Wafadhili mmeidekeza Tanzania, bado tunataka nyonyo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafadhili mmeidekeza Tanzania, bado tunataka nyonyo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 26, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Binamu yangu alimdekeza mtoto wake wa kwanza hadi kufikia karibu miaka minne mtoto alikuwa anakimbia kwa mama na kutaka nyonyo! Kwa kawaida viumbe karibu wengi tu huchukua jukumu la kulea vichanga vyao na katika muda wa malezi ya miaka ya mwanzo basi vinakuwa karibu sana na hao watoto wao. Kwa kadiri siku zinavyoendelea ndivyo wazazi wanajitahidi kuanza kuwafunza watoto wao kuanza kujitegemea.

  Hata hivyo katika ya vitu vyote ambavyo ni vichungu kwa mtoto na mama lakini ni vya lazima ni siku ya kumkatisha mtoto kunyonya au kumletea chakula na kumlisha. Ni wakati ambapo mtoto anatakiwa aanze kutafuta chakula yeye mwenyewe na mara kadhaa chini ya uangalizi wa wazazi ambao watahakikisha anakula chakula kizuri na bora na ambacho mwili wake mchanga unaweza kuhimili.

  Katika kuhakikisha mtoto anaacha kunyonya wanyama wanatumia namna mbalimbali. Mbwa kwa mfano, hufikia mahali humbwakia mtoto wake kila akikaribia nyonyo, na ng'ombe wao hurusha hata mateke na kumfukuza mtoto kwa pembe. Hawa wote wawili hawajifunzi mahali popote na wala hakuna tathmini ya kujua kama mtoto yuko tayari kujitegemea. Wanachofanya kimo ndani ya hulka yao kama wanyama.

  Ninapofikiria hili ninaona jinsi gani Tanzania (siwezi kuzisemea nchi nyingine) ilivyodekezwa na kuendekezwa na wafadhili kiasi kwamba hata wakati wa kuacha kunyonya ulipofika bado hatutaki kuachia nyonyo!! Meno yameshakuwa makubwa na mwili una nguvu lakini hatutaki kucheza mbali na nyonyo za "wazazi wetu" ambao tumewaita "wafadhili".

  Wafadhili hawa bahati mbaya hawatoi maziwa mazuri bali wanatoa dawa ikamatayo ya misaada ya kigeni. Sasa hivi hatuwezi kuamini au kufikiria hata kwa kidogo nini kitatokea endapo misaada hiyo itasitishwa. Cha kuudhi zaidi ni kuwa wafadhili hawa hawawezi hata kutubwekea au kutufukuza kwa pembe na kututaka tutafute chakula sisi wenyewe!

  Wafadhili hawa wanaamini kabisa kuwa tunawahitaji na ya kuwa pasipo wao "our survival chances are dim". Na sisi wenyewe hatuwezi kufikiria hata kidogo kuweza kuishi bila misaada ya kigeni na hivyo hata tukitaka kufanya lolote lile ni lazima tujiulize kama wafadhili wako tayari kutusaidia. Hakuna mradi mkubwa, na hakuna mpango mkubwa wa maendeleo ambao sisi wenyewe tunaweza kusema tutauanzisha, kuusimamia, kuufanikisha na kuuendeleza bila ya msaada wa wafadhili. Tumedekezwa tukadeka, na sasa bado tunataka nyonyo!!

  Ninachosema ni kuwa, wakati wa kutukatisha kunyonya umefika. Tayari tuna wasomi wa kutosha, tuna raslimali ya kutosha, tuna watu wa kutosha na tuna sababu za kutosha kujitegemea. Lakini zaidi ya yote tunaweza kujitegemea kwa kiasi kikubwa katika kujiletea maendeleo. Hadi hivi sasa ninachokiona ni importation of development ambapo kile tunachokiita "maendeleo" kwa kweli ni vitu tulivyocopy and paste kutoka ng'ambo! Juzi nilimsikia Waziri Mkuu akitaka watu wanunue vitunguu vya Tanzania!!! Yaani kwa maneno mengine Tanzania inaagiza hadi vitunguu kutoka ng'ambo ambayo wenyewe tunaviona ni 'bora'!

  Hatuwezi kuendelea kuagiza maendeleo kutoka ng'ambo na kuyaaita ni 'maendeleo yetu'. Development of a people can never be imported, it has to be brought forth from the people, by the people for the people!

  Napendekeza hatua zifuatazo zianze kuchukuliwa ili hatimaye na sisi tuwe katika mahali pa kutoa misaada ya kigeni kwa nchi nyingine na kuacha kusaidiwa tunavyosaidiwa sasa.

  1. Programu ya kuondoa kwa utaratibu misaada ya kigeni kwenye serikali kuu (Systematic phasing out of foreign aid).


  Tuangalie ni maeneo gani (sekta) ambayo tunaweza kuhakikisha tunayaendesha moja kwa moja kwa fedha zetu wenyewe. Binafsi naamini upande wa Ulinzi, Elimu, na Miundo Mbinu ni maeneo ambayo tunaweza kuanza nayo. Kutoka hapo tuangalie mengine na kuweka malengo yanayojulikana wazi ili ifikapo sema 2015, asilimia 100 ya bajeti ya Tanzania inatokana na fedha za ndani.

  2. Kukataa baadhi ya misaada

  Mara nyingi tumekuwa tukipokea misaada mbalimbali kwenye maeneo ambayo kwa hakika hatuhitaji. Msaada wa kuchimba visima, kujenga kliniki, au kuongeza madarasa ni misaada ya kudumaza. Kama Taifa tuwaambie wafadhili kuwa misaada yoyote ya kigeni haitapewa kwenye maeneo haya. Misaada ya mtu kuja nyumbani kwako kukuchimbia choo wakati una uwezo, sababu na raslimali za kuchimba choo hicho wewe mwenyewe ni misaada ya dharau! Misaada ya wageni kuja kutuonesha jinsi ya kusafisha miji yetu ni misaada ya kututweza!

  3. Kuelekeza misaada kwenye maeneo nyeti
  Binafsi naamini kuwa kama wafadhili kweli wanataka kutusaidia basi watusaidie katika maeneo ambayo kwa hakika tunahitaji misaada hiyo.

  - Wafungue Vyuo Vyao Vikuu kwa kutoa bid discounted tuition kwa wananchi wetu. Najua baadhi zinafanya hivyo, lakini hapa nazungumzia programs ambazo Tanzania inahitaji wasomi wengi. Zaidi ya yote, nchi wafadhili zitiwe shime pamoja na taasisi za kwao kuanzisha vyuo vyao vikuu au matawi yao nchini ili kusaidia katika kile kinachoitwa "transfer of knowledge". Na hapa nafikiria taasisi za kimataifa za utafiti wa Sayansi na Technolojia. Kwa mfano COSTECH ikiiwa na uhusiano na NASA, MIT n.k

  Hapa pia nafikiria suala la kusomesha madaktari wetu katika vyuo vyao vikuu. Au sisi wenyewe kuwa na utaratibu utakaochochea madaktari na mabingwa wa afya kuja Tanzania kufanya kazi na hawa wa kwetu, kutusaidia katika vifaa vya kisasa, na mbinu za kisasa za tiba.

  - Tatizo kubwa tulilonalo hadi hivi sasa ni kwenye udhibiti wa fedha za umma na usimamizi wa sheria. Maeneo haya kwa kweli tumeshindwa (and I mean that) kuyasimamia vizuri. Hapa kwa hakika tunahitaji msaada. Kwa hakika, ningependa kuona tunapata timu kama ya watu kutoka Japani au moja ya marafiki zetu kuiendesha Benki Kuu ya Tanzania, kuisafisha, na kuweka misingi ya kuhakikisha kuwa chembe la wingu wa ufisadi haliwezi kusikika tena.

  Yapo mambo mengine ambayo naamini pia yanawezekana. Lakini katika vyovyote tutakavyofanya, ni lazima tuweze kufika mahali kuwa "tunajitegemea". Ushirikiano wowote uliopo kati yetu na nchi za kigeni, uwe ni ushirikiano wa "walio sawa".

  Tusipofanya hivyo kwa haraka tutajikuta kuwa misaada hii ya kigeni ambayo tumeing'ang'ania katika nyonyo za wafadhili wetu inaendelea kututweza, kutudekeza na kwa hakika inatishia uhuru wetu, inabeza utu wetu, na kwa kadiri ya kwamba tunazidi kuishabikia na kuogopea kukatiwa ndivyo hivyo hivyo inaongeza utegemezi wetu wa kifikra. Ni lazima kama tunataka kupata nafasi ya kuendelea, tusimame kwa miguu yetu hata kama inatetemeka kwa kutokujiamini.

  Jamani, hata wanyama wanaachishwa kunyonya!! Nani kwetu atakuwa wa kwanza kusema "sitaki nyonyo, nataka nile chakula changu mwenyewe?"!
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji haya ni mawazo makubwa sana ambayo yanahitaji mtu mwenye mtazamo mpana kuyakubali. Nyerere aliwahi sema great ideas never die so easily...
  Bajetu yetu ilivyo, mipango mingi ya maendeleo haiwezi kukamilika bila kuwa ombaomba kila kona kwa so called donors. Imetufanya tuwe wavivu wa kutumia vichwa vyetu kufikiria.
  Cha muhimu nafikiri , ni lazima tufahamu kuwa donors hawayapi kipaumbele yote yale ambayo sisi tunaona yana umuhimu kwetu, mfano kuboresha elimu, huduma za afya na tija katika kilimo.
  Tunahitaji kubadili fikra.Donors hawataweza kutufanya tung'are katika safu za kiuchumu na kupata mabadiliko ya kweli bila sisi wenyewe kuanza dhana ya namna gani tunataka kujitegemea.
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  What spacific qualities ... makes a donor to be a donor?

  Who is the The original Donors.

  AND

  MOST IMPORTANT

  Who is the Donor of the Original Donors.

  Wanatoka Mbiguni au In the deep galaxies out there...?

  Is it destined kuwa Tanzania Can not/never qualify kuwa either Donor or original Donors?

  Nashindwa Kuelewa.

  Ni naamini kuwa ....

  Misaada yote toka kwa any kind of a donor ikikatwa to 0% By kesho asubuhi ... Tanzania isinge Perish completely! Idadi ya watanzania isingebakia sifuri...

  Tungepitia particular hardships etc.... and some would survive to bring the new race like those we call Donor of the donors!!!! Sijui njia nyingine ya kufikia ukombozi huu!!!!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Azimio.. yawezekana hatujiamini kuwa tunaweza kusimama! Nyie subirini tu muone jinsi nchi zote zilizokumbwa na majanga na zinatuzunguka zikitupita kwa kasi kama tumesimama!
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kweli tu zitatupita huku zinaenda mbio ,si unawasikia wanawake wakisema nakuzaa huku naenda mbio ,yaani hapo ni kukuonyesha jeuri tu ,na nchi hizi zilizotuzunguuka kwa kweli wameshakatiza mkondo huu wa kuwabeba mafisadi ,ni tayari wameshatupita na kutupiku.

  Serikali ikiambiwa ibadilishe katiba haitaki,ikiambiwa ibadilishe mahakama haitaki,ikiambiwa ibadilishe Muungano haitaki wakiambiwa wabadilishe tume hawataki ,sasa hayo yote si bure ni lazima kuna siri ndani yake kwa nini wanakataa kufuatilia na kubadilisha madai makuu yanayodaiwa kila siku ambayo yameonekana kuwa chanzo kikuu cha kuzorota na kuzorotesha maendeleo ya Mtanzania. Wanasubiri kitu gani ? Au wanasubiri nguvu za umma na kama wanasubiri nguvu za umma basi wajue Tanzania zipo tena zimekaa tu hazina la kufanya na kama la kufanya ni kuiondoa CCM madarakani basi muamsho mpya unatakikana ,Zanzibar wameshazifanyia try na zimeonekana zipo sasa kilichobaki ni kufanyiwa kazi na huenda 2010 ikiwa CCM itafanya manyago basi njia ni moja tu , kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu za Umma.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi bado kwa kweli nina tatizo hili la misaada ya kigeni... hivi kweli hatuwezi kuendelea pasipo hiyo? Kwanini isianze movement of "trade not aid campaign"?
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Umeongea point za maana sana.

  Ila jambo ambalo naona la muhimu pia si kukataa misaada yote bali tupokee ile misaada ambayo haiatatuathiri i mean ile ambayo haina masharti ya kutuumiza. kuna masharti mengine yanayo hatarisha our sovereighnity and we need to wake up.

  Foreign donations ni mojawapo wa chanzo cha mapato kwa taifa,lakini tujue kwamba mojawapo ya mbinu za kidiplomasia ni pamoja na kutoa misaada to secure the interest za taifa fulani,hii ni mbinu kubwa ya mataifa ya magharibi dhidi ya third world countries.We must be carefully.

  Pia,mimi naona ni bora tutegemee misada for some few years strategically.kwa mfano kupanga kwamba kwa miaka miwili tuitmie hiyo misada ktk kujenga viwanda vya ndani au miradi mikubwa yenye kutoa ajiri kwa watu wengi.After that tuachane nao.
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  This is a serious issue....misaada ni kilema kibaya......tatizo ya rinchi hiri ni kuwa kila kitu kinapelekwa kiCCM na Makambalians ndio wanaoamua destiny ya nchi.....
  ....hakuna maoni ya kitalaam yanayokuwa considered au kusikilizwa......inakera sana....


  Hapo ndipo kumekaa kitaaluma zaidi kwingine siasa nyingi.....unajua mamabo haya ukiweka siasa nyingi haki ya nani tutaishia kupiga mayowe mpaka vidole viote sugu....

  hao wafadhili mie huwa napigwa butwaa sana kuna sekta nyeti huwa hawagusi hasa sekta ya elimu.....mara nyingi hata misaada wanayotoa utasikia madawati sijui chaki na vidudu vya ovyoo ovyo..

  huyo raisi wenu juzi nimemuona akipokea wanafunzi sijui wa majuu nao yeye kashindwa kuweka na hajakutana na uongozi wa wanafunzi tanzania.....kuna kazi kubwa sana kufika......

  .........kuna mambo yanatia aibu sana yaani na huyo raisi sijui hamnazo au namna gani sijui.....ati bush alitoa vyandarau ambavyo sisi tunaweza kuchangishana na kutoa......

  contribution za kitaaluma wanaJF zinahitajika baada ya blah blah za kisiasa sasa ifikie na sisi tujiangalie jamani huyu mkwere hatabiliki hapaswi kutegemewa.....yaaani anatoka magogoni kwenda misungwi kufungua kisima cha mil 20!
   
 9. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwanakikijiji,naomba nitofautiane na wewe kuhusu misaada ya wafadhili.Kama taifa tunakua kwa muda mrefu,tofauti na mtoto wa kibinadamu.

  Tunahitaji misaada ili tukichangia na pesa zetu tuweze kukua na kulipeleka taifa mbele kiuchumi.Hebu angalia miundo mbinu iliyopatika kutokana na misaada jinsi inavyosaidia katika kusisimua biashara.Tungekataa barabara za Mwanza hadi Dar-es salaam tukawa tunapitia Kenya mikoa ya kati ingekuwa inaendelea kuwa doro.Bidahaa mabili mabali na wafanya biashara wangeendelea kupata shida.

  Misaada ya kuwapatia maji binadamu ukiikataa ni dhambi,na hasa inapokuwa uwezo wa bajeti ni mdogo.

  Halafu vipi ukubali misaada ya kuendelezwa kielimu na kukataa ile ya kuendeleza miundo mbinu?Kama taifa tunahitaji kila aina ya misaada ili ku supliment pale tunapopata mapungufu.

  Tuanachotakiwa kuzingatia si kukataa misaada bali ni kukaribisha misaada isiyokuwa na masharti au ile inayoweza kuingilia uhuru wa nchi.

  Kama nchi rafiki au mashirika ya kimataifa yannahitaji kutoa ili kuijenga nchi yetu sioni kama kuna kama kuna tatizo hapo hasaka uchumi wako ni mdogo.

  Umri wa mtu na umri wa nchi ni tofauti.Nchi inachukua mika mingi sana kuendelea na inahitaji mambo mengi kwa wakati mmoja lakini tatizo ni kuweza kujitosheleza.

  Nchi yetu ni maskini na haiwezi kuendelea bila kushirikiana na mataifa mengine ikiwaa ni pamoja na kupatiwa misaada ya kiuchumi.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Al... unakumbuka kuwa Rais Kikwete aliwaambia wafadhili kuwa fedha zilizoibwa/toweka/potea/disappear Benki Kuu siyo za wafadhili? Hivi unaamini kweli kuwa Tanzania haina fedha au uwezo wa kifedha wa kufanya jambo lolote inalotaka bila ya msaada wa wafadhili?

  Hata hivyo utajuaje uwezo kama kila siku ukiibiwa kutoka kwenye ghala lako ukiamka asubuhi unakuta magunia mengine mfadhili kayaweka. Hivi kweli utahakikisha komeo lako lipo?

  Kwa kadiri wafadhili wanaziba pengo la wizi na ubadhirifu wa fedha za Watanzania ndivyo vivyo hivyo hatuoni haja ya haraka, ya lazima na ya makusudi ya kusimamia fedha zetu, kwa sababu tunajua likitokea pengo hata kidogo tu wafadhili watatupa nyonyo tunyonye.!!

  Mimi ninaamini katika uwezo wa Tanzania na Watanzania kufanya karibu asilimi 99 ya mipango yake yote kwa uwezo wake wa ndani.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Well, Tunaweza kuendelea kabisa bila msaada.Lakini katika kufikia huko,ukilinganisha na kudumazwa kwa uchumi wetu na watu mafedhuli wasiolitakia mema taifa letu,tume-end up kwenye ufisadi na aibu.

  Hilo wazo la Trade,ni jema na lengo langu hapo juu kusema tutegemee misada for few years strategically ni katika kufikia huko.Hatuwezi kufanya trade deal without imfrustructures.So to prepare a conducive enviroment basi tutegemee hiyo bajeti ya misaada ambayo tulikua tunapunguza kuimarisha miundombinu.Pato letu la taifa halitoshi,ni bora tuitegemea ili kuongeza government expenditure,to build the ability to work,save and investing kisha tupige hatua.Hapo elimu inabidi pia ipewe kipaumbele katika government expenditure
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji tatizo sio misaada kwa utawala huu uliokuwepo ,hakuna lolote ambalo litawasaidia waTanzania hakuna,maana kama ni misaada kuletewa awamu zote zilizopita zilikuwa zikipokea misaada na yote ikiliwa ,mpaka jamaa wakasituka sasa wanaunda huko huko na kutuletea kitu mkononi na sio fedha tena na bado hicho kitu kinamegwa vilevile ,kama ni mradi mtu atafanya juu chini ili uwe wake tumeona ya Mkapa na Yona . Na ukisema tusiwe ombaomba na tusipokee misaada ndio mambo yatazidi kutukaba kisingizio kitakuwa siku hizi hakuna misaada.

  Hivyo yote haya husababishwa na utawala mmbovu na sivinginevyo nchi ikishakuwa na watawala binafsi wanaochumia matumbo yao basi kila mapato ya nchi kwanza hujitengea wao na kinachobakia wakababaisha huko kijijini , watawajengea zahanati japo haina madawa na hapo pia mtaambiwa wananchi mchangie,mtajengewa shule na hapo pia mtaambiwa mchangie kama haitoshi watakukamata na kukuhukumu eti hukuchangia ,huu kama si udikiteta ni kitu gani ?

  Na fanya pima utakavyo jawabu ni lilelile utawala mbovu na ukishakuwa na utawala mbovu huna utakaloliwaza na kuliwakilisha likafanyiwa kazi utaonekana huna la kufanya na zaidi utaambiwa Tanzania hajafa mtu kwa njaa.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Well, Tunaweza kuendelea kabisa bila msaada.Lakini katika kufikia huko,ukilinganisha na kudumazwa kwa uchumi wetu na watu mafedhuli wasiolitakia mema taifa letu,tume-end up kwenye ufisadi na aibu.

  Hilo wazo la Trade,ni jema na lengo langu hapo juu kusema tutegemee misada for few years strategically ni katika kufikia huko.Hatuwezi kufanya trade deal without imfrustructures.So to prepare a conducive enviroment basi tutegemee hiyo bajeti ya misaada ambayo tulikua tunapunguza kuimarisha miundombinu.Pato letu la taifa halitoshi,ni bora tuitegemea ili kuongeza government expenditure,to build the ability to work,save and investing kisha tupige hatua.Hapo elimu inabidi pia ipewe kipaumbele katika government expenditure
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo si misaada. Tatizo ni sisi wenyewe watanzania. Hatuna usimamizi thabiti wa kile tunachopewa kama misaada na kile tunachozalisha wenyewe.
  Ok tuseme misaada basi lakini bado hatuna management nzuri ya kile tunachopata, je tutafika wapi?. Kitu cha kwanza ni kuondoa tatizo la management kwani kusimamisha ama kuendelea kupata misaada hakutaleta tofauti kama tatizo hili halitatatuliwa.

  Unachukua maji toka mtungini (rasilimali zetu)na kuyamiminia katika kikapu na kikapu kinavujisha maji, mtungi unaishiwa maji,maji hayatajaa hata kama utatumia bahari (misaada) kujaza kikapu hicho, mpaka uvujaji ukomeshwe ndipo tutakapoweza kupata maji.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  tatizo ni kuwa kwa kadiri kuna mtu anazidi kujaza maji kwenye huo mtungi uliotoboka, na huko yanakotokea yanawafurahisha watu wachache haakuna haja ya kuziba tundu au matundu hayo. Wafadhili wakisitisha kujaza maji mtungi huo uliotoboka, ndipo sisi wenyewe tutakapoona uchungu wa kupoteza "maji yetu"..!
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Hili linatokea tunaona jinsi Rwanda inavyokuja juu. Si ajabu hata Zinbabwe miaka 10 ijayo kama wataweza kumaliza migogoro yao wanaweza kuwa wanafanya vizuri zaidi kuliko sisi. Hii inatokana na viongozi wetu kuweka mbele maslahi yao na kuwakingia vifua mafisadi.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  hakuna maendeleo yoyote mpaka pale CCM itakapoondolewa madarakani ,tusidanganyane tufanye hivi au vile,jinamizi hili linalokula uchumi wetu na kukwiba hazina pamoja na misaada ni lazima liandamwemwe na kuangamizwa , maana bora ukimwi au kensa unajua mwisho wake utafariki ,lakini gonjwa hili CCM kuuwa haliuwi na kuponyeka haliponyeki.
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya umma.na kitu kitakacholeta uamsho ni kudai katiba mpya especially kwa sasa tukielekea uchaguzi mkuu.ccm watagawanyika na hapo ndipo kwenye mwanya wa bkuimaliza kabisa
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  This was Posted on 19ThDec2006

  19th December 2006, 08:52 AM
  Mwanagenzi
  Mwanagenzi has no status.
  JF Senior Expert Member Join Date: Mon Sep 2006
  Location: Mtandaoni
  Posts: 715
  Rep Power: 24

  Thanks: 178
  Thanked 28 Times in 24 Posts
  Credits: 2,195

  Iddi Simba naye alonga!

  --------------------------------------------------------------------------------

  Bora Iddi Simba naye aseme!

  Danish aid slash a blessing-Iddi Simba

  2006-12-19
  By Guardian Reporters


  A former cabinet minister, Iddi Simba, has described the recent move made by the Danish government to reduce aid given to Tanzania as a blessing in disguise.

  Speaking during an exclusive interview with The Guardian yesterday in Dar es Salaam, he said: "In my view, the cutting of aid could be a blessing.

  If the government of Denmark, or any government for that matter, is unhappy with us about corruption, then they shouldn't link that fact with aid because I can quote many examples in the past when aid fuelled corruption."

  He said he was not saddened at all that Denmark had slashed its financial support for Tanzania.

  "So why should I be sad that (Danish) aid is being withdrawn? In fact, if you remove aid, then you remove corruption.

  So if we are serious about getting rid of corruption in our countries, let us address the root causes of corruption in our countries.

  I contend that aid facilitates corruption. So if you want to kill it (corruption), then at least kill that source (foreign aid)."

  He said the philosophy of foreign aid was not helpful to Tanzania. "As Iddi Simba, I do not believe, neither do I have faith in the significance of receiving foreign aid. I don't believe in it. I want you to understand me.

  The philosophy of aid for countries such as ours�I have no faith in it." (Read a full news feature in tomorrow's paper).

  The government of Denmark, through its embassy, had recently announced that it would reduce its general budget support to Tanzania by 20 per cent in the 2007/08 financial year.

  Among the sectors that may suffer from the move are alternative energy development, education and irrigation.

  The move results from government failure to fulfill its commitment to present long-awaited anti-corruption legislation during the last Bunge session, according to the embassy.

  Speaking to The Guardian on the same issue, the Chairman of the opposition United Democratic Party John Momose Cheyo, said he was totally against the action.

  He said: "These people! How can they do a thing like that? Is it that they want the people to go against their own government?

  When they slash aid, it is the people who are going to suffer, not the government. Their priority should be the people, not the government in power."

  He said the reasons given by the Danish embassy for reducing the aid did not hold water.

  "There must be another reason. Punishing the government does not help. Each government has got its own programme.

  If they had agreed that a draft bill should be presented in the House at a certain date, then it is not the duty of another government to press for its tabling," he added.

  Cheyo said once a donor country felt that the money it was extending for budget support was being misused, the proper step would have been to bring the issue up for parliamentary deliberation.

  "They shouldn't treat the government in that manner. If we allow donors to act in that way, then why did we fight for independence?" he asked.

  When asked by The Guardian as to why the government had failed to table the draft bill on corruption, thus earn the wrath of the Danish government, Philip Marmo, the Minister of State in the President's Office responsible for Good Governance said: "The government could not rush to table the Bill in Parliament before seeking people's views as provided for in the country's legislative programme.

  "We cannot rush the Bill to Parliament for the sake of money. We have a programme, a clear programme that guides us when the need to amend or make a new law arises."

  He said the government was still collecting people's views on amendment of the anti-corruption laws, adding that the Bill was a very crucial document, which needed to be prepared according to, laid down procedures.

  The minister said the Bill to amend the anti-corruption laws would be tabled in Parliament in February.

  "That is our story. I do not know what prompted Denmark to withdraw its support. But this is our position," he said.

  Talking about the same issue, specifically the possibility of Denmark restoring its aid level now that the government has said that it will table the draft bill on corruption in January, the Danish Ambassador to Tanzania, Carsten Nilaus Pedersen, responded: "It is too late for the government.

  It is good that they want to present the Bill to parliament now but that is contrary to our earlier agreement."

  Pedersen said they had earlier agreed with the government to present the anti-corruption legislation in the April Bunge session.

  However, the government extended the time to November this year, he said, adding that, however, despite the extension, the government had failed to fulfill its commitments to date.

  "We are serious about this. You cannot enter into an agreement and then just decide to break it up," he said.
  Denmark has a so-called 'Variable Tranche' as part of its general budget support to Tanzania.

  This means that for each financial year, 20 per cent of Denmark general budget support is linked to achievement of specific, jointly agreed performance criteria.

  The statement issued by the Royal Danish Embassy stated that Denmark and Tanzania had agreed to link 20 per cent of its general budget support to this specific indicator but the legislation was not tabled in parliament as agreed.

  Through its budget support, Denmark backs the implementation of the country's poverty reduction strategy MKUKUTA.

  Another person who responded to The Guardian on the issue was the Director of Legal and Human Rights Centre (LHRC), Helen Kijo-Bisimba, who said that the government had to respect an agreement they had reached with their Danish development partners by amending anti-corruption legislation.

  "I am wondering why the government was so quick to approve the Terrorism Act despite fierce criticism and opposition. However, it became slow on anti-corruption legislation," asked Bisimba.

  She described the decision as a challenge for the government to respect development agreements.

  "The Danish government had no alternative because their tax-payers must hold them accountable on how development money is spent," she said.

  On the other hand, she appealed to Denmark to be lenient and provide space for their development counterparts to finalize amendments on the anti-corruption bill.

  "Instead of cutting down the budget support completely, both sides (Danish and Tanzanian governments) must talk as development partners�my suggestion is that Tanzania should be given a second chance to finalize amendments on anti-corruption within a specified timeframe," said the human right activist.

  SOURCE: Guardian
   
 20. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ukiwa unaishi kwenye "projects" ni kazi sana kuhama. Nchi yetu ni "projects" ,tumezoeashwa tayari, hatuishi bila "food stamps". Food stamps zikikatwa tunalalamika kwelikweli. Its a shame !! Naona tukachukue mazuri ya Kagame tuyajaribu kwetu.
   
Loading...