Waethiopia waliokamatwa Arusha wagoma kula! - Masha kukutana nao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waethiopia waliokamatwa Arusha wagoma kula! - Masha kukutana nao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 1, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna Waethiopia kadhaa (inadaiwa wapata 100) ambao walikamatwa huko Arusha mapema mwaka huu wakiwa njiani kuelekea Afrika ya Kusini kutafuta maisha kwa kuingia nchini kinyume cha sheria na sasa wameamua kugoma kula na hali zao ni dhaifu sana. Umri kati ya vijana hao ni kati ya miaka 16 na 25.

  Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Masha na serikali ya TAnzania inaonekana haijui ifanye nao nini kwani hadi hivi sasa serikali ya Ethiopia haijaonesha utayari wa kuwapokea watuhumiwa hao wa uhamiaji haramu. Upande mwingine serikali inaonekana kudai kuwa si jukumu lao kuwarudisha hawa watu nchini mwao na ni kutokana na hilo watuhumiwa hao wameamua kugoma kula.

  Kutokana na udhaifu wao baadhi yao wanatarajiwa kukimbizwa hospitali ya Mt. Meru wakati wowote kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Waziri Masha anatarajiwa kuelekea Arusha wakati wowote ndani ya masaa 72 yajayo kujaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya wahamiaji hao.

  Fluid:
   
 2. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  amazing....

  hivi wale stow aways wanaokwenda nchi kama Sauzi na wanarudhishwa, ni nani anagharimia??

  au tufuate utaratibu wa nchi kama Sudan, Misri etc ambapo ukikamatwa unaenda tupwa jangwani after which utajiju....... wengi wanaishia kufa kutokana na joto, kukosa chakula etc...

  whichever way, lazima kimoja kifanyike....
   
 3. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Labda kama Waziri anaenda kuwabembeleza kula, lakini kama Addis Ababa wanaonekana hawako tayari kuwapokea na Dar wanasema si kazi yao kuwarudisha Ethiopia, basi tatizo la msingi, na waamuzi wahusika, hawako Arusha, bali Addis na Dar. Masha anaenda Arusha "kutafuta suluhisho la matatizo" kwa nani?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  swali zuri.. tutafahamu baada ya masaa 72 sivyo?
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  .............kwamba hakuna ubalozi wa ethiopia nchini,si ndivyo jamani?
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Sheria za uhamiaji kumrudisha mtu lazima uwe umemkamata na vitaburisho halali vya nchi husika.Kwa kawaida huwezi mrudish mtu eti kwa vile unakisia ni methiopia ama msomali
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wangewasaidia tu kuwasindikiza hao shemeji zetu hadi mpaka wa Malawi na kuwaachia wajitafutie njia zao hadi Afrika kusini. Hii mipaka ni laana tuliyorithi kwa wakoloni. Ingekuwa enzi zile za 1750 hawa wangepita tu bila pasipoti au mtu kuwauliza mnakwenda wapi.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ethiopia wanaibalozi Nairobi, Kenya na ndiyo ubalozi huo huo unaocover na Tanzania.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,550
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli Waziri Masha atakwenda Arusha kutafuta suluhisho la wahamiaji haramu hawa 100 wa Ethiopia, hiki kitakuwa kichekesho cha mwaka, nilitarajia aende Tarime kwenye mapambano, ama akashuhudie leakage ya North Mara.
  Kama ana shughguli fulani muhimu Arusha, halafu ataliangalia swala hilo kama by the way, then its fine.
  Sheria ya uhamiaji iko wazi, ukishikwa umeingia kinyume ncha sheria, ni lupango, hawa ni economic refugees, wawafunge, wakimaliza vifungo, waruhusu kuendelea na safari yao.
  Wabongo wanaorudishwa toka Bondeni, serikali hugharimia safari zao, hufikia mahabusu ya uhamiaji pale uwanja wa ndege, ndugu hutakiwa kuwakomboa kwa kurudisha gharama za serikali zilizotumika, na hapo huachiliwa.
  Wangekuwa ni Wasomali wanaokimbia mapigano nchini mwao, hii ingekuwa issue nyingine.
  Tusubiri haya masaa 72 ambayo sasa yamebakia 48.
   
 10. K

  Kaka Mdogo Member

  #10
  Jul 2, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na hili ndio tatizo kubwa la viongozi wa Tanzania. Hata vitu vya kitaalam wanavichukulia kisiasa. Kuna sababu gani ya Masha kwenda kuongea na mahabusu ambao hawataki kula. Wapeleke wataalam wa saikolojia wakaongee nao. Yeye aende Nairobi ubalozi au aende Addis Ababa akatafumbe ufumbuzi na serikali ya Addis. Hata wakigoma kula siye siyo issue yetu, tumewakamata wameingia kiharamu nchini tuwapeleke mahakamani na tuwahukumu kulingana na sheria zetu kama uwezekano wa kumaliza ili jambo kidiplomasia litashindikana.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Richard Mwangulube, MAELEZO Arusha
  WAETHIOPIA 31 kati ya 151 wanaoshikiliwa katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kufuatia afya zao kuwa mbaya baada ya kugoma kula.

  Watuhumiwa hao walikamatwa na polisi kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji baada ya kuingia nchini bila kibali wiki moja iliyopita na hivi sasa wanasubiri taratibu za kiseria kuwarejesha makwao.

  Baadhi yao walilazwa katika zahanati ya gereza la Kisongo ambao hali zao ni mbaya pamoja na Waethiopia hao kulazwa katika hospitali ya mkoa, kupewa maziwa na uji pamoja na chakula bado wamegoma kula kwa mujibu wa taarifa za wauguzi wa hospitali hiyo

  Wauguzi walisema waethiopia hao hali zao bado zinaendelea kudhoofika kutokana na hatua yao ya kuendelea kugoma kula.

  "Pamoja na kupewa uji wa maziwa na vyakula vitamu, bado waethiopita hao wamegoma kula hospitalini hapa," alisema muuguzi mmoja.

  Sababu za kugoma kula hazijawa wazi, lakini imekuwa ni kawaida kwa waethiopia wengi kukamatwa wakiwa njiani kutoka kwao kuelekea Afrika Kusini .
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,550
  Trophy Points: 280
  Kanzi ka Mwanakijiji ni mwisho. Hatimaye saa 72 za Mwanakijiji zimetimia, TBC imetangaza Waziri Masha anaondoka asubuhi hii kuelekea Arusha kusolve issue ya waethiopia.
  Huu ni uthibitisho kuwa Masha, ana matatizo, ila sio matatizo tuu, bali pia hana washauri wala hajui kupanga priorities zake.
  Mapigano ya Tarime yaliyopoteza maisha ya Watanzania 24, kwake siyo issue kubwa, akamtuma naibu wake Kagasheki, tena bora alivyokwenda Kagasheki angalau ukweli umejulikana, angeenda mwenyewe, angewakumbatia Barrick na singekubali kuchepuka kwenda kwenye ukweli.
  Kadri siku zinavyokwenda, ndipo nazidi kuamini kuna kusoma shule na kwenda shule. Kuna kuelimika na kupata vyeti, zaidi ya yote kuna na maamuzi ya busara ni kitu kingine kabisa ambacho hakihusiani na kwenda shule, vyeti wala kuelimika.
  Hiyo ndiyo timu ya askari wa miamvuli wa JK, maisha bora kwa Waethiopia.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Duh...

  Pasco naona umepiga misumari ya moto tupu halafu ya nchi sita yote kwa Lau, i hope he reads this one and understand!!!!

  The guy is just not good enough
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kuwatia kwenye ndege na pingu hadi huko kwao Ethiopia ila watu wa aina hii wakifika huko wanaweza kusema wao si waethiopia wanatoka Djibut na wakifika hukoa wakasema ni waTunisia hata waTz wakitua Uingereza wanajiita ni Wasomali ,wengine wamo humu JF.
   
 15. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kabisa kabisa hujakosea hasa nyinyi jamaa wa Pemba!
   
 16. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe Mwiba acha hizo Wa-habeshi ni wazuri. Waache waje kule kwetu Daraja -bovu si watapata wachumba tu.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mmh.. siku sauti hii itakapozimika milele ndipo mtajua ni kwa kiasi gani mlibahatika kuwa nasi.
   
Loading...