Nkungulume
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 2,988
- 1,209
Hodi wana jamvi leo nimekusudia kuongelea waendesha Pikipiki maarufu bodaboda.
Kweli hii kazi imekuwa ni msaada mkubwa wa ajira kwa vijana wetu na kurahisisha usafiri maeneo mengi ajira hii imenea nchi nzima.
Kwa mara ya kwanza ajira niliiona nchini Rwanda mwaka 1980 nikiwa safarini kwenda Bukavu inchini Zaire kwa sasa ni Kongo Kinchansa.
Na baadaye nikaona biashara hii Kampala Uganda kadri muda ulivyoenda hapa nchini kwetu wakaanza.
Kwa ujumla bodaboda wanasaidia sana kwa usafiri wa haraka kwani kwa sasa kila sehemu utawakuta.
Tatizo kubwa la hawa ndugu zetu wengi wao hawajui sheria za barabarani na kibaya zaidi hawataki kijifunza maana wao hawana kosa akipita kushoto au kulia kwao ni sahihi tu.
Na ikitokea bahati mbaya wakafanya ajali hata kama kosa ni lao wao hujichukulia sheria mkononi ili waonekane wao wako sahihi.
Kwa sababu hiyo wamekuwa ni sababu ya ajali nyingi zinazotokea na kusababisha ajali maeneo mengi na wakati mwingine kusababisha vifo na vilema vya maisha.
Kwa maana hiyo mamlaka husika tunaziomba ziwaelimishe hawa vijana kufuata sheria bila shuruti ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambazo zinaweza kuzuilika.
Nawasilisha jamvini kwa michango zaidi.