Waendesha minada hii watupiwe macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waendesha minada hii watupiwe macho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 22, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wengi wetu haswa wakazi wa mijini sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi kama masoko , vituo vya daladala na sehemu zingine za wazi watakuwa wameshawahi kuona au kushuhudia makundi Fulani ya vijana ambayo yanafanya udalali za kuuza vifaa haswa vya umeme kama pasi , tv , radio simu na bidhaa zingine ndogo ndogo .

  Mara nyingi vijana hawa huja na visingizio kwamba wameteuliwa kupiga bei vifaa hivyo kwa sababu wenye vifaa wenyewe wana madeni wameshindwa kulipa kwahiyo kampuni yao imechaguliwa kupiga mnada vifaa hivyo kwa bei ndogo na nafuu .

  Mfano dare s salaam , vikundi hivi viko vingi sana karibu kila kituo cha dala dala kikubwa utawakuta vijana hawa na vifaa vile vile wanavyouza , ajabu ni kwamba askari wa jiji wanaona bishara zile kama sio usumbufu kwa raia wengine kwahiyo wao ni sawa tu kufanya minada ile wamachinga wanaopita mitaani wao ndio kupambana na askari kila siku lakini sio hawa .

  Pia imeonekana vijana hawa wanafadhiliwa na vikundi vya wenzao wambao ndio wamejiteua kama walinzi wa vituo vya daladala wale wanaokusanya mapato ya daladala zinazopita maeneo yao au kupakia abiria kwenye vituo vyao vya dala dala .

  Zaidi ya yote wahalifu wanaonyesha sasa wanataka kujificha kwenye vipanda hivi haswa muda wa mchana kujifanya wanajishugulisha mfano halisi ni kuwaona wakiwa na vitambulisho wa kampuni hiyo ambayo haijasajiliwa .

  Hii ni sehemu nyingine ambapo viongozi wa miji na mitaa hii waangalie jinsi ya kuweza kuondokana na makundi haya ya vijana , kama wameruhusiwa kisheria kuendesha minada basi wawe na sehemu maalumu za minada sio kuhama hama mara kwa mara pia wanapofanya biashara zao leseni zao ziwe wazi , la sivyo ni kutengeneza vikundi vidogo vidogo vya vijana wavivu .

  Huwa nashangaa ninapopita naona hema moja lina watu zaidi ya 50 wamezunguka wanataka kununua simu na vitu vingine ina maana waliozunguka hawana kazi za kufanya mpaka kwenda katika midana kama ile karibu kila siku
   
Loading...