Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,132
Wafadhili wa Kimataifa wanaweza kuwa Mafisadi Wakubwa:: Kuliko Mafisadi waliondani ya nchi kama kina Lowasa,Balali etc???
Ni nani Fisadi zaidi ya Mwingine? Mzazi anaye mpa mwanae kiasi kikubwa cha fedha ambazo atazitumia vibaya na hatimaye baadaye kumpelekea kuwa fisadi mkubwa asiyeweza kujitegemea? Ni nani fisadi zaidi ya mwingine Yule anaye Mkopesha mwenzie kiasi kikubwa cha fedha ambacho anajua fika atazichezea na kumpelekea kuwa fisadi na kuzichezea kifisadi tu!
Tuwaeleweje Wahisani na wafadhili wetu Wanojua fika kuwa Watanzania hatuna mapungufu ya kweli ya Kifedha kama tunavyolalamika; lakini wanaendelea kuzidi kutupa misaada na hatimaye tunashindwa kujitegemea.Wafadhili wetu wanaelewa Fika Kiasi kikubwa cha fedha tunachochezea kifisadi kama Kile cha BOT, RICHMan etc lakini bado wanatupumbaza, wanaendela Kutupa misaada.
Nani Fisadi wa kweli: Yule anyekulemaza kwa ufisadi wa ndani kwa Kukupamba kwa miasaada ya kiini macho kama vile hakuna Ufisadi unaondelea nchini?
Rais amevunja baraza la Mawaziri lililojaa mafisadi. Rais hana cha kufanya kwa baraza la Wafadhili/Donors na wahisani wengine? Watanzani wazalendo wa kweli hawana cha kumshauri Rais na serekali kwa hili?
Furaha za Watanzania wanazozionyesha kwa kutikiswa kwa mafisadi wachache ndani ya taifa bila kutikiswa mafisadi wanaotulemaza kwa misaada ni kiini amcho? Ni furaha na shangwe za kitoto?
Wafadhili wa nje wakituonyesha umakini, uwajibikaji na Upendo wa kweli kwa Kutukatalia Misaada ya kijinga inayotupumbaza..Hii itatufanya kuwa makini na Fedha nyingi inayochezewa na wachache nchini?
Kama kweli tunataka kupigana na mafisadi, Tuhoja na ikibidi kukataa Baadhi ya Misaada toka mataifa mbalimbali?