa madaraja hayo watachukua Baiskeli,magari na mikokoteni yao iliyo jaa bidhaa na kuzipishajuu ya mapaa ya hoteli zako na kujenga uchumi wa nchi.
Katika ujenzi wako huo wa mahoteli kama vifaa vingi vya ujenzi umevitoa kutoka kwa nchi wafadhili,wafadhili hao hawatasita kuchukuamshiko wako. Lengo kuu la wafadhili ni kutufadhili tupate maendeleo ili hatimaye wao nao wapate kufaidika.
Kwa mfano Huwezi kwenda kuchimba dhahabu mpanda kama barabra za mpanda hazina madaraja ya kuaminika na viwanja vya ndege vya uhakika.Mfadhili atagharimia ujenzi wa madaraja na hata viwanja vya ndege ili aje kusimika mmirija yake.

Kundi lolote la watu dhaifu duniani hutafuta mtu au kundi jingine la kubebesha lawama za kushindwa kwao.Hii ni tabia halisi ya kundi la watu wasio na malengo ya uhakika katika maisha yao.

Sisi watanzania hatuko tayari kusema ukweli kwamba, wengi wetu kama siyo wote tumejaa mawazo ya wizi kwa mfano wa wizi alio ufanya MH Former PM Lowassa.
Tunaiba kwa sababu tunadhani kuna kundi la watu waitwao wafadhili ambao kazi yao kubwa ni kujazia pengo tulilo liacha kwa wizi.

Ndiyo maana Rais Kikwete aliweza simama wima kwa miguu yote miwili na kuwaambia nchi wafadhili kwamba Fedha tulizo iba ni zetu wenyewe siyo zao wafadhili kana kwamba sentensi hiyo inamjenga kisiasa.
Rais naye anaishi kwa kuipa fedha majina na mafungu.
Fedha ya wafadhiri,fedha ya wavuja jasho, fedha ya kusafiria na kutibiwa nje nk.
Asijue kwamba fedha ya makusanyo ya kodi ikiibiwa ndivyo wewe Rais utakavyo zidi kuomba toka kwa wafadhiri.

Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, sasa sijui watu wenye vipara vikubwa kama Prf Sarungi na Mungai wana akiliz zote?

Wafadili wa kimataifa hawana uwezo wa kufanya ufisadi Tanzania bila sisi Watanzania wenyewe kuwaruhusu kwa moyo mmoja kufanya hivyo.

Zidumu fikra sahihi ndani ya JF.
 
Kwanza:.... Wafadhili wa nje wanatoa fedha wengi kwa nia njema, nia njema pekee haisadii kama sisi wapokeaji tumejaa mawazo yenye nia ya kujinufaisha katika ubinafsi wetu.

Pili:.....Sisi watanzania hatuko tayari kusema ukweli kwamba, wengi wetu kama siyo wote tumejaa mawazo ya wizi kwa mfano wa wizi alio ufanya MH Former PM Lowassa.Tunaiba kwa sababu tunadhani kuna kundi la watu waitwao wafadhili ambao kazi yao ni kujazia pengo tulilo liacha kwa wizi.

Tatu:......Wafadili wa kimataifa hawana uwezo wa kufanya ufisadi Tanzania bila sisi Watanzania wenyewe kuwaruhusu kwa moyo mmoja kufanya hivyo.

Nimevutiwa zaidi na vipengele vitatu!

Kwanza: Nia njema yao tunaiharibu sisi wenyewe, nakubalina kabisa kuwa hapa tatizo ni la kwetu. Nilifikiri wangetakiwa wawe na nia njema iliyozidi hiyo kwa Vipi? Waone upuzi wetu na hivyo wasiiedelee kuwapa wapuuzi misaada. Swali kwani nini uwepe wapuuzi na wabinafsi Misaada huku ukijua fika ni wabinafsi, waharibifu nk? Kama sio kuwa unataka kuwakamua kifisadi? Nia njema ya kweli an kubwa kuliko hiyo unayosema ingekuwa ni kuwakatia na kuwanyima miasaada;Kwangu hiyo ndio nia njeama na sio kuendelea kutupumbaza kwa faida yao!!

Pili: Tunaiba na kutawanya hivyo maana wafadhilili watatupa zaidi na zaidi..The same argument kama wafadhili wanajua tunafikra za kijinga namnahiyo na wanania njema sana na sisi..wangetunyima misaada tu maana tunafikra za kijinga..kama wao sio mafisadi wanatupa miasaada ya nini ..kama sio kutonyonaya ndani ya ujinga wetu? Ili nisiwaite mafisadi watunyime Misaada.Kwani wakitunyima Nini kitatokea? Tuzidi kuwa wajinga au Kuna uwezekano wa kumaka. Na kama kuna uwezekano wa kuamaka na wao wanajua..Ni dhahiri hawataki tuamke ndio maana hawataupuka kuitwa mafisadi kamili.

Tatu: Hawawezi kufanya ufisadi wa kimataifa bila sisi kuwaruhusu. That is right na hata wao wanjua hivyo. Kama wanajua kuwa sisi ni majuha na bado wanatumia ujuha wetu kututumia kutekeleza ufisadi wao ..mimi nachagua kuita kitendo hicho ufisadi. Naningependa watanzania wajue wanaonekana hivyo,wanafaa kutumika, haweheshimiki, wanachezewa na hivyo waamke kwenye unyonge huo!!Lakini hao wanajua udhaifu wetu na kuutumia huku wakisema wana nia njema na sisi..Sioni kwanini waisitwe mafisadi.

Kama Tunajeuri ya kupingana na Ufisadi Ni rahisi tu! Tuungane nchi nzima tuwaeleze waelewe kuwa tunawaita Mafisadi. Unajua kwanini tunaogopa sisi na viongozi wetu kuona kama ninavyoonyesha na kwanini hakuna wa kufungua mdomo, Hata rais na kuwaeleza ukweli? Sisi ni wanyoge Tumeganda fikra na maono,hatuwezi kuishi bila kuuedekeza ufisadi wao. tunajifanya sio ufisadi, tunarembesha sauti na sentensi tusije kuharibu mahusiano haya ya kifisadi.. Wamefanikiwa kutufanya SOKO!!
 
Misaada ya kimataifa hailengi kutunufaisha

Na Thomas William​

MISAADA kutoka nchi zilizoendelea haiwezi kuwa mwarobaini wa umasikini na kusuasua kwa maendeleo ya nchi zinazoendelea hususan barani Afrika.

Hakika katika zama hii ya utandawazi, soko huria na mwenye nacho ndiye mwenye nguvu kila nchi inajitahidi kufanya kila iwezalo kujinufaisha na kupata maendeleo.

Hivyo hata kama nchi moja inatoa misaada kwa nchi nyingine, kwa namna nyingine huwa ni uwekezaji ili ije kunufaika baadaye katika nchi iliyopewa msaada.

Jambo hili lipo wazi kwa sababu asasi za kimataifa za fedha na nchi zilizoendelea zinapotoa misaada au mikopo huja na masharti kadhaa.

Ili nchi inayopewa misaada au mkopo iendelee kupatiwa hulazimika kufuata masharti hayo vinginevyo mifereji huzibwa. Kwa mantiki hiyo, wafadhili hao si wa kweli.

Mfadhili na mhisani mkubwa ni Mungu pekee kwa kuwa ndiye mfadhili asiyekuwa na masharti waliobaki hufadhili kwa malengo wayajuayo. Mungu ameipendelea Tanzania kwa sababu kuna rasilimali nyingi kama vile madini, maziwa, bahari, misitu, wanyama, vivutio vingi vya watalii na ardhi nzuri yenye rutuba inayoweza kutumiwa kuzalisha mazao mbalimbali.

Watanzania kwa kupendwa na Mungu amewapatia akili na utashi ili kutambua mema na mabaya.

Kwa akili walizonazo, walitambua kwamba wakoloni ni wabaya na kuwafukuza. Wakoloni hawa hawa waliowafukuzwa leo hii wamegeuka wapendwa wanaleta misaada, haijulikani ni kwa jema gani.

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwa vile alikuwa anaona mbali, alitambua mapema kwamba mfadhili pekee ni Mungu, ndiyo maana alisema fedha si msingi wa maendeleo.

Kutokana na msimamo wake hakuwa tayari wakoloni kurudi kwa njia ya misaada ya fedha. Alibaini kwamba maendeleo yanaletwa na watu na fedha ni matokeo ya maendeleo.

Kinyume cha ulivyokuwa mtazamo na msimamo wa Mwalimu Nyerere hivi sasa fedha inachukuliwa kama msingi wa maendeleo hivyo ni vigumu kuponyoka kwenye mikono ya ukoloni mamboleo kwa kuwa wanarejea kwa njia ya misaada.

Nchi zilioendelea zinatoa misaada ili kuzifunika macho nchi zinazoendelea ili kampuni zao ziendelee kunyonya.

Zinatoa misaada ili kampuni zao ziendelee kuchimba madini, wapate mahali pa kuuza bidhaa zao na kupunguza tatizo la ajira katika nchi zao kwani kampuni za kigeni zinapokuja huja na wafanyakazi kwa kisingizio kwamba hakuna wataalamu wenye sifa.

Miongo kadhaa imepita tangu wafadhili walipoanza kutoa michango yao katika mikakati ya kupambana na umasikini na kuleta maendeleo lakini maendeleo yameendelea kudumaa na umasikini kuzidi kuongezeka.

Nchi imegeuka dampo la magari na vifaa vingine vinavyotumia umeme vichakavu huku rasirimali nyeti zikiendelea kusombwa kwenda kwa nchi tajiri na yakiachwa mahandaki na vifusi vinavyosababisha magonjwa ya vifua.

Wafanyakazi wanaokuja na wanaoitwa wawekezaji ambao awali Baba wa Taifa aliwaita wanyonyaji, kupe au mabepari wanapewa mishahara minono wakati wazawa wakilipwa kiduchu hata kama wana sifa zinazofanana na
pengine kuwazidi.
source:http://www.newhabari.com/mtanzaniajumapili/habari.php?id=69&section=ushairi

Pamoja na makala hiyo,niafikiane na mtizamo huu:

Kwanza: Nia njema yao tunaiharibu sisi wenyewe, nakubalina kabisa kuwa hapa tatizo ni la kwetu. Nilifikiri wangetakiwa wawe na nia njema iliyozidi hiyo kwa Vipi? Waone upuzi wetu na hivyo wasiiedelee kuwapa wapuuzi misaada. Swali kwani nini uwepe wapuuzi na wabinafsi Misaada huku ukijua fika ni wabinafsi, waharibifu nk? Kama sio kuwa unataka kuwakamua kifisadi? Nia njema ya kweli an kubwa kuliko hiyo unayosema ingekuwa ni kuwakatia na kuwanyima miasaada;Kwangu hiyo ndio nia njeama na sio kuendelea kutupumbaza kwa faida yao!!

Pili: Tunaiba na kutawanya hivyo maana wafadhilili watatupa zaidi na zaidi..The same argument kama wafadhili wanajua tunafikra za kijinga namnahiyo na wanania njema sana na sisi..wangetunyima misaada tu maana tunafikra za kijinga..kama wao sio mafisadi wanatupa miasaada ya nini ..kama sio kutonyonaya ndani ya ujinga wetu? Ili nisiwaite mafisadi watunyime Misaada.Kwani wakitunyima Nini kitatokea? Tuzidi kuwa wajinga au Kuna uwezekano wa kuamaka. Na kama kuna uwezekano wa kuamaka na wao wanajua..Ni dhahiri hawataki tuamke ndio maana hawataupuka kuitwa mafisadi kamili.

Tatu: Hawawezi kufanya ufisadi wa kimataifa bila sisi kuwaruhusu. That is right na hata wao wanjua hivyo. Kama wanajua kuwa sisi ni majuha na bado wanatumia ujuha wetu kututumia kutekeleza ufisadi wao ..mimi nachagua kuita kitendo hicho ufisadi. Naningependa watanzania wajue wanaonekana hivyo,wanafaa kutumika, haweheshimiki, wanachezewa na hivyo waamke kwenye unyonge huo!!Lakini hao wanajua udhaifu wetu na kuutumia huku wakisema wana nia njema na sisi..Sioni kwanini waisitwe mafisadi.

Kama Tunajeuri ya kupingana na Ufisadi Ni rahisi tu! Tuungane nchi nzima tuwaeleze waelewe kuwa tunawaita Mafisadi. Unajua kwanini tunaogopa sisi na viongozi wetu kuona kama ninavyoonyesha na kwanini hakuna wa kufungua mdomo, Hata rais na kuwaeleza ukweli? Sisi ni wanyoge Tumeganda fikra na maono,hatuwezi kuishi bila kuuedekeza ufisadi wao. tunajifanya sio ufisadi, tunarembesha sauti na sentensi tusije kuharibu mahusiano haya ya kifisadi.. Wamefanikiwa kutufanya SOKO!!
 
JC.

Nimeona jambo hapo. I dont know how long litaonekana kwa watanzania na kuanza kuchapa kazi wka jasho na maarifa yao binafsi!!
 
mimi nina shaka pia rais wetu nae ni fisadi.yote hayo ya richmond,bot nk anayajua vizuri na yeye ni mshirika.lkn bwana wadanganyika wanaendelea kufanyiwa usanii na tunampa sifa kibao jk.yaani kashindwa kabisa kuwalaani mafisadi!!! tumekwisha.km serikali yake imeoza kiasi hicho na yeye pia kaoza.hivi kweli watu kujiuzulu,kupatiwa mp mpya na baraza jipya la mawaziri ndio
kutamsaidia vp mlalahoi!! tungesikia bei ya umeme imeshuka,na mafisadi wamefilisiwa.ngojeni kwanza nilie kwa uchungu.
 
Azimio Jipya,
Mfano wako mkali sana na kusema kweli ni lazima nikubali maneno yako mia kwa mia....Haikuwa rahisi hadi nilipopima uzito wa hoja nzima hasa baada ya kuelewa kwamba mtoto wangu asingeweza cheza kamari kama hakuna wafadhili wanaojenga sehemu hizi za anasa na zenye mvuto mkubwa. Kweli pamoja na kuwa kamari ni haramu kwa waislaam hapa nyumbani lakini waislaam kibao wanajimwaga mchana kweupeee! hivyo basi hata dhana ya itikadi ktk imani ya dini na misahafu yote kulaani kitendo hicho bado watu hawaelewi....
Ndio kusema kwamba, Uharamu tu peke yake hautoshi isipokuwa kukata kabisa mizizi ya mchezo huu wa Kamari. Kutoruhusu ama kukubali kupokea wafadhili ambao tunafahamu wazi kuwa wanayotaka kuyaleta ni haramu...Swala la kusema sisi sii wote waislaam nadhani linaweza pingana na ukweli kuwa sisi wote ni Watanzania na bila kujali dini tukumbuke tu kuwa athari za Kamari hiyo haitamchagua muislaam pekee kwa maana hiyo Ufisadi hauwezi kubakia kwa kina Lowassa na Mramba na wengineo ila utasambaa hadi kwetu waumini wa kweli.

Shukran sana mkuu umenipa somo safi na mnakubaliana na wewe kuwa pamoja na kuwa mikopo yenye riba ni haramu, muhimu tukiwatazama wafadhili wa mikopo hii kama Mafisadi wakubwa kuliko neno lenyewe..
Hata Yesu na mitume wote walitumwa kuja ku deal na watu wenye kukumbatia mabaya na sio kueneza imani peke yake..Na mdio maana walitupwa katikati ya Mafisadi badala ya kuletwa kwetu Africa kulikojaa Amani na Utulivu (Ujinga). From there kwa hao Mafisadi dini ( yaani neno la Mungu) limeweza kuelea haraka zaidi na leo hii kuna zaidi ya waumini billioni nzima.
Big it up!
 
aiseeh kwa mwendo huu hatutafika popote,yaani leo matatizo yetu ya rushwa na uzembe tunawasingizia wafadhiri,hamko serious nafikiri na mnaongea conspiracy tuu,hiyo mikopo ya WB na IMF ni kama kupewa bure tuu maana interest sometimes ni 1-2%...inasikitisha sana wengi wanavyofikiria na badala ya kuangalia tatizo la kweli tumebaki kusingizia hata wasiokuwemo!
 
Koba:

Haya hapa maneno yako!
"..yaani leo matatizo yetu ya rushwa na uzembe tunawasingizia wafadhiri..."

Kama wewe unamfadhili mwanao kwa miaka nenda rudi..na huku unajua fika kuwa anateketeza na kufuja ufadhili wako kwa uzembe uliokithiri...na mtoa rusha ..Na bado kwa makusudi kabisa unatoa nguvu kubwa kabisa kumtetea...!! Watu wenye fikra timamu wakueleweje? Lazima wajiulize una nia gani? Unafaidi nini kuendelea kuufadhili uzembe, rushwa na uharibifu wa mwanao? Tunahakika wewe sio chizi, tutakuchuguza kuwa kwa nini umharibu mwanao? au kupitia upuuzi na ufinyu wa mwanao unapata nini?? Kwanini uendelee kumfadhili wakati umegundua fika mapungufu dhidi yake kwa uachomfadhili? Kama huwezi kujibu mswali hayo..Utatuziaje kukuita Fisadi?

Unajua kabisa Fedha unazompa mwanao anazifanyia uzembe kama wa BOT...anazitumia kwenye rushwa kama za Richmond, hanamaendeleo, nimbinafsi.etc.. Tunashangazwa na nyedo zako wewe mtu usiye na matatizo ya kiakili kwa nini usimpe msaada stahili?

UPI?

Ondoa ufadhili wako. STOP!!!!!

Hiyo ndio hatua ya kwanza ya upendo na msaada wa kweli! Huo ndio ufadhili wa kweli kwa mwanao Hatua hiyo itamfanya sifubae na kuwa zezeta wa kizembe na kutoa rushwa. Hilo halitamfanya abadilike? There is a possibility he will work up!! Na hatimaye atakufadhili wewe mzazi muda sio mrefu..maana hata yeye ana utu, heshima na maadili yote ya kibinaadamu ya kuchapa kazi na kujitegemea, uliyokuwa unayaua kwa faida ulizokuwa unazipata.

Ujumbe?

Kiukweli kabisa Tanzania haina qualification hata moja ya kupewa ufadhili na Mfadhili yeyote ambaye sio chizi..au jina kamili tumuite "fisadi mfadhili". Wewe angalia kwa makini fedha zote zinayochezewa hapa nchini..alafu bado mtu anakuongezea nyingine..they are klling you wake up sir!!! tangu taifa lipate uhuru Kiasi gani cha fedha kimeingia nchini kama misaada ya kifadhili na unajua Tumeitumiaje na tumeedelea kiasi gani..na bado tunazidi kupewa.

Kama watanzania sio Mazezeta Waaadamane kukataa miasaada na “ufadhali wa Kutupumbaza na kutufanya mazeta.”

Hoja hii haitapendwa na haitatiliwa maanani, why?

1. FISADI MFADHILI amesha capture most of Intellectuals na watamteea tu!

2. Watanzania wameshanogewa na ufadhili wa kuwanya wasiwe responsible, wasijitume, wasitumia mawazo na nguvu zao kama watu kamili..hawaoni kuwa hivyo sio sawa. Kila kukicha wimbo ni mfadhili.mfadili...ukimgusa..Unaonekana wewe ndio adui.wake up guys oneni ushenzi wa wafadhili…we will never explore our potentials!!

3. Watanzania hawajiamni..bila mfadhili bila kujiuliza hao wafadhili wana fadhiliwa na nani? Tunaogopa na hatupendi wazo la KUJITEGEMEA na wao wamedrill vichwani mwetu Hatutawezi kushi bila wao..WE ARE TOTALY BRAINWASHED. HATUONI KUWA HUO ni ugonjwa!!
 
Kuna sistah mmoja wa kizungu alikuwa anafundisha historia sekondari. Sasa historia ya Tanzania inasema wamisionari walitangulia hili wakoloni waje kutunyonya. Na yeye kama mzungu akawa anapata taabu kuelewa mtazamo wa watanzania na akawa anadai dini na ukoloni imetuletea ustaarabu.

Kuna watu wanaona misaada yao kwetu inatuletea maendeleo au ustaarabu. Lakini kwa maoni yangu misaada ni ulemavu wa akili. Nchi lazima ielewe jinsi ya kuvinjari (navigate) kutoka nje ya matatizo yake.

Kuna matatizo yanayotokana na ukweli kuwa eneo letu kijiografia linaitaji mitulinga ya nguvu kupata maendeleo.

Lakini matatizo mengine kama ya madeni, upungufu wa chakula, ufisadi hayo ni man made na nchi ni lazima ijue kutoka nje ya matatizo hayo bila misaada ya nje.
 
aiseeh kwa mwendo huu hatutafika popote,yaani leo matatizo yetu ya rushwa na uzembe tunawasingizia wafadhiri,hamko serious nafikiri na mnaongea conspiracy tuu,hiyo mikopo ya WB na IMF ni kama kupewa bure tuu maana interest sometimes ni 1-2%...inasikitisha sana wengi wanavyofikiria na badala ya kuangalia tatizo la kweli tumebaki kusingizia hata wasiokuwemo!

Koba:

Kuna mtu hapa alitoa mfano wa baba na mtoto. Wengi wetu kwa mara ya kwanza tumepewa pesa ya nguvu ni wakati tunakwenda shule (boarding). Nakumbuka sana, ilinichukua wiki mbili kumaliza pesa ya matumizi ya miezi mitano shuleni. Na nilipoandika barua ya maombi ya pesa kwa wazazi nilitoa visingizio mbali mbali lakini sikuletewa pesa za kutosha na nikaanza kujifunza mbinu za kujifunza matumizi mazuri na kuwa mvumilivu. Lakini wazazi wangeendelea ku-pump pesa inawezekana ningemaliza shule na elimu lakini nisiyejua kutumia.

Pesa za misaada zinafanya watanzania wawe watulivu na kuridhika na huduma zozote wanazopewa na serikali. Lakini serikali ikinyimwa misaada ni lazima watu watakosa huduma fulani na hata kuiondoa serikali madarakani. Na serikali itakayofuatia italazimika kujifunza kutafuta pesa na kutumia pesa (fiscal conservatism).
 
“Wafadhili wa Kimataifa wanawe fedha zinatolewa kwa nchi maskini halafu kwa kushirikiana na nza kuwa Mafisadi Wakubwa”:: Kuliko Mafisadi waliondani ya nchi kama kina Lowasa,Balali etc???

Ni nani Fisadi zaidi ya Mwingine? Mzazi anaye mpa mwanae kiasi kikubwa cha fedha ambazo atazitumia vibaya na hatimaye baadaye kumpelekea kuwa fisadi mkubwa asiyeweza kujitegemea? Ni nani fisadi zaidi ya mwingine Yule anaye Mkopesha mwenzie kiasi kikubwa cha fedha ambacho anajua fika atazichezea na kumpelekea kuwa fisadi na kuzichezea kifisadi tu!

Tuwaeleweje Wahisani na wafadhili wetu Wanojua fika kuwa Watanzania hatuna mapungufu ya kweli ya Kifedha kama tunavyolalamika; lakini wanaendelea kuzidi kutupa misaada na hatimaye tunashindwa kujitegemea.Wafadhili wetu wanaelewa Fika Kiasi kikubwa cha fedha tunachochezea kifisadi kama Kile cha BOT, ‘RICHMan’ etc lakini bado wanatupumbaza, wanaendela Kutupa misaada.

Nani Fisadi wa kweli: Yule anyekulemaza kwa ufisadi wa ndani kwa Kukupamba kwa miasaada ya kiini macho kama vile hakuna Ufisadi unaondelea nchini?

Rais amevunja baraza la Mawaziri lililojaa mafisadi. Rais hana cha kufanya kwa baraza la Wafadhili/Donors na wahisani wengine? Watanzani wazalendo wa kweli hawana cha kumshauri Rais na serekali kwa hili?

Furaha za Watanzania wanazozionyesha kwa kutikiswa kwa mafisadi wachache ndani ya taifa bila kutikiswa mafisadi wanaotulemaza kwa misaada ni kiini amcho? Ni furaha na shangwe za kitoto?

Wafadhili wa nje wakituonyesha umakini, uwajibikaji na Upendo wa kweli kwa Kutukatalia Misaada ya kijinga inayotupumbaza..Hii itatufanya kuwa makini na Fedha nyingi inayochezewa na wachache nchini?

Kama kweli tunataka kupigana na mafisadi, Tuhoja na ikibidi kukataa Baadhi ya Misaada toka mataifa mbalimbali?
misaada mingi inaaminika ni mipango ya vigogo nchi tajiri kufisidi serikali zao. fedha zinatolewa kisha kwa kushirikiana na vigogo wa nchi iliyopewa fedha fedha karibu yote inarudi ulaya huku nchi maskini ikibakiwa na deni. mashart kama vile ya ununuzi utumishi wa wataalam huwrkwa kuhakikisha hela inarudi yote ilikotoka huku nyie mnabakiwa na deni kulipwa hadi na vitukuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom