Waendesha bodaboda mnakera kulazimisha watu kupanda pikipiki zenu

Kwema ndugu zangu,

Bodaboda wana tabia za ajabu sana sijui kwanini.

Unaweza ukawa unatembea unashangaa wanakupigia honi.

Au upo njiani unatembea unashangaa boda huyu hapa "oya braza wapi" sasa nabaki najiuliza ina maana mimi sijui napokwenda au?

Leo nimeshuka kwenye gari akaja boda na pikipiki yake akanambia bro twenzetu kanikomalia kweli kweli, honi kibaoo nikamuuliza unajua napokwenda "akanambia we panda nikupeleke hadi ndani.

Nikaamua kupanda muda huo nishajipigia K Vant moja kichwa cheupeee. Tukaenda tumefika maeneo nikamwambia tayari nishushe. Nimeshuka tu akaomba mtonyo.

Nikashangaa nikahoji kivipi, akaongeza oya bro si nimekubeba nadai hela yangu bro.

Nikaongea nae kistaraabu, unakumbuka ulivyokuwa unanipigia honi alafu sijakuita kwahiyo mi najua umenisaidia tu.

Wakat anataka kushuka ikaja gari nikaingia ikaondoka.

Bodaboda mnakera sana na fujo zenu.
mimi binafsi hata kama wanatafuta riziki ila hapana too much ,
muda mwingine nabadilisha njia tu ili nikwepe usumbufu

napokaa mimi nkitoa mguu tu ,hata kichwa hakijaonekana boda kama 5 au 6 zishafika afu speed 120 breki mguuni kwangu WTF!!!!

Huwa cpandi naenda panda ya yule aliyetulia kijiweni afu nasepa ..

sikatai ni wanaume wenzangu wanaotafuta but guys this is to much....
 
Binafsi kwangu bodaboda wanamchango mkubwa sana, hizo nyingine ni changamoto tu za mazingiya yao.
Ni sawa na mwanaume ukikatisha uwanja wa fisi, malaya wanajua umeenda kuwanunua.
 
Back
Top Bottom